Hii ndio hali ya Bumbuli ambayo Mbunge wake ni Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi

Wiki Ijayo tutakuwa Chalinze ili kuona Maendeleo ya hapo , Maana Mbunge wake anayeitwa Riziwan Kikwete naye alipita bila kupingwa , tutafika Rwangwa na Mtama

Hatujawahi kuogopa kulogwa
 
Wiki Ijayo tutakuwa Chalinze ili kuona Maendeleo ya hapo , Maana Mbunge wake anayeitwa Riziwan Kikwete naye alipita bila kupingwa , tutafika Rwangwa na Mtama

Hatujawahi kuogopa kulogwa
Hehe mtawekwa chupa kwenye mipododo kama wa kule
 
Ni wakati wenu Chadema kuchukua jimbo muweke lami!
Tena bila hata ya kutegemea serikali kuu,wilaya itabakiwa na mbunge mmoja tu(sio 3),mbunge huyu atapewa ziara ya kuitangaza wilaya hii ujerumani na Switzerland 🇨🇭,kitu cha kwanza ni kuitengeneza ile pass kwa juhudi za wananchi na kuongea na jiji la Capetown wapeleke wataalamu wa kujenga hizi pass (western province ndani ya SA kumejengwq pass mpaka unafurahi kuziona),pass hii itakua na look out nyingi tu,watalii kutoka ujerumani na Switzerland wataanza kuja kwa wingi na ndio watatoa ajira za kujiajiri kwa vijana wa Lushoto (kila watalii 14 kuna one job opportunity),Switzerland watasaidia kujenga zile cable cars,within 3 yrs Lushoto kutasimama,kwa sasa ni huzuni kubwa kuona nguvu kazi ya vijana inapotea na wamejikatia tamaa ya kuishi
 
Umeeleza vizuri. Lakini kwa nini kila kitu cha maendeleo katika wilaya au halmashaurI tusubiri fedha/uamuzi kutoka serikali kuu/hazina. Kama ni hivyo kwa nini tuna wakuu wa wilaya na ma-ded. Na mchango wa wananchi utaonekana wapi. Tusilaumu Waziri Makamba. Inawezekana tatizo ni kubwa kuliko uwezo wake hata kama ana nia nzuri. Tutafute chanzo cha tatizo hilo badala ya kulaumu/kushutumu watu.
 
Tusilaumu Waziri Makamba. Inawezekana tatizo ni kubwa kuliko uwezo wake hata kama ana nia nzuri. Tutafute chanzo cha tatizo hilo badala ya kulaumu/kushutumu watu.
Makamba ni kiongozi. Kiongozi akishindwa kusimamia, hasa aliyo ahidi kuwa atayafanya, lawama itamwangukia, hata kama kushindwa kwake kulikuwa nje ya uwezo wake.

Kuhusu uhusika wa serikali, huko ndiko kodi zetu zinakokusanywa. Ni haki yetu kufaidika na kodi hizo katika mambo ambayo hatuna uwezo nayo kiwilaya. Uwepo wa wizara nzima ya utalii, kusimamia shughuli zote zinazohusika na sekta hiyo, maana yake ni kwamba hawa ndio wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa shughuli hizo.
Kama tutataka kila wilaya iwe na serikali kamili inayoendesha mambo yote ya maendeleo wilayani humo, basi hatuna sabau ya uwepo wa hili liserikali kuu litakalokuwa linatumia pesa za wananchi tu bila ya kufanya kazi yoyote wilayani.
 
CCM haijawahi kumiliki ofisi,imepora,

Itawezaje kujenga barabara kweli?
Eti kwamba CHADEMA ndio ije kujenga Ofisi zake kwa siku 14 baada ya kushika madaraka? Mbula. Ina maana gani hiyo?

Barabara wanajenga CCM?🤔😌
 
Hao wakazi ndio wanaojenga Barabara? Au Serikali huweka miundombinu ili kuchochea maendeleo?
Ukisoma vizuri, kwa kutulia utaona nimeandika kwamba mbunge hupeleka taarifa ili serikali ikatatue, hata barabara nimetaja.
 
Dah wewe uliyeleta uzi ni mchawi chawi kabisa. January hahusiki na mabarabara kabisa.
 
Botswana naona inasifiwa sana hii nchi.
 
Botswana naona inasifiwa sana hii nchi.
Hawa ni watu wachache sana, lakini viongozi wao wamejua jinsi ya kutumia raslimali zao kuu, hasa mbili: Almas na ng'ombe vizuri sana.
Kubwa zaidi, hawana uvumilivu hata kidogo na ufisadi.

Hata sisi, pamoja na wingi wetu huu, raslimali tulizo nazo zingeweza kutusukuma mbele zaidi na kwa haraka, lakini tunakwazwa sana na CCM. Kazi kubwa wanayoifahamu siku hizi hawa watu ni kupeana ulaji tu, na kupewa "kamba ndefu" ili wale kwa urefu wa kamba zao. Hebu tazama teuzi zinavyofanywa siku hizi, hakuna cha 'merit' wala nini, sifa kubwa ni kuwa "chawa" au unategemewa kufaidisha hao wanaokuteuwa ili waendelee kukaa madarakani; akina Makonda ni mfano mzuri hapa.

Botswana hawana mchezo na elimu yao, kama tunavyofanya sisi hapa. Watu wanamaliza kidato cha nne, utadhani ndiyo kwanza wamemaliza shule za primari! Chuo kikuu, sitaki hata kulinganisha.

Mambo ni hivyo hivyo hata Namibia. Si uliwahi kusikia kisa cha Balozi wetu aliyeteuliwa kwenda kutuwakilisha huko; balozi aliyemshangaza hata Rais wao kapelekwa kufanya kazi gani huko!
 
Acha porojo .weka ushahidi kuwa hiyo ni barabara ya Bumbuli.maana wewe kwa uongo na kubandika picha za kuokoteza unapenda sana .
Jibu hiyo hoja ya lissu kuhama chadema kisha tuambie huwa habari unaokoteza wapi maana kuna hii pia ya bashite kuongea na waandishi wa habari pia uliinya wewe
 
kiongozi makini hujali taifa kwa ujula

hata mwalimu hakusukumiza mandeleo butiama pekee
Mwalimu hakuchaguliwa na watu wa Butiama, bali alichaguliwa na Watanzania wote. Januari ni Waziri kwa sababu alichaguliwa na watu wa Bumbuli. Aliwaandikia kijitabu cha kiingereza akiwaahidi kuwaletea maroli ya barafu ili wawe wanasafirisha matunda yao kupeleka kwenye masoko Dar, na vile vile kuwanunulia hisa New York Stock Exchange
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…