Siasa za nani alipata degree or not ,hazina mantiki kwa sasa kwani iko wazi CCM ina wasomi wengi na wenye uwezo mkubwa kuliko CHADEMA.
Upeo wa kisiasa na kitaaluma ni vitu viwili tofauti,mfano mzuri ni Dr.Kawambwa ni mtekelezaji wa objectives,hajui porojo za kisiasa ,hana sababu za kutafuta umaarufu kwenye media kama J.Mnyika na ZZK.
Miradi mingi katika wizara zote alizowahi kuongoza ameacha matunda mazuri .
Jambo la msingi,turudi kwenye maadili ya mtanzania,tuwaepushe watoto na starehe za mapema ili wawe makini ktk elimu.
Wanafunzi wengi wanatumia muda mwingi ktk starehe ndiyo maana wamefeli.
Mimi nimesoma chuo ambacho kiliweka sheria kali yakutotumia simu uwapo darasani,ukibainika ilikuwa unanyang'anywa nakupelekwa kwa Principal,wengi tulitii sheria hiyo na kuwa makini darasani.
Hiyo ni university level,lakini tulipokuwa Advance Level tulikuwa huru tukionyeshana umaarufu wa kuvaa nguo(pamba) na kuwa na mademu wengi,hakika matokeo yalikuwa ni mabaya sana licha ya wanafunzi wengi kuwa na uwezo mzuri darasani kwani nilibaini majority tuliingia tukiwa na Division One na Two lakini mambo yalikuwa kinyume kwenye Final(Wengi walipata Zero).
Facebook,Twitter,SMS kwenye SIMU na NGONO za utoto zimewafelisha watoto wetu,BUNGE liunde kamati na kuwasilisha muswaada utakao nasua akili za watoto wa kitanzania.