imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Hata humu jf tuanzishiwe Jukwaa la kuwa tunaambiana na kupashana habari za Barabarani.Shida ipo hapa nowadays huwa respond yao imekua ndogo sana wanasingizia wingi wa comments hivyo wanashindwa kuzisoma kwa wakati..
Kuna siku nakuja Dar nimepita Gairo ilikuwa ni usiku wa sasa nne hivi niko mdogo mdogo mara ghafla naona Gari tatu zimegongana Barabara zimefunga Barabara na hakuna alama yoyote.
Hakuna cha Traffiki wala nini ikanibidi niweke Reflector yangu na nikachukua Oanga langu na kuanza kukata majani kwa umbali wa kama mita mia pande zote
Majeruhi na Maiti tukazisomba kuzipeleka Gairo ndio kujua chanzo cha ajali Fuso ilianguka pale Jamaa walikufa wote Gari nyingine zikaja kuigonga ile Fuso na moja kutumbukia korongoni ikaja IT gari dogo Sienta nayo ikaingia chini ya Tela.
Nchi za wenzetu kila gari kubwa ina Radio call na mnapewa frequency moja kama kuna ajali amnayo imefunga Barabara na ni sehemu hatari mnaambiana.