Hii Mikopo ya Bajaji sasa imekua kama kausha damu, tuwe makini

Hii Mikopo ya Bajaji sasa imekua kama kausha damu, tuwe makini

Sidhani kama umenielewa au pengine kuna mambo unapitia maishani yanayokuvuruga ndio maana unapanik kwenye mambo madogo yanayohitaji fikra ndogo kiuchanganuzi........

Ngoja nikufafanulie....kidogo....

Serikali ndio msimamizi wa shughuli zote za kiuchumi kupitia sera, Sheria na taratibu zilizowekwa.......

Pamoja na kuwa tupo kwenye soko huria lakini pia kuna muongozo wa kuongoza shughuli hizo..........hata haya mambo ya makopo yana utaratibu wake.......kinyume na utaratibu maana yake ni utapeli.......
Ukitapeliwa ni tamaa zako zimekupeleka huko wewe unataka serikali ikufungie ndani usiende kwa matapeli?
Ni kama kusema serikali izuie watu kufanya ngono maana watapata ukimwi
 
acha wakope tu maana serikali haina mpango na raia wake, kila mtu ajipambanie mwenyewe...serikali haiwezi kopesha wala haiwezi simamia hii mikopo umiza kwa raia wake....Acha wakope waendelee kumuomba Mungu awasaidie ktk maisha yao ya hapa duniani
 
Hata kama wanatengeneza wenyewe hiyo hela ni kubwa sana hapo unaingia kwenye kitanzi cha wazi wazi. Kwanza huo ni zaidi ya wizi na unyanyasaji wa kiuchumi
Hiyo kampuni marejesho sio 28,000 ni 27,714 ambapo kwa wiki ni 194,000 faida yake ikiharibika wanatengeneza wenyewe kwa kipindi chote cha mkataba 2yrs. Kuna kampuni rejesho ni 31,200 na kila kitu ni kwa dereva.
Hii inafanyika hata kwa maboss wa mtaani na ni kawaida kabisa walio katika kiwanda hiki wanajua ndio maana kelele hamna.
Kwa kiasi flani haya makampuni yamekuwa mkombozi kwa watu kwasababu maboss wa mtaani manyanyaso yalikuwa makubwa sana kwa madereva wengine wanasubiria mkataba unataka kuisha anakutafutia makosa anakunyanganya chombo
 
Pitapita zangu maeneo ya town nikaona bango kubwa linalohusu mkopo wa bajaji na pikipiki nikaamua isiwe shida ngoja nijisogeze yaliyojiri ni kama yafuatayo;
Aina ya bajaji ni RE
Kianzio cha mkopo ni 700,000 na marejesho kwa siku ni 28,000 kwa miaka miwili inamaana hapa ndani ya miaka miwili unarejesha zaidi ya 20 milion aisee huu ni unyonyaji wa hali ya juu

Halafu nimekutana na jamaa pale ndo anatoa hiyo pesa anafurahi na kusema marejesho ya elfu 28,000 kwa siku kwake haisumbui huyu jamaa atakuja juta baadaeView attachment 3115668
Kwa mkataba huu ata mke anatoka speed Mungu tusimamie
 
Ni kama ile mikopo ya simu

Kausha damu ya mswahili hasa
 
Hawa pamoja na wanao nunua simu za mikopo akili zao zina fanana
Kuna jirani yangu mdada siku natoka job namuona duka la simu za mikopo anafuraha huyo anapiga picha ya selfie na muuzaji ( katika ununuaji wa simu za mkopo moja ya kipengele muhimu cha kupewa tambo ni lazima upige picha ya selfie na muuzaji kwa ushahidi)

Moyoni nikasema wololoyaeeeee hata mwezi haukuisha namuona na kitochi chake safi tu anadunda mchezo umemshinda.

Nb hivi vitu vya mkopo ukituliza akili utajikuta unavinunua kwa bei ya mara mbili mpaka tatu yake ni bora mtu awekeze kidogo kidogo dukani mpaka ikitimia achukue tambo
 
Back
Top Bottom