Wahindi na wachina wananyanyasana hata wao kwa wao, Wahindi wana kitu kinaitwa "castes", kuna castes tano wanaamini wahindi weusi na watu weusi ni daraja la mwisho kabisa hawana tofauti na watumwa, hawaruhusiwi kupanda farasi, hawaruhusiwi kuingia kwenye mahekalu ya dini za kihindi, n.k.
Kuhusu ukabila kwenye biashara binafsi tushukuru nchi yetu ina ukabila wa chini, Kwenye biashara binafsi maboss hupenda kuwaweka watu wa karibu wanaowajua na kuwaamini ambao mara nyingi huwa ni ndugu, watoto wa shangazi, binamu, n.k. kama ni kampuni kubwa kuna nafasi kwa wengine bila kujali sana kabila.