Ushauri kwa vijana,
Hii mijadala ya elimu ya Nape na Mnyika ina mafundisho mengi sana kwa vijana kama mnataka kujifunza. Wekeni siasa pembeni na jifunzeni jinsi maisha yanavyobadilika na jinsi ambavyo kushindwa jambo moja sio mwisho wa mafanikio.
Hapa inaonyesha wazi Mnyika alikuwa na uwezo mkubwa sana shuleni na bado ana uwezo mkubwa maana hata hoja zake nyingi zina mshiko. Lakini inakuwaje kwa miaka yote hiyo kashindwa kumalizia hako kadegree ambako kwa uwezo wa Mnyika ni kadogo sana? Sidhani kama muda ndio tatizo pekee, labda hata hakuona umuhimu, kitu ambacho mimi nakielewa maana hata akina BIll Gates, Jobs hawakuona umuhimu wa kubaki vyuoni wakati tayari kichwani walikuwa na uwezo wa kufanya yale waliyotaka kufanya baada ya vyuo.
Tukija kwa Nape ni wazi uwezo wake ulikuwa mdogo, hakuwa na credits za kuingia A-level. Lakini kijana Nape hakulala chini na kuanza kulia au kulalamika, badala yake aliamua kujiendeleza kwa kuunga uunga elimu. Mwisho wa siku amesoma mpaka sasa ana masters yake kwenye Public Administration. Hili ni fundisho hata kwa vijana wote waliofeli mwaka huu, tumieni elimu hiyo ya Nape kama hamasa ya kwamba kama Nape ameweza kwanini na nyie msiweze? Bila kujali umepata sifuri au division four. Elimu ya karne ya 21 bado :banplease:kijana una nafasi ya kuweza kusoma, kujiendeleza na mpaka hata kuwa profesa ukitaka. Uamuzi ni wako, kuamua kupambana au kuishia kucheka wengine. Ukipata F si unarudia?
Sisi sote tuliosoma zamani tunawajua watu wengi sana ambao form six walipata zero hata ya F zote lakini wengine sasa ni maprofesa, madaktari, wachumi nk. Kama mtu anabisha, awaangalie watu waliokuwa wanasoma PCB miaka ya 80. Utawakuta wengi pamoja na kufeli form six lakini leo wako mbali sana. Walichofanya, walijiendeleza na kufeli form six haikuwa sababu ya kuwakwamisha. Kuna jamaa mmoja juzi juzi akaniambia utani akimsema msomi mmoja maarufu wa sheria TZ kwamba alipata division zero PCB Tabora. Nilishutuka sana, sikuamini. Lakini ukweli ndio huo, kupata four au zero sio mwisho wa elimu.
Binafsi kuna vijana nimewahi kuwasaidia ambao form four walitoka na points kama hizo za Nape. Through kuwashauri na kuwasaidia, leo hii wamemaliza degree zao na wana mafanikio kwenye kazi zao.
Sawa tutumie siasa kuchekana kama kujifurahisha, lakini kwenye mioyo yetu tutambue hili ni somo tosha. Kufeli jambo mara moja sio mwisho wa dunia. Badala yake amka, jipukute na anza safari tena kwa speed hata kubwa kuliko mara ya kwanza.
Wakati wewe unacheka na kupoteza muda, wenzako wanasonga mbele.
Pamoja na maelezo haya mazuri, hii ni moja ya sababu ya kushuka kwa elimu yetu tunayoishuhudia sasa. Ni hawa hawa wanaoendesha mambo ikiwemo elimu. Je unamsemaje mtu anayefikiria kupata PhD ya mtandao ni sahihi na akajiita Dr ilimradi tu atambuliwe mpaka pale watu wanapopiga kelele ndiyo anaconda Mzumbe kuifanya formal! Unafikiri atasisitizia watu kusoma elimu inayoeleweka na kuweka msingi mzuri wa elimu. Kubwa hawa ndio walimu walioko kwenye shule zetu zinazotoa msingi wa elimu yetu. Tunahitaji mabadiliko siyo vyeti vya 'darasani'