Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

Yani hakuna usawa kabisa.shithole Tanzania
 
Aanze kwanza kushusha mshahara wake au kutoa slip salary yake Kama alivyowadanganya wanyonge
Unataka kusema aliposema ameshusha mshahara wake ilikuwa danganya toto?
 
Sheria za mafao wanapitisha wao. Hakuna mwanadamu asiyejipendelea yeye kwanza, though hii ni too much. 5 years 230M kwa kazi ya kusifia na kupiga makofi???
Mbaya zaidi ni hao hao wabunge ndio waliipitisha hii sheria ya mafao, upuuzi tuu. Natamani kila watakapopanda kwenye majukwaa ya kampeni washushwe na fimbo za kutosha. Tumechoka viongozi wanafiki. Halafu ni hao hao walimu wanapewaga nafasi ya usimamizi kwenye chaguzi nyingi na walivyo mambulula huwa wanafata maelekezo ya kijingaaa badala ya kusimamia sheria za uchaguzi. Wacha wateseke mpaka akili ziwarudi.
 
Mkuu, haya marupurupu ya juu kwa wabunge ndiyo hasa kivutio cha wao kuwa wabunge. Endapo wangalikuwa wanalipwa kama watu wa kada zingine walio wengi wao wala wasingekubali kuifanya kazi hiyo.
 

Nina dada yangu Mwalimu amestaafu toka mwezi wa sita mwaka 2018. Mpaka leo anafuatilia mafao yake na hajalipwa. Mbaya zaidi kwa sasa anaumwa na hana msaada wowote wa kifedha.

Hapo ndipo ninapowaona wale wafanyakazi wanaoiba na kuchukua rushwa wakiwa kazini ni mashujaa. Kwa nchi hii hali ilipofikia kufanya kazi kwa uaminifu kwa kutegemea utakuja kulipwa mafao ni ujinga wa hali ya juu!!!
 
Wajinga ni sisi wananchi kukubali kudanganywa na hawa wanasiasa, inatakiwa nchi iwe chini ya wananchi na sio wanasiasa wasiojali.
Tumekuwa taifa la waoga, wanafiki na watu wa kujipendekeza kwa watawala baadala watawala wajipendekeze kwetu.
Hakuna taifa hata moja duniani lililo chini ya wananchi bali mataifa yote yako chini ya wanasiasa. Huu mfumo unaboa sana na mwisho wa siku tunajikuta tunawafanyia wao kazi na wanajineemesha
 
Kimsingi neno 'kutunga sheria' imekaa kisiasa mnoo. Kiuhalisia ni kwamba wabunge wao 'hupitisha' sheria tu. Wizara ya sheria na katiba pamoja na mamlaka zake ndo hutunga sheria. Ambao hao 'watungaji' huishia kupata 70m baada ya miaka 30.
Kwahiyo huo mchakato wa kupitisha sheria uwe unafanywa na nani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…