Hii ndio Orodha ya makundi ya watu wanaohitaji Katiba Mpya na wasiohitaji

Kenya wana katiba tunayoambiwa ni bora sana lakini ufisadi na umasikini kwa raia umekita mizizi!

Ndio kusema kwamba katiba ya Kenya ni nzuri kwa wanasiasa tu!

Katiba nzuri na huku una njaa ni sawa na unyani[emoji205][emoji205][emoji205]
Unaweza kuthibitisha kauli yako?
Tunahitaji Katiba ya Wananchi itakayotokana na mawazo yao na siyo Katiba nzuri.Kama Katiba ya Kenya haijatatua changamoto zao za kiuchumi,kijamii,kisiasa,usawa ama haitoi Haki sawa kwa wananchi,ni jukumu lao kuiboresha na isiwe sababu ya Watanzania kutokuandika Katiba yao.
Sidhani kama ni sahihi kuwatisha Wananchi, ujenzi wa uchumi hauwezi kuwa mbadala wa Katiba Bali Katiba Bora ni msingi wa kujenga uchumi endelevu.
Tusiwapotoshe Watanzania. Kwenye madaraka hawastahili kuwazibia Wananchi kujipatia Katiba waitakayo.
 
Sihitaji Katiba wala nini nachotaka ni ugali mezani na kulipa ada za wanangu bila shida.
Nakubaliana na wewe. Naamini wewe na mm ni wale ambao hatujui kilichopo kwenye katiba ya sasa. Mimi naongezea hitaji la moyo wangu la kuwa na viongozi waadilifu na hodari wa kusimamia haki kwa kutumia busara. Wabunge wasimamie maendeleo ya wapiga kura wao na wazikane nafsi zao wasikubali Kula kabla wananchi wao hawajashiba.
 
Ukiwa an Average Tanzanian
Wala huna maslahi na Katiba mpya wala ya zamani
Maadam unachunga mdomo wako na kufuata sheria za nchi.,
 
usikimbilie kuwalaumu hilo kundi. Hata hawaviongozi wanaharakati nao sometimes ni kikwazo. Hebu fikilia kiongozi anatumia miaka zaidi ya 8 kuhubiri kuwa Fulani ni mwizi. Fisadi cha ajabu kwenye uchaguzi huyo wanayemwita fisadi ndo wanampa apeperushe bendera ya chama kugombea. Unategemea vijana wamwamini tena?
 
Kenya wana katiba tunayoambiwa ni bora sana lakini ufisadi na umasikini kwa raia umekita mizizi!

Ndio kusema kwamba katiba ya Kenya ni nzuri kwa wanasiasa tu!

Katiba nzuri na huku una njaa ni sawa na unyani[emoji205][emoji205][emoji205]

Pamoja na mapungufu yote hayo uliyosema, bado katiba ya Kenya ni nzuri na madhubuti kuliko yetu. Na uchumi wa Kenya ni bora kuliko wetu. Hapa unachosema ni sawa ww umepata kwenye masomo F, anasifiwa mwenzako mwenye C+, ww unasema huyo mwenye C+ pamoja na kusifiwa, lakini hajapata A!
 

Kwa taarifa yao hao wengi unaosema hawataki katiba mpya, kwa wingi wao huo huo hata ikija kwao ni sawa. Hilo kundi kubwa ni lile linaloburuzwa kwa chochote. Kwahiyo usitake kuonyesha kuwa hawaitaki kwa maana ya uelewa. Kwa maneno marahisi hilo kundi kubwa hawajui chochote, kwao kizuri au kibaya ni sawa tu.
 

Sio kwamba hawataki, hao bado wako usingizini. Hili kundi ni la kuswaga tu kama ng'ombe. Maana hata ikija hiyo katiba mpya kwao ni poa, isipokuja ni sawa tu. Sasa kama watu wanakunywa maji ya tope na wanyama, huku viongozi wakitembea na maVX ya 500m na hawajui lolote wanaona sawa tu, hao unawaambia kuhusu katiba mpya ili iweje? Hayo ni ya kuburuza tu.
 
Uko sahihi viongozi wengi ni wafanyabiasha ndio maana wanataka katiba inayowalinda. Wenzetu wenye mfumo mzuri biashara na uongozi ni tofauti Cc. Trump administration ilishindwa kwa sababu mfumo wa wenzetu haukumpa nafasi kufanya ujinga na nchi kwa ajili ya biashara zake na ndio tunataka katiba ya aina hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…