Ok ila rejesho la 28k wanaliweza.
Sina jibu la moja kwa moja kwasababu.
1. Tabia zetu waswahili za kujisifia (kusema uongo/ kupika taarifa)
2. Sijui undani wa hiyo kazi ( nakaa kijiweni nikiwa na mda/nikikutana nao ndio tunaongea)
Ila naweza kusema wanafikisha kwa sababu
1. Maisha ya kumudu gharama za kila siku
2. Hawajawahi kunyang'anywa ukishindwa rejesho wanazichukua bajaj zao
3. Week iliyopita mmoja alipata ajali ilitakiwa laki sita hakubabaika aliilipa (aligonga ukahitajika upasuaji)
4. Wanacheza michezo ( waswahili /wamama watanielewa) kwa siku 10,000 mwengine 5,000 kwa siku kama anapata excess ya 10,000 inamaana anafikisha hiyo hesabu
Siku za weekend nashindaga kijiweni nilichokiona kwa watu wanaofanya kazi hizi ni.
1. Umalaya na wanawake wanajirahisha sana
2. Kuchoka mara nyingi nawasikia wakidai kuchoka kuendesha chombo
3. Kazi inayotaka uwe na akili iliyotulia ukiwa na wenge unasababisha kitu na kitakugharimu mfano ajali
4. hawathamini pesa swala la kula 5000 mchana kwake ni kawaida, kuhonga kwa sana.
5. Vijiweni kuna watu hawana kazi wanapasiana trip ili mwenzao asikae kinyonge hii inapelekea uharibifu wa chombo na kupoteza target ya kipato kwa siku hiyo
6. Elimu ya fedha hawana hawajui cha kufanya ili kujikuza labda ndio maana wanamatumizi rafu.
NIELEWEKE: SINAMANUFAA NA KAMPUNI ZA KUKOPESHA ILA NASEMA NINAYO YAONA KWA VIJANA WENZANGU NA KUTOA MAELEZO KWA MWENYE NIA AWE NA ABC AAMUE ATLEAST AKIWA ANAFAHAMU KITU