Hii ndio kazi 'Critical' wanayoweza kufanya UVCCM kwa sasa kulisaidia taifa sasa na baadae

Hii ndio kazi 'Critical' wanayoweza kufanya UVCCM kwa sasa kulisaidia taifa sasa na baadae

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
Kwa sasa, kazi ya msingi inayofanywa na UVCCM ni kupongeza kazi nzuri zinazofanywa na serikali chini ya Mhe. Rais Mama samia.

Jambo wanalofanya ni zuri kwa kuwa ni kweli kuna kazi nzuri na kubwa zinazofanyika. Aidha, ni muhimu kwa kuwa mtu anapofanya jambo jema na akapongezwa, hiyo ni incentives kwake kufanya mambo ya maana zaidi na asipopongezwa taratibu huvunjika moyo na kurudi nyuma. Hivyo kwa hili wanafanya jambo jema.

Hata hivyo pamoja na umuhimu wa kazi hiyo wanayofanya; kwa kufanya kazi hiyo tu na kuishia hapo ; wanakuwa wanatumia uwezo wao chini ya kiwango sana (under utilize their potencials/ capabilities).

Tunaweza kusema labda wanatumia uwezo wao kwa 1℅ na 99℅ wanaacha kuitumia iko idle na hii sio tu kwamba ni hasara kwa chama na kwa taifa bali pia ni hatari kwa namna fulani sasa na baadae.

Inaendelea...
 
Kimsingi kazi ya kupongeza/ kusifia vitu (pamoja na uzuri wake) haihitaji kufikiri kama ambavyo kazi ya kukosoa/ kupinga haihitaji kufikiri.

Kwa lugha nyingine kazi hizi ni rahisi sana na zinaweza kufanywa na mtu yoyote tu. Kwa lugha nyingine ni kazi rahisi ambayo anayeifanya hufanya huku ubongo wake ukiwa umerelax kabisa.

Kwa bahati mbaya ni kwamba ubongo ulivyoumbwa, hakuna kukua kwa uwezo/ubora wa kufikiri kwenye vitu rahisi rahisi hali vitu vinavyo mlazimisha mtu kufikiri sana ( there is no growth in a confort zone).

Aidha, Kwa kuwa uongozi ni uwezo mkubwa wa kufikiri, kuwa na vision na kutatua matatizo complicated , na kwa kuwa malengo ya jumuia za vijana kwenye vyama vya siasa ni kufua vijana kifikra kuwaandaa kuwa viongozi bora, hatamaye hali tajwa hapo juu huchelewesha kufikia lengo mahususi mapema.

Inaendelea.......
 
Vile vile ikumbukwe kuwa kiongozi bora ni yule mwenye fikra nzuri zinazotatua matatizo ya watu.

Fikra nzuri au mbaya ni matokeo ya mchakato ndani ya akili ya mtu. Na mchakato huo huathiriwa na vitu mtu anavyoingiza kichwani.

Kwa lugha nyingine ubongo wa mtu ni kama kiwanda au computer ambapo huchakata vitu mtu anavyoingiza kichwani mwake na kutoa 'output' ambayo ni mawazo/ fikra za mtu ( mbaya au nzuri ).

Kwa mantiki hiyo mawazo/fikra za mtu huamuliwa na ni input gani ambayo mtu huingiza kwenye ubongo wake ili ichakatwe. Kama unaingiza makorokoro, ubongo unachakata makorokocho na kutoa makorokoro.

Kama unaingiza vitu vya maana, ubongo unatoa vitu vya maana na kama huingizi kitu ume relax (confort zone) kiwanda kinazunguka tupu. Yaani ni sawa na youtong inatembelea bila abiria huku inachoma mafuta.

Inaendelea.......
 
Kwa kuwa lengo la jumuia za vijana ndani ya vyama vya siasa ni kuandaa viongozi bora, na

Kwa kuwa viongozi bora ni wale wenye fikra nzuri za kutatua matatizo magumu, na

Kwa kuwa fikra za mtu hutegemea ni nini anaingiza kwenye kichwa chake na kwa kadiri anavyofikiri zaidi ndivyo uwezo wake wa kufikiri unavyoongezeka na kinyume chake, na

Kwa kuwa jumuia hizi sio watendaji wa moja kwa moja kusema watasimamia miradi;

Ni muhimu pamoja na kupongeza kazi nzuri zinazofanywa; wakaanzisha program za mafunzo yanayolenga kujengea vijana uwezo wa uongozi na kuboresha mitizamo yao juu ya dunia na maisha.

Hii itasaidia kulifikia kwa haraka zaidi lengo la kuandaa viongozi bora wa baadae. Vinginevyo kuna hatari inakuja mbeleni ukitizama kwa makini unaweza kuing'amua.
 
Ikumbukwe kuwa mtu kujiunga na chama cha siasa au jumuia ndani ya chama cha siasa peke yake, hakutoshi kumfanya mtu huyo awe kiongozi bora: bali fikra za mhusika ambazo huamuliwa na nini huingiza akili mwake amma kupitia mafunzo, uzoefu, na.k

Kosa tunalolifanya ni kudhani kuwa watu wakishajiunga na chama/jumuia tayari washakuwa na uwezo wa uongozi ambapo kimsingi haipo hivyo.
 
Mbona unapost mwenyewe, unacomment mwenyewe tena?!!
Kwa sababu nilikuwa sijamaliza hoja yangu. Vile vile wanao comment kama wewe wanakwepa hoja wanakimbilia kwa mwenye hoja.

Vile vile usiwe unafanya vitu kwa kuwa watu hufanya bali fanya kwa kuwa ni sahihi na muhimu hata kama hakuna anayefanya au kukuunga mkono.
 
UVCCM fufueni SUKITA na Mashamba yenu pale Ihemi.

Uwanja wa Samora Iringa mmezungusha fremu ila mnesahau kuweka choo ( Akili hamna).

Vibanda vya kitimoto pale Iringa vipo zaidi ya mia Ila choo kimoja. ( najiuliza hivi hawa UVCCM huwa hawanyi au kukojoa)??? Au mnataka wateja waendelee kuchafua mazingira?
 
Unachosha akili yako bure..uvccm hakuna mwenye akili wengi ni wachumia tumbo..wazee wa ndio mzee hawana critical thinking wapo kama mazuzu.

Wanasubiri beat ili waingize voko...sio kupe sio chawa ni mazezeta flan hivi.

Hata chama kimewapuuuza sasahivi wanatumika kwa maslahi ya vigogo wa chama ili kufikia malengo yao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Uzi ni wake nawewe anzisha wako uwasifie mataga jambo lamama
Halafu pia vitu vya msingi wachangiaji huwa hamna. Hata ukienda sehemu yenye VIP na Regular, unaweza ukakuta VIP kuna watu wawili lakini Regular kuna watu 3000 hata kupumua shida. Watu wengi wanapenda vitu cheap cheap iwe ni mijadala au vitu tangible.
 
Mbona mkuu ni kama mwendelezo wa bandiko na wala siyo kwamba jamaa anakomendi mwenyewe? Ila watu wanaandika jamani duh, huo muda mwautoa wapi?
Huwa kila mtu hupata muda kwa vitu ambavyo vina matter kwake. Mfano mimi nashangaa mtu anapata watu muda wa kufuatilia movie, kuangalia tv au kujua wasanii wote duniani? Ishu ni kwamba kila mtu hupata muda kulingana na vipaumbele vyake.
 
Unachosha akili yako bure..uvccm hakuna mwenye akili wengi ni wachumia tumbo..wazee wa ndio mzee hawana critical thinking wapo kama mazuzu.

Wanasubiri beat ili waingize voko...sio kupe sio chawa ni mazezeta flan hivi.

Hata chama kimewapuuuza sasahivi wanatumika kwa maslahi ya vigogo wa chama ili kufikia malengo yao.

#MaendeleoHayanaChama
Tatizo ni kwamba jamii yetu ina watu wengi wenye uelewa na fikra zenye utata mkubwa. Watu hao hao ndio huingia kwenye vyama vya siasa randomly.

Na kwa bahati mbaya hakuna mikakati mahsusi ya kuwajengea uwezo na kuboresha mitizamo yao. Assumption ni kuwa wakiingia humo, automatically washapata sifa ya kuwa viongozi bora, lakini kiuhalisia mambo hayapo hivyo.

Sasa tunafanyaje mkuu?, kwa sababu mifumo ya kufikiri ya watu (wanasiasa/viongozi) specifically ndio huamua hatma ya taifa.
 
Back
Top Bottom