Hii ndio gari KABAMBE atakayopewa Mshindi wa shindano la urembo MISS LAKE ZONE

Yaani hekaheka zote za matangazo ya u- miss, hii ndiyo zawadi ya mshindi wa kwanza!!!!!!

Hongereni miss Lake zone
 
Hili gari linawafaa sana......yaani mnataka wapewe gari mupya kwa kukaa uchi!
Shubaaaaaaaaaaamit!
 
Nimejikuta nacheka mwenyewe kama chiz, hiyo ndo gari gani Bora wangeweka hata boxer ingevutia kidogo ila sio huo mkweche.
 
Daah sasa analoendea swalehe shule ... Si ndo maana wanaliwa sana hawa daah maskin
 
Mashindano yatakuwa wapi na kiingilio ni sh. Ngapi
 
hahahahaha, zawadi ni zawadi aiseee anaewaonea huruma hao wasichana basi akawanunulie gari jipya
 
Wamekanunua kwa madalali wa mtaa wa UHURU
 
😳😳 Kwani wangenunu pikipiki mpyaaa wakaiweka kama zawadi ingekuwaje!!!??? huku ni kudhalilishana kwa kweli... unatoa zawadi kuu kuu😡😡
 
Mgeni mashuhuri ni yule bwana mkubwa mfalme wa mitandao...
 
Huu ni utani na kuwadhalilisha dada zetu. Labda iwe ni photoshop na sio kweli Mamlaka zinazohusika zimetoa baraka kwa mdhamini kutoa gari yenye hali hiyo.
 
Bora hata zawadi ingekuwa mkokoteni mpya kuliko hiyo gari. Aibu sana kwa waandaji na dharau kwa washiriki.
Gari iliyochoka ndio nzuri kuanzia sababu inakuwa Na matatizo kibao unaujua umakenika Bila kwenda chuo mara breki zimepitwa,mara inachemsha ,nk ukija nunua mpya Kila kitu unajua huhitaji fundi wa kukwambia.Hao waliotoa zawadi naona wamelizangatia hilo. Cha umuhimu atembee Na box la spana namba zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…