Pre GE2025 Hii nchi ina shida nyingi sana, ajabu CHADEMA wanaaandama kisa sheria ya uchaguzi. Kwahiyo matatizo mengine hamyaoni?

Pre GE2025 Hii nchi ina shida nyingi sana, ajabu CHADEMA wanaaandama kisa sheria ya uchaguzi. Kwahiyo matatizo mengine hamyaoni?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mimi bwana sipendi sana kuandika mambo ya siasa hizi za Bongo siku hizi sio kwasababu sipendi ila sipendi tu kuandika kuhusu hizi siasa uchwara.

Ok ni hivi, acha niandike kwa ufupi kuhusu tamko la Mbowe (CHADEMA)

Nimefikira sana kuhusu kauli na kuendelea kujifunza kuhusu mambo mengi sana juu ya siasa uchwara zilizopo Tanzania kutoka upinzani na chama tawala.

Kwenye hili la CHADEMA juu ya kutangaza maandamano yatakayoanza rasimi tarehe 24 Jan 2024 Ili kupinga miswaada mitatu ya sheria ambayo itaanza kusikilizwa hivi punde huko bungeni, ambayo miswaada yenyewe itahusu maswala ya uchaguzi, sio kosa kuhusu hilo maana nalo ni swala la msingi lakini naomba uelewa zaidi kuwa je watanzania swala la uchaguzi ndio swala pekee muhimu zaidi Kuliko mengine?

Kinachoonekana hapa ni kuwa CHADEMA hili la uchaguzi limekua tatizo au kikwazo kwao kwasababu lina msrahi kwao ya nafasi za uongozi maana wao hapo ndio wanapo patia Pesa na ulaji.

Sijaona umuhimu sana wa CHADEMA kuhitaji kutumia nguvu kubwa ya maandamano kwajili ya kutetea hili la uchaguzi, maana yapo ya maana zaidi kwa watanzania na hawakutumia nguvu kama hii wanayotaka kuitumia sasa.

Ok ni hivi....

Yapo mambo mengi sana ambayo ni matatizo makubwa kama mafuta kupanda bei, Ulaghai kwenye pembejeo, Ukatikaji wa Umeme usio na tija, Vikokotoo kwa watumishi wasio wanasiasa, Sheria mpya ya Bima ya afya, Kuwaongezea Viinua mgogo wanasia wa ngazi za juu, Sheria mbovu za kodi, Ukosefu wa ajira, na Upigaji kwenye ripoti ya CAG.

Ajabu sasa mambo haya ambayo yanawaumiza Watanzani kila leo na kuwaingiza kwenye umasikini mkubwa na kuwaacha bila matumaini ya kesho yapo na yanafahamika na wanasiasa hawa wanao jiita watetezi wa haki za watanzania lakini awajaweza hata siku moja kutoka mbele na kuitisha maandamano makubwa nchi nzima.

Wapo kimya na ikijulikana kuwa hayo matatizo yapo na yakiwatesa watanzania wanasiasa hawa hawajawahi kutumia nguvu kubwa kama hili waliyotumia ya kuitisha maandamano kupinga haya na kupigani haya.

Isipokuwa wamekaa kimya kama hayapo. Je, swali ni kwanini?

Jibu ya hili ni kwasababu hayana masilahi ya moja kwa moja kwao, ila yale ya uchaguzi yana faida ya moja kwa moja kwao, kwasababu yanawagusa wao, kwa mantiki hiyo inaonesha kuwa wanasiasa wetu hawapo kwajili ya matatizo yetu bali macho yao yanangalia chaguzi na jinsi wao watakavyo weza kushinda viti hivyo au nafasi hizo ili wapate ulaji, Wanacho Linda na kupigani ni nafasi zao na matumbo yao na sio kero za watanzania.

Kwasababu huu ndio maana niliona siasa zetu ni upuuzi mtu, hakuna mwanasiasa wala kiongozi ndani ya CCM au nje ya CCM aliyepo kwajili ya Mtanzania.

NB: Jiepushe kutumika kwajili ya matumbo na manufaa ya watu wachache ambao wemejivisha koti la uzalendo ili hali ndani yao ni matapeli wa kisiasa.

Siasa safi anza kupigania uchumi wako mwenyewe, ukiwa safi kiuchumi huto tumika na hawa wanasiasa uchwara kwa masilahi yao binafsi.

Zingatia kuwa Siasa zetu bado zinatafunwa na matumbo yenye njaa, Ulafi, Unafi, Ujinga na Undumila kuwili.

Wewe una matatizo. Unailaumu CHADEMA kwa matatizo yalitoletwa na CCM? Yani CCM unayoiabudu imeleta matatizo, ila lawama unapeleka kwa CHADEMA. Punguza unafiki.
 
Katika hilo nimewashangaa sana pia CHADEMA, umeme umekata wamekaa kimya kama hakuna kitu,
Sera ya kikokotoo wapo kimyaaaa,
Bima ya Afya kwa wote hawajasema kitu,

Leo hii Tume huru ya uchaguzi ndo wanataka tuwapiganie, aiseee mm hapana, ila wakianzisha maandamano ya Bima ya afya, Umeme, Maji humo aisee mimi nimo mstari wa pili baada ya ule wa kina Mbowe,

Punguza unafiki. Yani aliyeleta matatizo yote hayo ambaye ni CCM unamlamba miguu na ku.sujudia, ila CHADEMA wanaotaka kuandama ili kuweka mfumo mzuri wa uchaguzi unawaona wabaya . Punguza unafiki
 
Mtoa mada hajapinga maandamano point yake ya msingi kwanini linapokuja suala linalogusa maslahi ya moja kwa moja kama umeme huwakuti wakiandamana au kutumia nguvu kubwa kama wanavyofanya kwenye suala la uchaguzi?
Hana hoja na wewe unayekazia huna hoja vilevile. Ninyi ni akina nani kuwapangia vipaumbele Chadema. Wao hawajayaona hayo, wewe umeyaona, basi chukua hatua. Unadhani kuna aliyezaliwa kwa ajili yako, wewe ukae tu yeye akufanyie kila kitu? Sahau.
 
Hawa ni wanasiasa wachumia tumbo.
Chadema na Ccm ni kulwa na doto.

Sheria za uchaguzi ni maslahi yao kwani shida yao ni vyeo tu.

Wananchi tuna matatizo kibao wao hawana haja hata yakuyaongelea.
Mfumuko wa bei, Nauli juu, umeme shida, maji shida, ufisadi kila wizara. Uwajibikaji serikalini zero. Nk...
Haya yote chadema hawayaoni.
Unafiki wa hawa watu upo wazi sana.

Punguza upumbavu, Usipende kuhusisha CCM na CHADEMA. Mmejaza CCM bungeni na kwenye halmashauri na mitaani na vijijini, halafu unakuja kubinua mdomo kuhusu CHADEMA. Yani CCM yenye Rais na Mawaziri wanaotunga sera unailinganisha na CCM . Punguza ujinga.

Hujui kazi za bunge lililojaa CCM? Hujui kazi za Halmashauri zilizojaa CCM? Hujui kazi za wwnyeviti wa mitaa waliojaa CCM ?. Wote hao umewaruka unawalalamikia CHADEMA ambao hawana mamlaka yeyote. Very stupid.
 
Mtoa mada hajapinga maandamano point yake ya msingi kwanini linapokuja suala linalogusa maslahi ya moja kwa moja kama umeme huwakuti wakiandamana au kutumia nguvu kubwa kama wanavyofanya kwenye suala la uchaguzi?

Kwa hivyo ameona CHADEMA ndio wenye serikali?. CCM Ina madwani, wabunge, wakuu wa mikoa, mawaziri, Rais. Hajawaona hao? Yani CHADEMA outsider ndio kaonekana mbaya ila mwasisi wa matatizo mnaficha na kumuogopa. Acheni unafiki.
 
Mleta mada punguza unafiki kabisa. Mmejaza CCM bungeni, kwanini msiwalaumu hao wabunge wa CCM kwa matatizo yanayotokea? Bunge la kazi gani. Yani ulivyomnafiki, unajaza Wana CCM bungeni na kwenye halmashauri zote. Hawa ndio wa kuwabana wawaletee umeme na maji.

Ni unafiki wa Hali ya juu kuwachekea Mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao ni zao la CCM na kushindwa kuwabana kuhusu matatizo yenu na kuja kusubiria maandamano ya CHADEMA na kuanza kuongea unafiki. Very stupid.
 
Andiko lako unelileta kishabiki chafema wametoa sababu za kuandamana kwao moja ni maswala ya Sheria ya uchaguzi pamoja na mfuko wa bei nakadhalika
 
Wanaandamana ili kushinikiza hoja yao ya kuongeza idadi ya wabunge iwepo kwenye sheria. Ni maandamano yenye nia ovu ya kushinikiza mambo yatakayotuongezea umaskini zaidi. Baada ya kuzidiwa nguvu na kina Mdee sasa naona wanataka kulazimisha kuingiza vimada bungeni kupitia sanduku la kura. Maandamano ya Januari 24 ni maandamano haramu.
 
Punguza upumbavu, Usipende kuhusisha CCM na CHADEMA. Mmejaza CCM bungeni na kwenye halmashauri na mitaani na vijijini, halafu unakuja kubinua mdomo kuhusu CHADEMA. Yani CCM yenye Rais na Mawaziri wanaotunga sera unailinganisha na CCM . Punguza ujinga.

Hujui kazi za bunge lililojaa CCM? Hujui kazi za Halmashauri zilizojaa CCM? Hujui kazi za wwnyeviti wa mitaa waliojaa CCM ?. Wote hao umewaruka unawalalamikia CHADEMA ambao hawana mamlaka yeyote. Very stupid.
Mkuu unafikiri kwa kutumia kiungo gani?
Watanzania sio majuha km mnavyodhani. Watanzania kwa sasa wamekwisha jua kuwa hawana mtetezi. Wanasiasa waliopo wote kwa sasa ni wanafki na wabinafsi.
Mbowe tangu alipoingia kwenye maridhiano na Samia kaufyata.
Nchi imekamatwa na mafisadi maisha ya wapiga kura yapo rehani hali ni mbaya kila sekta Chadema kimya.
Huwezi ku win raia kama kwenye shida zao haupo pamoja nao.
Kuna njia nyingi kwa vyama vya siasa kuweza kuiwajibisha serikali nje ya bunge au nje ya madaraka.
Nahitimisha kwa kusema hawa ni wanafki.
Watanzania tupo km watoto yatima kwa sasa hatuna mtetezi.
 
Hawa ni wanasiasa wachumia tumbo.
Chadema na Ccm ni kulwa na doto.

Sheria za uchaguzi ni maslahi yao kwani shida yao ni vyeo tu.

Wananchi tuna matatizo kibao wao hawana haja hata yakuyaongelea.
Mfumuko wa bei, Nauli juu, umeme shida, maji shida, ufisadi kila wizara. Uwajibikaji serikalini zero. Nk...
Haya yote chadema hawayaoni.
Unafiki wa hawa watu upo wazi sana.
Hakuna popote cdm wanapokuzuia wewe kuyaongelea hayo matatizo.
 
Mim toka nimejua wao huwa hawaumii sijui wanalibdwa na sheria za kimataifa sitaki kusikia ujinga.
Mtaenda barabaran ffu wanakupiga wewe wanaawaacha wao. Unakula virungu unavunjika miguu unaishia kupewa pole
Bora nikae nyumban nile ugali wangu na watoto.waende wenyewe wakaandamane
 
Wanaandamana ili kushinikiza hoja yao ya kuongeza idadi ya wabunge iwepo kwenye sheria. Ni maandamano yenye nia ovu ya kushinikiza mambo yatakayotuongezea umaskini zaidi. Baada ya kuzidiwa nguvu na kina Mdee sasa naona wanataka kulazimisha kuingiza vimada bungeni kupitia sanduku la kura. Maandamano ya Januari 24 ni maandamano haramu.
Sawa, una dukuduku jingine kwa ufafanuzi zaidi?
 
Mim toka nimejua wao huwa hawaumii sijui wanalibdwa na sheria za kimataifa sitaki kusikia ujinga.
Mtaenda barabaran ffu wanakupiga wewe wanaawaacha wao. Unakula virungu unavunjika miguu unaishia kupewa pole
Bora nikae nyumban nile ugali wangu na watoto.waende wenyewe wakaandamane
Mkuu hayo maandamano hayatakiwi kufanywa na nyie watu mliozaliwa kuishi Ili mle ugali.
 
Hakuna popote cdm wanapokuzuia wewe kuyaongelea hayo matatizo.
Okay wasitusumbue na maandamano yao ya kudai vyeo vyakisiasa.
Na Hatuwahitaji kwenye harakati zetu za kupambana na mafisadi.
waandamane na wake zao pamoja na watoto wao maana wakipata hivyo vyeo hao ndio watakao kula nao.
 
Hakuna unayetaka ww ushiriki hayo maandamano Yao, Bali ni shobo zako tu.
 
Hakuna unayetaka ww ushiriki hayo maandamano Yao, Bali ni shobo zako tu.
Hakuna fala wakuandamana kisa nyie muingie madarakani.
Mtakula mlipopeleka mboga!
Chadema hii ni mfu.
Chadema ile iliyojengwa na Dr Slaa ndio kilikuwa chama cha watu.
Kila kulipotokea dhuruma na ufisadi chadema walikuwa na wananchi.
Sio hawa kenge maji hawa!
 
Mkuu hayo maandamano hayatakiwi kufanywa na nyie watu mliozaliwa kuishi Ili mle ugali.
Sawa. Acha mim nile ugali wang wan watoto nyie nenden mkaikomboe nchi. Ukwel ukienda barabarn family yako ndio itayopata shida.wao huwa hawapigwi
 
Sawa. Acha mim nile ugali wang wan watoto nyie nenden mkaikomboe nchi. Ukwel ukienda barabarn family yako ndio itayopata shida.wao huwa hawapigwi
Kwani Hadi sasa familia zetu zinapata Raha?
 
Kwanini wewe umezuia kuandamana mpk uwalazimishe CHADEMA waandamane kwa kitu unachopenda wewe?
 
Back
Top Bottom