Hii ndio Orodha ya makundi ya watu wanaohitaji Katiba Mpya na wasiohitaji

Hii ndio Orodha ya makundi ya watu wanaohitaji Katiba Mpya na wasiohitaji

HII NDIO ORODHA YA MAKUNDI YA WATU WANAOHITAJI KATIBA MPYA

Na, Robert Heriel

Mjadala unaoendelea katika Siasa mitandaoni ni ishu ya Katiba.

Wanaohitaji Katiba Mpya wamegawanyika katika makundi Yafuatayo;

1. Wanasiasa hasa wa vyama vya Upinzani

2. Wanasiasa upande wa Zanzibar.

3. Wanaharakati wa mrengo wa kiliberali.

4. Wasomi wenye elimu kuanzia stashahada mpaka uzamivu. Wenye exposure ya dunia na wenye kutaka mabadiliko kwenye nchi.

Kiuchunguzi makundi hayo ukiyajumlisha ili upate idadi kamili basi ni wazi ni asilimia 20% tu ya Watanzania wote.

Makundi yasiyohitaji Katiba mpya na wala yasiyojishughulisha kama kujua kinachoendelea;

1. Wanawake wengi hapa nchini hawana mpango na ishu za Katiba mpya wala hawalijui Katiba ya zamani.

2. Vijana wa umri chini ya miaka 40 ambao wanaelimu ya chini na Hali zao za kimaisha ni duni. Hawa ukiwakuta kijiweni ukileta mambo ya Katiba mpya ndio utavuruga kila kitu. Kwanza hawatachangia mada. Kundi hili mada zake ni Udaku, mpira, kisha Diamond na Ally Kiba

3. Wana CCM
Kundi hili lipo lipo, hili ni Kama bendera, Inategemea serikali itakapoegemea. Serikali ikisema Katiba mpya ndio, nalo linasema Katiba mpya ndio, serikali ikisema hapana, nalo linasema hapana.

4. WAZEE Hasa wenye miaka kuanzia 60+
Kundi hili litasimama upande serikali ilipo. Kundi hili sio la kulaumiwa Kwa sababu wengi wao elimu Yao ni duni, exposure ya dunia iendavyo pia ni hafifu.

Kundi hili lisilohitaji au kujishughulisha na masuala ya Katiba ndilo kundi lenye watu wengi zaidi, karibu 80% hawana mpango wa Katiba mpya wala hawajihusishi na Siasa.

Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa Watanzania wengi wanaamini katika serikali iliyopo madarakani, wanaiheshimu na kuigopa.
Hivyo serikali ikisema No! Basi watu nao watasema No!

Hata hivyo, uchunguzi wangu umebaini kuwa Watanzania wengi ni WANAFIKI, Unafiki wa Watanzania waliowengi unachangiwa kwa kiasi kikubwa cha Umasikini,
Ulimbukeni,
Elimu duni,
Woga na kujikomba Kwa wenye mamlaka.

Aidha Kama nilivyoeleza kwenye andiko langu lililopita ni kuwa, wanaodai Katiba mpya ni Kwa sababu ya mapungufu ya Katiba hii ambayo yanawafanya wasinufaike na Nchi yao.

Na wanaccm wengi wao hasa watawala, hawaoni Upungufu wa Katiba iliyopo hivyo inawanufaisha.

Kundi la mwisho ambalo ni wananchi ambao hawapo upande wowote hawa ni Bora liende, maisha yasonge, mauti ije, kaburini wafukiwe.

Binafsi, ninahitaji Katiba mpya itakayonufaisha makundi yote ya wananchi wa TANZANIA.

Hata hivyo, Siwezi kataa kuwa ndani ya jamii yangu, wananchi wengi hawana habari na Katiba mpya kwani wao ni Bora maisha siku ziende.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
Kwakuwa wana CCM ni wengi. Kwakuwa vijana chini ya miaka 40 na wenye kipato duni ni wengi. Kwakuwa wazee wa miaka zaidi ya 60 ni wengi na kwakuwa akina mama ni wengi, basi mjumuisho wao inaonesha wasiotaka Katiba Mpya ni WENGI SANA! Hivyo basi, wanaodai Katiba Mpya ni wahuni wachache ambao hawatakiwi kuyumbusha mawazo ya wengi!
 
Kwakuwa wana CCM ni wengi. Kwakuwa vijana chini ya miaka 40 na wenye kipato duni ni wengi. Kwakuwa wazee wa miaka zaidi ya 60 ni wengi na kwakuwa akina mama ni wengi, basi mjumuisho wao inaonesha wasiotaka Katiba Mpya ni WENGI SANA! Hivyo basi, wanaodai Katiba Mpya ni wahuni wachache ambao hawatakiwi kuyumbusha mawazo ya wengi!

Na Kwa kuwa wenye elimu ni wachache

Wenye uwezo kiuchumi ni wachache
Wenye Ari na nia ya kutimiza ndoto za maisha yao ni wachache

Wenye kupenda haki ni wachache

Hili unamzungumziaje?
 
3. Wana CCM
Kundi hili lipo lipo, hili ni Kama bendera, Inategemea serikali itakapoegemea. Serikali ikisema Katiba mpya ndio, nalo linasema Katiba mpya ndio, serikali ikisema hapana, nalo linasema hapana.
Nimecheka kama mazuri vile… CCM watuaribia sana hiki kizazi kinachoitwa watoto wa TEUZI.
 
Ni kweli mkuu umegusa makundi yoteyote. Hapo kwenye kila kundi la wapigania katiba pia kuna uhaba wa wanawake, sijui kwanini wanawake wanakua nyuma kwenye mambo mtambuka kama haya. Ni mara chache mno mijadala ya katiba/siasa si mtaani si mitandaoni wanaume hutalawa mijadala hii.

Aisee wajitafakari tunawahitaji sana katika harakati za kukomboka jamani.

Lakini yote kwa yote Elimu Elimu Elimu.

Elimu na umasikini hapo ni kigingi
 
Tungepata walau msimamzi wa katiba hii iliyopo naamin tungefika tupatakapo.
 
4. WAZEE Hasa wenye miaka kuanzia 60+
Kundi hili litasimama upande serikali ilipo. Kundi hili sio la kulaumiwa Kwa sababu wengi wao elimu Yao ni duni, exposure ya dunia iendavyo pia ni hafifu.

Kundi hili lisilohitaji au kujishughulisha na masuala ya Katiba ndilo kundi lenye watu wengi zaidi, karibu 80% hawana mpango wa Katiba mpya wala hawajihusishi na Siasa.
Tanzania haina wazee 60+ kwa uwingi uliousema,CCM imeua wazee wetu kwa kuwapa umasikini.
Takwimu zinaonyesha vijana ndio asilimia 80 Tanzania . Na hawa vijana kwa uwingi wao wakielimishwa umuhimu wa katiba mpya.
 
Ukimuonyesha mtanzania uhusiano wa wazi na moja kwa moja jinsi gani katiba imefanya tuwe na hali mbaya ya kiuchumi au jinsi gani katiba itaboresha need ya chini kabisa ya kila mwananchi kama ilivyo kwenye Maslow's hierarchy basi hata hilo kundi ambalo halina muda na katiba litaanza kufikiri zaid,
,, msiwahukumu kuwa hawataki katiba wakat mnajua dhahiri kuwa hayo yooote ya kutaka au kutokutaka katiba ni for your own interests za kisiasa

CCM wanatumia advantage ya kutuweka kwenye hali duni for more than 60 years kutufanya tusifikirie vitu vikubwa,,,,siwezi kutaka burger wakati mlo wa siku ni shida kuupata( simple personality calculation) siwezi kuwaza self esteem au self actualization level wakati physical and security needs sijazipata bado

CHADEMA wana hoja nzuri za kutaka mabadiliko ya kiutawala ( na sio kikatiba kama wanavyo claim wao) najua kama CHADEMA wangekuwa wenye nchi sasa hv hoja ya katiba isingekuwa kipaumbele kwao,, ( wenye fikra finyu watakataa)

Makundi hayo hayawezi kuwasikiliza kwa sababu hamjagusa sehemu ambayo wao wanaona ina umuhimu pesa, mlo, mavazi na uhakika wa kuingiza kipato kila siku,,,, sio CCM au CDM hakuna mwenye maelezo ya moja kwa moja ubadilishwaji wa katiba utaleta uhakika wa kupata angalau pesa ya matumizi ( nazungumzia kazi)

Mnasahau kuwa kundi la hao ambao hawataki katiba ndio kubwa zaidi tanzania wajuzeni hao ambao mnaona ni washenzi,,, kuhusu umuhimu wa katiba ambao unagusa maisha yao ya kila siku moja kwa moja (ukiwatoa CCM ) hapo mtafanikiwa
Twitter na mitandao ya jamii isiwadanganye kuwa each citizens of this doomed county anataka katiba


#politiciansarefiltyliers

Umenena iliyokweli
 
Tanzania haina wazee 60+ kwa uwingi uliousema,CCM imeua wazee wetu kwa kuwapa umasikini.
Takwimu zinaonyesha vijana ndio asilimia 80 Tanzania . Na hawa vijana kwa uwingi wao wakielimishwa umuhimu wa katiba mpya.

😃😃😃😃

Ati imeua Wazee wetu
 
Bwana Rohe: majibu yako haya hapa.

1. Wanasiasa hasa wa vyama vya Upinzani

WAENDE BUNGENI, WAJENGE H OJA, NAONA WAKO 2 WA KUCHAGULIWA NA 19 WA KUTEULUWA JATIKA BUNGE LAXWATU 400+ TUWAOMBEE, HII HIUITWA UPHILL TASK, LABDA WATAFANIKIWA. INGEKUWA NI CHAMA KIMOJA INGEKUWA RAHUSI ZAIDI BASHIRU NA POLEPOLE WANGESIMAMIA, LAKINI VYAMA VINGI LAZIMA IWE KURA YA WAZI. KUBADILISHA KATIBA NI LAZIMA IANZIE AU IISHIE BUNGENI, HAWO NDIYO WAWAKILUSHI WAXWABANCHI WSLIOPIGIWA KURA. KENYA RAILA OGINGA NA UHURU WAMEUNGAMISHA MAKABILA YAO BBI IMEKATALIWA - UKIWEKA KALENJIN NA WAXIGUA WA PWANI NA WAPARE WAUTWA WAKAMBA NGOMA INAKUWA DRONI 49:51

2. Wanasiasa upande wa Zanzibar.


ZANZIBAR NI SERIKALI YA MAPINDUZI, WAARABU WALING'OLEWA KWA NGUVU HAWAKUOMBWA KATIBA MPYA. NAO WAJARIBU.

3. Wanaharakati wa mrengo wa kiliberali.

WHAT THE HELL IS THAT? UNA MAANA MASHOGA? WAENDE EU

4. Wasomi wenye elimu kuanzia stashahada mpaka uzamivu. Wenye exposure ya dunia na wenye kutaka mabadiliko kwenye nchi.

WEWE ULIZAMIA WAPI? KANA KWELI UNAXEXPOSURE YA DUNIA NI LAZIMA USHAFIKA USA NA UK NA RUSSIA NA CROATIA NA INDIA. NI LINI USA WAMESEMA WANATAKA KATIBA MPYA? PERMANENT INTERESTS, NO FRIENDS.

Mkuu ahsante Kwa kushiriki mjadala
 
Na Kwa kuwa wenye elimu ni wachache

Wenye uwezo kiuchumi ni wachache
Wenye Ari na nia ya kutimiza ndoto za maisha yao ni wachache

Wenye kupenda haki ni wachache

Hili unamzungumziaje?

..kuna makosa ktk uwasilishaji au uchambuzi wa makundi kuhusu katiba.

..mchambuzi amefanya kosa la kuchanganya kundi linalopinga katiba mpya, na kundi lisilokuwa na uelewa wa katiba.

..mchambuzi au mtoa mada alitakiwa ayabainishe makundi yafuatayo.

1. Kundi linalodai katiba mpya.

2. Kundi linalopenda katiba ya zamani.

3. Kundi lisilokuwa na uelewa wa katiba.

..makundi # 1 na # 2 yanatakiwa kuwaelimisha na kuwashawishi walioko ktk kundi # 3.

..vilevile kuna umuhimu wa KUJIFUNZA toka ktk kundi # 3. Kutokuielewa katiba haimaanishi kutokuihitaji katiba.
 
Kwa mujibu wa tathmini hii ambayo si haba akisikika mtu anapinga katiba mpya bila shaka ni:

1. Mwanamke,
2. Mzee,
3. Boda boda, machinga, sungu sungu, mpiga debe, vibaka vibaka na wa namna hiyo
4. Wana CCM, wasiojitambua, wanafiki na wenye Maslahi binafsi.

Hiiiiii bagosha!
Mengi uliyoyaandika ni ya kweli kabisa.
Ifike mahali tukubaliane kwamba:
1.Katiba mpya ni hitaji mhimu kwa Watanzania
2.Katiba mpya iliyo bora haiwezi kuletwa na wanufaika na Katiba iliyopo.
3.Katiba mpya na iliyobora kwa nchi nyingi za Africa, huwa inapatikana kwa njia mbili tu
a)Kwa utashi wa wenye nguvu ya kimamlaka,na/au

b) Kwa ushindi wa wenye mamlaka ya nguvu.(Hapa tofautisha wenye nguvu ya kimamlaka na wenye mamlaka ya nguvu)
4.Watanzania walio wengi ni mbumbumbu wa kisiasa, hivyo hawajitambui na kimsingi hawawezi kushiriki katika vuguvugu la kudai Katiba mpya japo ina manufaa makubwa kwao.
5.Kutokana na hoja hizo hapo juu, ni wazi kwamba upatikanaji wa katiba iliyo bora kwa Watanzania inategemea tu utashi wa mwenye nguvu ya kimamlaka ambaye, kwa hali ilivyo kwa sasa, ni Rais tu.(Rejea ujio wa Demokrasia ya vyama vingi Tanzania)
Vinginevyo, wenye mamlaka ya nguvu,( jambo ambalo sisi wananchi hatuombei litokee katika nchi yetu na Mungu aepushie mbali) wataleta hiyo katiba mpya.


Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom