Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Ushauri kwa vijana,

Hii mijadala ya elimu ya Nape na Mnyika ina mafundisho mengi sana kwa vijana kama mnataka kujifunza. Wekeni siasa pembeni na jifunzeni jinsi maisha yanavyobadilika na jinsi ambavyo kushindwa jambo moja sio mwisho wa mafanikio.

Hapa inaonyesha wazi Mnyika alikuwa na uwezo mkubwa sana shuleni na bado ana uwezo mkubwa maana hata hoja zake nyingi zina mshiko. Lakini inakuwaje kwa miaka yote hiyo kashindwa kumalizia hako kadegree ambako kwa uwezo wa Mnyika ni kadogo sana? Sidhani kama muda ndio tatizo pekee, labda hata hakuona umuhimu, kitu ambacho mimi nakielewa maana hata akina BIll Gates, Jobs hawakuona umuhimu wa kubaki vyuoni wakati tayari kichwani walikuwa na uwezo wa kufanya yale waliyotaka kufanya baada ya vyuo.

Tukija kwa Nape ni wazi uwezo wake ulikuwa mdogo, hakuwa na credits za kuingia A-level. Lakini kijana Nape hakulala chini na kuanza kulia au kulalamika, badala yake aliamua kujiendeleza kwa kuunga uunga elimu. Mwisho wa siku amesoma mpaka sasa ana masters yake kwenye Public Administration. Hili ni fundisho hata kwa vijana wote waliofeli mwaka huu, tumieni elimu hiyo ya Nape kama hamasa ya kwamba kama Nape ameweza kwanini na nyie msiweze? Bila kujali umepata sifuri au division four. Elimu ya karne ya 21 bado :banplease:kijana una nafasi ya kuweza kusoma, kujiendeleza na mpaka hata kuwa profesa ukitaka. Uamuzi ni wako, kuamua kupambana au kuishia kucheka wengine. Ukipata F si unarudia?

Sisi sote tuliosoma zamani tunawajua watu wengi sana ambao form six walipata zero hata ya F zote lakini wengine sasa ni maprofesa, madaktari, wachumi nk. Kama mtu anabisha, awaangalie watu waliokuwa wanasoma PCB miaka ya 80. Utawakuta wengi pamoja na kufeli form six lakini leo wako mbali sana. Walichofanya, walijiendeleza na kufeli form six haikuwa sababu ya kuwakwamisha. Kuna jamaa mmoja juzi juzi akaniambia utani akimsema msomi mmoja maarufu wa sheria TZ kwamba alipata division zero PCB Tabora. Nilishutuka sana, sikuamini. Lakini ukweli ndio huo, kupata four au zero sio mwisho wa elimu.

Binafsi kuna vijana nimewahi kuwasaidia ambao form four walitoka na points kama hizo za Nape. Through kuwashauri na kuwasaidia, leo hii wamemaliza degree zao na wana mafanikio kwenye kazi zao.

Sawa tutumie siasa kuchekana kama kujifurahisha, lakini kwenye mioyo yetu tutambue hili ni somo tosha. Kufeli jambo mara moja sio mwisho wa dunia. Badala yake amka, jipukute na anza safari tena kwa speed hata kubwa kuliko mara ya kwanza.

Wakati wewe unacheka na kupoteza muda, wenzako wanasonga mbele.

Pamoja na maelezo haya mazuri, hii ni moja ya sababu ya kushuka kwa elimu yetu tunayoishuhudia sasa. Ni hawa hawa wanaoendesha mambo ikiwemo elimu. Je unamsemaje mtu anayefikiria kupata PhD ya mtandao ni sahihi na akajiita Dr ilimradi tu atambuliwe mpaka pale watu wanapopiga kelele ndiyo anaconda Mzumbe kuifanya formal! Unafikiri atasisitizia watu kusoma elimu inayoeleweka na kuweka msingi mzuri wa elimu. Kubwa hawa ndio walimu walioko kwenye shule zetu zinazotoa msingi wa elimu yetu. Tunahitaji mabadiliko siyo vyeti vya 'darasani'
 
BUTIMBA TTC ni chuo cha ualimu lakini ni center ya kufanyia mitihani kwa wanafunzi ambao hawako mashuleni.,na hili ni kwa sababu Mheshimiwa Nape hakuwa ameendelea na sekondari kwa mtindo wa Boarding School.,kwa kuwa hakupenda kuendelea kukaa boardingi hivyo aliyasoma masomo yake ya high level akiwa nyumbani na kisha kwenda chuoni hapo kufanya mtihani wa form six.


MUONGO NAMBA MOJA NA MWISHO DUNIANI!!!! Kama umehama boarding ndo uhame na day school na pia uhame na shule. Muongo kabisa!! Njoo na uongo mwingine huu umekwama!!!
 
Nahisi hujasoma,na kama umesoma ni katika ngazi ya chini sana(kama sivyo niwie radhi). Unapoona title au status ya shule/chuo sio lazima specifically iwe kinachofundishwa ni hicho unachoona kwenye title pekee,kwa mfano TTC sio lazima iwe ualimu pekee,kuna shule zinaitwa Technical school kwa mfano Moshi Technical,Tanga,lakini kuna wanafunzi wamesoma PCB katika shule hizi,hujaelewa nini.

chicken's footprints!
 
Sasa tujadili mstakabali wa tanzania na mgwanyiko wa elimu dunia tujadili tatizo la mitaala na mfumo mbovu wa elimu linalosababisha kuzalisha watu tegemezi kwa taifa, tujadili ukosefu wa maji safi na salama kwa wakzi wa jiji la dar es saam na miji mikubwa tujadili ucheleweshwaji wa huduma za jamiii kwa wananchi na fursa za upatikanaji wa huduma nzuri kwa mlipa kodi tukomboe tanzania kwa kujadili maswala ya msingi ya tanzania
 
Sasa tujadili mstakabali wa tanzania na mgwanyiko wa elimu dunia tujadili tatizo la mitaala na mfumo mbovu wa elimu linalosababisha kuzalisha watu tegemezi kwa taifa, tujadili ukosefu wa maji safi na salama kwa wakzi wa jiji la dar es saam na miji mikubwa tujadili ucheleweshwaji wa huduma za jamiii kwa wananchi na fursa za upatikanaji wa huduma nzuri kwa mlipa kodi tukomboe tanzania kwa kujadili maswala ya msingi ya tanzania
Ni muhimu pia tujadili ukweli wa viongozi wetu.

Hapa kuna mashaka ya Nape kutumia sifa za kughushi za O level na A level.

Umesahau Ujerumani yule aliyekuwa waziri wa ulinzi Bw. Gutenberg alijiuzulu kwa kuwa PhD yake iligundulika kuwa feki?
 
Nahisi hujasoma,na kama umesoma ni katika ngazi ya chini sana(kama sivyo niwie radhi). Unapoona title au status ya shule/chuo sio lazima specifically iwe kinachofundishwa ni hicho unachoona kwenye title pekee,kwa mfano TTC sio lazima iwe ualimu pekee,kuna shule zinaitwa Technical school kwa mfano Moshi Technical,Tanga,lakini kuna wanafunzi wamesoma PCB katika shule hizi,hujaelewa nini.


Ninasema hivyo kwa sababu mimi pia nilikuwa nasoma katika Shule ya Sekondari ya Butimba, katika kipindi hicho hicho ambacho mnasema Nape alikuwa anasoma, shule hiyo inamilikiwa ama ipo chini ya uongozi wa Butimba TTC, hakukuwa na kitu kama hicho. Labda mseme kwamba, alifanya mtihani as a Private Candidate kwenye kituo cha Butimba TTC nitakubaliana nanyi, but kusema kwamba alisoma EGM hapo Butimba TTC ni upotoshaji.

n.b : Kuna uhusiano gani kati ya hoja yangu ni kiwango changu cha elimu? Mi nadhani wewe ndio haujasoma kwa sababu wasomi huwa hawajibu hoja zao kwa kutoa maneno ya kashfa. Fahamu kuwa kusoma hakukufanyi kujua kila kitu kaka!
 
Nahisi hujasoma,na kama umesoma ni katika ngazi ya chini sana(kama sivyo niwie radhi). Unapoona title au status ya shule/chuo sio lazima specifically iwe kinachofundishwa ni hicho unachoona kwenye title pekee,kwa mfano TTC sio lazima iwe ualimu pekee,kuna shule zinaitwa Technical school kwa mfano Moshi Technical,Tanga,lakini kuna wanafunzi wamesoma PCB katika shule hizi,hujaelewa nini.

Mkuu jipangeni vizuri kuhusu hili ambalo mnataka kuuamisha Umma kuwa mpo sahihi.....kuna makosa mmefanya kaaa na wenzako Nape,Mafilifili na Tandaleone litawaaacha nyakanyaka mwisho wa siku.Unachojaribu kufanya hapa ni kujaribu kupilizia Mavi Pafyum!Sorry!:rockon:
 
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
Kweli ww ni mbulula,BUTIMBA ni chuo cha ualimu na kina shule ya mazoezi inayotoa elimu ya o-level prided,mm nimesoma hapo,huyu nape alikuwa na darasa lake binafsi la A-level?,wadanganye magamba wenzako mwehu we.
 
Huu usanii wa katibu wa uenezi na Itikadi haukubaliki...

Credit 3 za kufanyia mtihani wa Form6 alizipata wapi???

Alifeli form 4 kwa kupata division 4 ya point 29. Labda muandike na shule aliyorisiti vinginevyo asingeruhusiwa kuketi kwa mtihani wa kidato cha 6. Usanii ndio kazi yenu huko CCM, kila kitu mnachakachua hata Lukuvi ana MASTER
 
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;

  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu “3” kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa –Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika “thesis” iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)
hatuhitaji siasa kwenye elimu sawa alisoma Nsumba akamaliza alipata division ngapi na ya point ngapi? Je, alisoma EGM butimba TTC kuna shule pale ya secondary au kuna chuo cha ualimu? kuhusu hizo thesis azilizo andika anaweza kutupa link ya kutuonyesha hata paper mmoja aliyopublish wakati akimaliza hata Masters yake?
 
Jamani angalieni uwezo wa Nape wa kutoa hoja kwenye video clip hii.



Ndio maana nasema, CCM ilikosea sana kumchukua mtu wa Division IV Form 4 (29 points) na elimu ya uchakachuzi iliofuata kuwa ndiye mpanga mikakati wao, na msemaji wao.

Anadhani kukasirika kunafanya point isikike zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Hivi unaelewa maana ya CV? Hii ni taarifa ya sehemu alikosomea. Ungeongeza sifa yake ya KUJICHUBUA. Tangu lini TTC wana kidato cha 5 na 6?
 
BUTIMBA ni chuo cha ualimu,mm nimesoma hapo,kina shule ya mazoezi inayotoa elimu ya o-level,haijawahi kuwepo high school pale,mm nimesoma hapo,hiyo elimu ya A-level alifundishwa na nani huyo nape?,acha kutufanya mambulula,wadanganye magamba wenzako mwehu wewe.
 
Mbona sasa sioni kama anatumia ELIMU yake kwa manufaa ya TAIFA...zaidi naona anainufaisha CCM tu!!!
 
Dah! Hii kusema ukweli imekaa kama MEMKWA pyua!
 
Back
Top Bottom