Hii nchi ya UAE ina ajenda gani na nchi za Africa, kila kukicha ni wao, nini wanataka ?

Na wafaransa waliovamia kijiji kimoja huko Nigeria majuzi tu na kuua wakaazi wote mleta huu uzi alisema lolote lile hapa? Huo ndio udini.
Wafaransa na Nigeria wapi na wapi mkuu, hawana hata uhusika kwenye ukoloni wa Nigeria.

Mauaji ya Nigeria yanafanywa na Bokko Haram, wamo hadi ndani y jeshi la Nigeria, wanaua wanaeshi wenzao au kuwafanyia figisu wakiona wanaua sana ndugu zao
 
Wazungu wanakomba mali za Afrika toka hata kabla nchi hazijapata uhuru,wanakomba madini mpaka leo,kule Mwadui wanachimba Almasi toka nchi haijapata uhuru mpaka leo,ila hilo huwezi kuuliza,Dhahabu wanazichota kila leo.
 
Thank you! Jamaa udini na ubaguzi umemjaa tu. Maana kama sio hilo basi angeliuliza kwa nini kila kukicha wafaransa wanzidi kujenga kambi katika nchi za afrika tena wala sio nchi ambazo waliwahi kutawala? hawezi kuuliza hilo kwa sababu hafuatilii international affairs isipokuwa anasikiliza kasumba za vibarazani tu.
Hapana haujajibu kibusara bali kwa hisia ya kidini. Somo linahusu UAE na wewe kwa akili ndogo unaongelea Ufaransa wakati haihusiki na mada basi fungua uzi maalum kuihusu Ufaransa.
 
Wafaransa na Nigeria wapi na wapi mkuu, hawana hata uhusika kwenye ukoloni wa Nigeria.

Mauaji ya Nigeria yanafanywa na Bokko Haram, wamo hadi ndani y jeshi la Nigeria, wanaua wanaeshi wenzao au kuwafanyia figisu wakiona wanaua sana ndugu zao
ndugu amka, nani aliwasiadia biafra katika civil war ya nigeria 1967 - 1970? PLease fuatilia international news, mimi sijazungumzia mauaji ya boko haram, nazungumzia mauaji ya hivi karibuni yaliyofanywa na wafaransa na kuripotiwa kwenye international news outlets duniani kote. taarifa mabazo wafaransa wenyewe wameshindwa kukanusha.
 
Hapana haujajibu kibusara bali kwa hisia ya kidini. Somo linahusu UAE na wewe kwa akili ndogo unaongelea Ufaransa wakati haihusiki na mada basi fungua uzi maalum kuihusu Ufaransa.
No, ukisoma between the line ya muanzishaji wa mada hii, lengo lake kuu ni hilo la udini, full stop.
 
Wazungu wanakomba mali za Afrika toka hata kabla nchi hazijapata uhuru,wanakomba madini mpaka leo,kule Mwadui wanachimba Almasi toka nchi haijapata uhuru mpaka leo,ila hilo huwezi kuuliza,Dhahabu wanazichota kila leo.
Aliyeleta ujamaa uliotaifisha rasilimali za nchi ni Nyerere aliyerejesha ubepari ni Mwinyi, Magufuli alipambana na kampuni za wazungu za madini, za mafuta, ardhi na utalii tofauti na awamu hii au ya JK.
 
Kuna tofauti kubwa ya wakoloni wazungu na wakoloni wa sasa Wachina na Waarabu,
Wazungu pamoja na mabaya yao angalau walituletea shule, vyuo, hospitali, reli, mazao mbalimbali na wakatuachia mfumo wa kujitawala wa jamuhuri na demokrasia tuliouharibu baadaye. Wachina na Waarabu ni wanyonyaji wa rasilimali wakituambukiza udini na uimla zaidi.
I take hujui ni kiasi gani cha rasilimali ambazo muingereza tu peke yake amezipora afrika kwa ujumla na bado anaendelea kupora inderectly katika nchi mbali mbali za afrika.
 
Kuna mahali nimesema Wazungu wakiwemo Waingereza hawahusiki kupora rasilimali Afrika?
Mimi nimekubali wazungu wamehusika kupora rasilimali Africa lakini nikakuonyesha angalau baadhi ya vitu vya maana tulivyovipata kutoka kwao, na wewe unapaswa ukubali kwamba Wachina na Waarabu ni waporaji walioibukia kwa kasi kupora rasilimali Africa( Hata hivyo Waarabu ni kama wanarudi tu kujiimarisha tena maana walikuwepo hapa kuanzia karne ya 7 mpaka ya 19 wakifanya biashara ya utumwa na kuvuna pembe za tembo na faru. Walikuwa pia wanatawala hapo Zanzibar mpaka mwaka 1964.
 
Aliyeleta ujamaa uliotaitisha rasilimali za nchi ni Nyerere aliyerejesha ubepari ni Mwinyi, Magufuli alipambana na kampuni za wazungu za madini, za mafuta, ardhi na utalii tofauti na awamu hii au ya JK.
Point yako hapa ni ipi hasa? Hayo maelezo yako unafikiri mimi siyajui hayo?

Point yangu ni kwamba mzungu anachota mali Africa from ever since ila hatusikii hii milio kama ya mleta mada,ni sawa na issue ya bandari,kuna watu walikua hata hawajui Bandari ilikua inaendeshwa na nani na kwa miaka mingapi,ila ujio wa DP World tukaanza kusikia kila milio,

Mleta mada anasumbuliwa na Islamophobia japo amejaribu kukwepa ila hilo lipo wazi kabisa.
 
Harakati za uhuru zilikuwa kumuondoa mzungu akaenda kujipanga akarudi kivingine, sijui unataka milio gani zaidi ya vita vya uhuru walivyopigana Waafrika huko Zimbabwe, Angola, Msumbiji, SA n.k!
 
ndugu amka, nani aliwasiadia biafra katika civil war ya nigeria 1967 - 1970? PLease fuatilia international news, mimi sijazungumzia mauaji ya boko haram, nazungumzia mauaji ya hivi karibuni yaliyofanywa na wafaransa na kuripotiwa kwenye international news outlets duniani kote. taarifa mabazo wafaransa wenyewe wameshindwa kukanusha.
Hakuna haja ya kuandikia mate kama wino upo, Hakuna taarifa yoyote ya Wafaransa kuua Wanigeria.

Naomba hizo taarifa za international news outlets, Punguza kuamini story za vijiweni
 
No, ukisoma between the line ya muanzishaji wa mada hii, lengo lake kuu ni hilo la udini, full stop.
Ufaransa wana historical ties na Afrika toka wakati wa ukoloni hivyo inajulikana wazi kwamba wana maslahi yao Afrika tofauti na UAE ambao hawana mafungamano kama hayo.

Hivyo basi UAE kuingia Afrika ghafla na kuunga mkono vikundi kama RSF vinavyopigana vita dhidi ya serikali ya Sudan ni jambo linalonyanyua watu kope.
 
Harakati za uhuru zilikuwa kumuondoa mzungu akaenda kujipanga akarudi kivingine, sijui unataka milio gani zaidi ya vita vya uhuru walivyopigana Waafrika huko Zimbabwe, Angola, Msumbiji, SA n.k!
Unaonekana hata hujui nini kinachojadiliwa hapa,

Kule Mwadui mzungu anapochimba Almasi kabla hata ya uhuru,ni lini aliondoka kuchimba almasi?

Kwahiyo umekubali kua mzungu alijipanga kisha akarudi kivingine,sasa mbona issue ikihusu mzungu hatusikii hii milio kama ya mleta mada?
 
Point yako hapa ni ipi hasa? Hayo maelezo yako unafikiri mimi siyajui hayo?

Point yangu ni kwamba mzungu anachota mali Africa from ever since ila hatusikii hii milio kama ya mleta mada,ni sawa na issue ya bandari,kuna watu walikua hata hawajui Bandari ilikua inaendeshwa na nani na kwa miaka mingapi,ila ujio wa DP World tukaanza kusikia kila milio,

Mleta mada anasumbuliwa na Islamophobia japo amejaribu kukwepa ila hilo lipo wazi kabisa.
Una uwezo mdogo sana wa ku analyze hali ilivyo unakimbilia mambo ya dini, Huko Sudan wanakofadhili vita, nchi iliyojaa waislam risasi zinachagua dini ?
 
Kuna mahali nimeona raia hasa wa kutoka nchi za ulaya wanapanga kuboycot biashara zozote zile ambazo zina uhusiano na UAE kwanzia mashirika yao ya ndege kama Fly Emirate,Etihad,Dubai Airways n.k, makampuni yao ya kuuza na kusambaza mafuta, na hata clubs za michezo ambazo zinafadhiliwa na mashirika yao kama Arsenal,Benfica,Real madrid,Olympic Lyon n.k

Katika huo mjadala walioongelea pia na mauaji yaliyofanyika hapa kwetu kuwa UAE wamehusika kama ambavyo wanahusika kule Sudan kuwafadhili kundi la RSF.

Yaan ule ushenzi uliokuwa unafanywa na mataifa kama France,UK na US ya kudestabilize mataifa ya dunia ya tatu yenye rasilimali lukuki sasa hivi ndio unafanywa na hawa wapumbav wa UAE sema hawafanyi kwa akili wao wanamwaga mahela tu.
 
Unaonekana hata hujui nini kinachojadiliwa hapa,

Kule Mwadui mzungu anapochimba Almasi kabla hata ya uhuru,ni lini aliondoka kuchimba almasi?

Kwahiyo umekubali kua mzungu alijipanga kisha akarudi kivingine,sasa mbona issue ikihusu mzungu hatusikii hii milio kama ya mleta mada?
Hujawahi kuona nyuzi za hapa jukwaani wakiwasema vibaya nchi za wazungu??
Hujawahi kuona hata uzi mmoja wakimshangilia Traore kuwafukuza Wafaransa Burkinafaso??
Hujawahi kuona nyuzi za malalamiko jinsi gani Tanzania hainufaiki ipasavyo na uchimbaji madini wa kampuni za kizungu?
Hujawahi kuona nyuzi za watu kumuunga mkono jiwe aliposema gesi ya kusini sio yetu ni ya wazungu?!
 
Hujawahi kuona nyuzi za hapa jukwaani wakiwasema vibaya nchi za wazungu??
Hujawahi kuona hata uzi mmoja wakimshangilia Traore kuwafukuza Wafaransa Burkinafaso??
Katika hizo nyuzi hujawahi kuona wagalatia wanamsema vibaya Traore na kua upande wa wakoloni?
 
The UAE has been more aggressive than any other outside actor. There is overwhelming evidence that it has played a major role in fuelling this brutal fight over resources, mainly by providing arms and other support to the RSF, which is accused of mass killings, sexual violence and ethnic cleansing against civilians. The UAE's top interest is Sudan's gold, but food is also a key priority. Over the past decade and a half, the country has been vying to seize control over farmland and water sources in Sudan to produce food for export.

In pursuit of its own food security, the UAE has pumped over US$6 billion into Sudan’s foreign reserves, agricultural expansion projects and a Red Sea port. As the war raged, two Emirati firms –International Holding Company (IHC), the country’s largest listed corporation, and Jenaan – were farming over 50,000 hectares there. Shortly before the war broke out, a deal was signed between IHC and the DAL group – owned by one of Sudan’s wealthiest tycoons – to develop an additional 162,000 ha of farmland in Abu Hamad, in the north. This massive farm project, backed by the UAE government, will be connect by a 500 km road to a new port on the coast of Sudan to be built and operated by the Abu Dhabi Ports Group.

Kutoka grain dot org

Back
Top Bottom