Hii misafara ya viongozi imekuwa kero sasa

Shida ipo hapa nowadays huwa respond yao imekua ndogo sana wanasingizia wingi wa comments hivyo wanashindwa kuzisoma kwa wakati..
Hata humu jf tuanzishiwe Jukwaa la kuwa tunaambiana na kupashana habari za Barabarani.

Kuna siku nakuja Dar nimepita Gairo ilikuwa ni usiku wa sasa nne hivi niko mdogo mdogo mara ghafla naona Gari tatu zimegongana Barabara zimefunga Barabara na hakuna alama yoyote.

Hakuna cha Traffiki wala nini ikanibidi niweke Reflector yangu na nikachukua Oanga langu na kuanza kukata majani kwa umbali wa kama mita mia pande zote

Majeruhi na Maiti tukazisomba kuzipeleka Gairo ndio kujua chanzo cha ajali Fuso ilianguka pale Jamaa walikufa wote Gari nyingine zikaja kuigonga ile Fuso na moja kutumbukia korongoni ikaja IT gari dogo Sienta nayo ikaingia chini ya Tela.

Nchi za wenzetu kila gari kubwa ina Radio call na mnapewa frequency moja kama kuna ajali amnayo imefunga Barabara na ni sehemu hatari mnaambiana.
 
Humu watu wanaendekeza habari za ngono tu. Hata ukianzisha thread/jukwaa la traffic updates watatokea wapuuzi na kuuharibu uzi wenyewe wote.
 
Wewe itakuwa old skul mwenzangu, PUGU ROAD!! port access road nk
 
Nchi ikijengwa kwa misingi ya Dhulma Nchi yetu imedhulumu sana Nyumba za Watu imedhulumu Mashamba Viwanda vya watu

Hadi juzijuzi Awamu ya 5 Watu wamedhulumiwa sana.

Lakini Faraja kaja Samia na kasema wale waliodhulumiwa na Utawala wa Awamu ya 5 watarejeshewa Fedha zao na Mali zao

Kwahiyo ile Tiketi niliyopigwa kwa Dhulma pale Chamwimo niliamua kumfanyia "Kisomo" yule Trafiki siku hizi nikipita pale simuoni.
Jazakalah kheyr.
 
Wazungu husema 'silence means consent'.
Ukimya wetu watanzania umemaanisha kuridhia kila jambo tunalofanyiwa.
Kinachotugharimu watanzania ni waongeaji wazuri mno kuliko kutenda. Na hili limekuwa na faida kubwa kwa wana CCM.
Wepesi wa kulalama ndani ya JF huku ni waoga wa vivuli vyao,uzuzu umewakolea, wamepiga kelele kuhusu ajali ya moto kariakoo, mauaji ya Mtwara, ajali ya ndege ziwa Nyanza, milipuko ya mabomu yaliyoua watu wengi etc etc sasa kimiyaa wanalalama kuhusu hizi blue lights!!
 
Dodoma hapa kuanzia bungeni mpaka kisasa sheli kwa hizi siku mbili tumemuona mtemakuni
 
Wabongo ni watu wa kwenda na trend na udaku. Serikali ishajua hilo kiasi cha kulipa kina Diamond washikane matako hadharani kudivert attention kutoka kwenye mambo ya msingi.
 
Kama dua imetiki ukute mwamba anaendesha zake gari kwa kutumia mfuniko wa ndoo huku makazi yake yakiwa jalalani.
 
Kama dua imetiki ukute mwamba anaendesha zake gari kwa kutumia mfuniko wa ndoo huku makazi yake yakiwa jalalani.
Wacha nikupe siri ya wazi Temeke ina wataalam wa Visomo kama umedhulumiwa basi huwa vinafika na vingine kinasomwa leo kesho majibu.
 
Moja ya hotuba zake maarufu iliyoandikwa kwanza katika makala mwaka 1963 halafu ikajumlishwa katika kitabu chake kiitwacho 'Uhuru na Umoja' ilikuwa barua kali aliyowaandikia wenzake kuwaomba wamsaidie "Kufuta maradhi ya ukubwa" Nyerere aliandika hivi katika mwaka huo wa 1963. ". . . Na vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa vimuli muli vya polisi. Mpaka sasa, kila ninapouliza sababu ya utaratibu huu wa fahari ambao si wa kidemokrasi, nimehakikishiwa kwamba wananchi wanaupenda sana. Lakini kauli hiyo inamashaka sana. Kweli wananchi wanapenda kupigiwa makelele na kufukuzwa barabarani kwa sababu tu Raisi au Waziri au Mkuu wa mkoa amependa kutembea barabarani saa za alasiri? Lazima tuache kujidanganya. Fahari ya namna hii haina uhusiano wowote na mapenzi ya wananchi, kwa sababu ni kinyume kabisa cha demokrasi. Lazima tuikomeshe"
 
Huyo aliyejibu kuwa wananchi wanapenda itakuwa ana walakini.

Tunakubali lazima kuwe na utofauti katika misafara ya viongozi sababu za kiusalama na kiitifaki. Tatizo linakuja katika kutekeleza utofauti huo.

Panapozuiwia magari kwa lisaa lizima kwa vile mtu mmoja anataka kupita tena kipindi cha rush hour, hapo kunakuwa sio itifaki tena bali uonevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…