Hii Mikopo ya Bajaji sasa imekua kama kausha damu, tuwe makini

1.Hesabu hawarudishi kwa siku ni kwa wiki ambayo ni 194,000..
2. Bajaj ni RE kweli zinavuma kwa ubaya sababu hazipendi ujanja wetu wa kutojali vyombo vya moto.
3. Kurejesha hesabu kikubwa kila week uwaekee chao hata kama hujafikisha hiko kiasi
4. Kwangu kampuni ni bora kuliko boss wa mtaani (maboss baadhi yao wanauswahili na karaha za hapa na pale)
Bajaji za RE ni michosho bora TVS
 
Inawezekana kwa hiyo kampuni.
Nyingine inahesabiwa. Labda wao wanaitumia kama bima ya mkopo Ni vile haihesabiwi ktk marejesho.
Mkuu hiyo hela haihesabiwi...ngoma inahesabiwa 0 ukianza kuwa elfu 28000 yao ndo wanaanza kukaunti. Kianzio ni dhamana yako maana hakuna cha bure.
 
Kuna muda maisha yanakupiga na unakuta hiyo ndio the best option iliyopo . By the way hiyo option ni bora zaidi kuliko hii ya mabosi wa kitaa .

Hapo akili ya kazi ni kuhakikisha na wewe una kibubu chako unajiwekeza hata kama ni 15k kila siku.
 
Bajaji za RE ni michosho bora TVS
Michosho sababu haziendani na tabia yetu ya kutojali chombo na spea zake kuwa ghali hii imepelekea kutokuwa na soko la haraka ukitaka kuuza.. Lakini naweza kusema durability yake ni kubwa tofauti na TVS ukitaka kuamini gusa body ya TVS alafu gusa body ya RE, watumiaji wa TVS wanalalamika body kutoboka na nyingi zimeshachomolewa tofauti na RE
 
Hivi kabla haujakopa si kuna terms and conditions? Kabla haujakopa hakikisha unapewa mchakato mzima wa marejesho yatakavyokuwa mpaka unarudisha deni.
 
Utashangaa na roho yako, giza limeingia una elfu 30 wakati uliskia watu wanalaza 80
Bajaj wanapakia kama daladala siku hizi sio rahisi mpaka jioni uwe na 30,000 hata kama siku mbaya.. Nishauliza hilo majibu yao ni hesabu hukosi utakosa wewe (dereva) siku hiyo mbaya
 
Kuna muda maisha yanakupiga na unakuta hiyo ndio the best option iliyopo . By the way hiyo option ni bora zaidi kuliko hii ya mabosi wa kitaa .

Hapo akili ya kazi ni kuhakikisha na wewe una kibubu chako unajiwekeza hata kama ni 15k kila siku.
Watu wanabisha tu wanataka waone kama makampuni yananyonya raia me nawapinga sababu
1. Makampuni yapo mengi sana yanakopesha hizo bajaj inamaana mkopaji anatakiwa ajishughulishe kujua mashart yapi yatambeba.
2. Tuna kitu tumemezeshwa kwamba kuwa afsa usafirishaji ni kama umepotea kwenye ramani kumbe sio kweli ile inaweza kuwa starting point ya kwemda mbele zaidi kuliko wa ofisini.
 
Inawezekana kwa hiyo kampuni.
Nyingine inahesabiwa. Labda wao wanaitumia kama bima ya mkopo Ni vile haihesabiwi ktk marejesho.
Ndio kile kianzio kinatumika katika kulipia hizo bima, latra tra n.k
 
Ipo hivyo mkuu
Sasa kama ipo hivyo inakuwaje mtu anakuja kulalamika kama ni kausha damu? Kabla haujakopa si unaangalia kama unauweza? Let say unaambiwa tunakupa bajaji kianzio labda toa milioni 4 ,Then kila mwezi uwe unaleta laki tatu kwa muda wa miaka miwili ,haujashikiwa bunduki kuchukua sasa inakuwaje mtu aje kulalamika wakati ulipewa masharti mwanzoni kabisa?

Mimi nachojua kabla ya kuchukua mkopo kuna vigezo na masharti yapo , mkopo mzuri pale mwanzoni unapochukua ila ukishapata unaleta uzembe na hivyo kufanya ugumu kurejesha.

Madereva wa bajaji na boda wengi ni wavivu wa kufanya kazi ,akishapata elfu 10 tu anaenda kulala hafanyi kazi ,kwa mwendo huo lazima utaona ni kausha damu ,all in all mikopo ya hivyo ni mizuri kwa wanaojielewa.
 
Nakubaliana na wewe, changamoto ya hizi kazi.
1. Wanapenda sana ngono na wanawake wanajirahisisha kwa kweli
2. Kuchoka (wengi wanadai chombo kinachosha kuendesha)
3. Akili (ukiwa mkazaji pale kijiweni utaitwa wewe dhiki ndio maana upumziki)
4. Malengo madereva wengi hawana malengo ya mda mrefu wanawaza ya mda mfupi ndio maana kuna vitu wanafanya vinawatoa kwenye reli
N.B: binafsi nawaangalia zaidi hawa marafiki zangu waliochukua wapo watatu, najitahidi sana kukaa mazingira yao ya kazi nielewe kwa maana naamini ukiwa serious na hii kazi ni tundu la kutoboa
 
1.Ndiyo hivyo nilitumia tafsida tu wakishapata hela wanaenda kulala(kufanya starehe).
2.Waongo ,hakuna kazi isiyochosha ,tatizo hwajui wanachofanya ,hawajui muda gani wa kufanya kazi muda gani wa kupumzika ,hajui kusoma trend ya biashara yake ,kuna muda hakuna wateja huo muda ndiyo wautumie kupumzika.
3.Wengi ni wazushi ,waongo waongo ,inabidi wapewe elimu ,wafanye kazi kiprofessional kama Bolt/Uber ,wawe waaminifu hapo wataaminiwa na watapata kazi nyingi sana za simu .kazi za simu ndiyo zenye hela,washua hawawapi kazi za simu kwasababu waongo na lopolopo(hawana siri),si waaminifu.
4.Nakubaliana na wewe 100%.
 
Nafikili kuna mabadiliko yatatokea kwa maana zamani hizi kazi walifanya watu wasiokuwa na elimu sasa hivi adi graduate yupo field, naimani kubwa sana kuutatokea ushuhuda wa vijana kutoboa kupitia hizi kazi za usafirishaji baada ya miaka flani.
 
Back
Top Bottom