Hii nchi ya UAE ina ajenda gani na nchi za Africa, kila kukicha ni wao, nini wanataka ?

Hii nchi ya UAE ina ajenda gani na nchi za Africa, kila kukicha ni wao, nini wanataka ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Hivi karibuni Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imekuwa ni nchi iliyojizolea umarufu kwenye mijadala ya nchi za Africa

Hizi ni Baadhi ya nchi

Tanzania

  • inashutumiwa kwa ununuzi wa ardhi kubwa ndani ya hifadhi za wanyamapori, wakazi wa maeneo hayo kama Wamaasai huhamishwa kuwapisha.
  • Mkataba wa DP World kusimamia Bandari ulizua mjadala mkubwa, ambapo wakosoaji walihoji kukosekana kwa uwazi na kuhatarisha kuiweka bandari chini ya udhibiti wa kigeni kwa muda mrefu.

SUDAN
  • Inashutumiwa kwa kufadhili vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi .
  • Inadaiwa kusafirisha dhahabu kinyume cha sheria kutoka Sudan

MSUMBIJI
  • imewekeza kwenye miradi mikubwa ya gesi asilia Cabo Delgado na maeneo mengine ya pwani.
  • maeneo hayo yamekuwa na changamoto za vikundi vya kigaidi kama Ansar al-Sunna

SOMALIA
  • imewekeza katika bandari na vituo vya kijeshi (hasa Somaliland na Puntland) bila ruhusa ya serikali kuu, jambo linaloonekana kama kuvunja mamlaka ya kitaifa.
  • Inashutumiwa kufadhili serikali za majimbo badala ya serikali kuu ya Mogadishu.

Jamhuri ya Afrika ya Kati
  • Ripoti zinaonyesha usafirishaji wa silaha na biashara ya madini unaohusishwa na makampuni ya UAE kwa serikali na waasi.
 
Hivi karibuni UAE imekuwa ni nchi iliyojizolea umarufu kwenye mijadala ya nchi za Africa

Hao jamaa wanataka nini ?
Wana pesa za wanajipanga kwa miaka mingi ya baadaye mbeleni watakapokuwa hawana mafuta na gesi tena, ndio maana wananua rasilimali na biashara mbalimbali kwa fujo kote duniani, wakikuta nchi ina mifumo na taasisi dhaifu kiutawala, yenye viongozi mafisadi wasio Wazalendo inakuwa nafuu na kicheko zaidi kwao.
 
siyo afrika tu, dubai ni crime capital of world, umafia wote duniani unaanzia dubai, criminals woote wamejificha huko wakituma mashambulizi kwa walengwa wao …
 
Shida yako Nini?

Au uarabu wao?
Thank you! Jamaa udini na ubaguzi umemjaa tu. Maana kama sio hilo basi angeliuliza kwa nini kila kukicha wafaransa wanzidi kujenga kambi katika nchi za afrika tena wala sio nchi ambazo waliwahi kutawala? hawezi kuuliza hilo kwa sababu hafuatilii international affairs isipokuwa anasikiliza kasumba za vibarazani tu.
 
Mafuta nowadays yanaanza kupoteza value duniani, especially with all these electric cars na solar energy innovations zinavyoibuka kila leo. Bila kuuza mafuta na gas, UAE basically iko doomed economically. So what they are doing sasa hivi ni ku-focus kwenye ku-expand influence yao, wanainvest na kukamata “fursa” kwenye nchi ambazo ni wapumbavu na viongozi wao wachumia tumbo (mostly Africa), ili waandae future ya vitukuu vyao. In short, wanatumia akili, sisi tunaona kama wanatusaidia — kumbe wanapanga kuvuna keshokutwa.
 
Thank you! Jamaa udini na ubaguzi umemjaa tu. Maana kama sio hilo basi angeliuliza kwa nini kila kukicha wafaransa wanzidi kujenga kambi katika nchi za afrika tena wala sio nchi ambazo waliwahi kutawala? hawezi kuuliza hilo kwa sababu hafuatilii international affairs isipokuwa anasikiliza kasumba za vibarazani tu.
Udini gani huo mkuu

UAE wanahusishwa na vita ya Sudan, nchi iliyojaa waislam, hapo udini utoke wapi ?
 
Wafaransa ni Wakoloni na wanyonyaji wa zamani, Wachina na Waarabu ni wanyonyaji wapya.
I hope aloanzisha uzi huu atasoma comment yako. Maana aim yake ilikuwa ni kulenga udini na ukabila tu! its ok kwake kuwa wafaransa, wachina waingereza wanaivamia afrika kila siku, lakini mwarabu NO!!!!
 
siyo afrika tu, dubai ni crime capital of world, umafia wote duniani unaanzia dubai, criminals woote wamejificha huko wakituma mashambulizi kwa walengwq wao …
Kwa mujibu wako kiongozi au siyo, au niseme kwa mtazamo wako Dubai ni crime capital of the world .. ? Toa Evidence tano juu ya hili , Tangible one Mkuu Kiongozi
 
I hope aloanzisha uzi huu atasoma comment yako. Maana aim yake ilikuwa ni kulenga udini na ukabila tu! its ok kwake kuwa wafaransa, wachina waingereza wanaivamia afrika kila siku, lakini mwarabu NO!!!!
Kuna tofauti kubwa ya wakoloni wazungu na wakoloni wa sasa Wachina na Waarabu,
Wazungu pamoja na mabaya yao angalau walituletea shule, vyuo, hospitali, reli, mazao mbalimbali na wakatuachia mfumo wa kujitawala wa jamuhuri na demokrasia tuliouharibu wenyewe baadaye. Wachina na Waarabu ni wanyonyaji wa rasilimali wakituambukiza udini na udikteta/uimla zaidi.
 
Back
Top Bottom