Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Mamlaka ya serikali za mitaa ALAT ingepigia kelele hili kama walichofanya kwenye kodi ya majengo/nyumba.

Haiingii akilini usumbufu wote ule wanaopata wananchi wanaopakana na hifadhi afu pesa wakatumbue wengine huko
Kwa hapa nchini national park inayoongoza kwa kuingiza hela nyingi ni Ngorongoro ikifuatiwa na Kilimanjaro. Lakini hao wananchi wanaozunguka hizo mbuga hata hawajui kama hizo mbuga zinafaida gani kwao zaidi ya kuwa harassed tu wanapoingia maeneo ya hifadhi. Kama ngorongoro hata wale wamasai wanaokaa mle ndani kila mara wanataka kuwatimua. Ni uonevu wa hali ya juu
 
Kuna Meru DC na Arusha DC wapi ni makao makuu ya Arusha DC na mipaka yake?
Arusha DC makao makuu ni pale Sekei. Meru DC makao makuu ni Usa River pale Leganga.

Meru DC inaanzaia inapoishia Tengeru kuendelea mpaka na mkoa wa Kilimanjaro. Arumeru ni eneo lote la kuzunguka Arusha City inapakana na Longido kwa Kaskazini, Meru kwa Mashariki, Meru kwa kusini na Monduli kwa Magharibi
 
Shida iko hivi hiyo hardware pale Kkoo inalipa kodi yake TRA, anachoambulia Ilala ni leseni ya biashara tu ambayo gharama yake ni ndogo kuliko PYE ya mtumishi wa umma wa ngazi ya chini wa Wilayani. Ndiyo maana Halmashauri hazitaweza kujitegemea unless ziwe na migodi kama Geita au Kahama.

Tena wakati wa magu hali ilikuwa mbaya zaidi maana hata ushuru wa mabango ulichukuliwa na TRA. Something need to change kama kweli tunataka kupeleka hii nchi mbele
 
Tanzania imekua shamba la bibi ndio maana baadhi ya viongozi wasio waadilifu wanaibatu hawaogopi.
Wengine wanawaziba midomo takukuru na macho yanatupiwa mchanga kabisa.
Ukianhalia halmashauri kama Tanga, Arusha Mbeya,Mwanza nk eti zimepitwa na Dodoma. Tatizo ni wizi. Hapo Dodoma wapo katibu na macho ya wakubwa ndio maana. Utaona kadri muda unavyoenda nao watashuka. Tanga kuna maeneo ya taasisi yamekodishwa kwa wafanya biashara lakini taasisi hizo hazipati hata mia moja na wawekezaji wanapeleka kwa mabosi. Viwanda vimefungwa wajasiriamali kama mama lishe hawauzi na kulipa kodi tena,wizi mtupu na madiwani na mbunge wamemuachia mkurugenzi halmashauri. Takukuru tanga hawajawahi kuonekana wakitetea maslahi ya uma kama ilivyo kwa mikoa mingine. Wanaungana na wezi na kuwahakikishia ulinzi. Halmashauri nyingine hasa majiji yaliyopitwa na Dodoma viongozi wake wasaidiwe
Waziri wa uwekezaji,fedha,viwanda na biashara saidia tanga huyo wa Tamisemi akifika tanga anakaa meza moja na hao wabadhirifu.
 
Nielimishe tafadhali, maendeleo maana yake ni nini?
Maendeleo ni dhana pana ila kwa muktadha wa mjadala wetu ambapo najua unataka kujua ni vipi kujenga nyumba ya kuishi sio maendeleo, nitakujibu...

Chakula, mavazi na malazi (nyumba) vimeainishwa kuwa mahitaji ya msingi ya mwanadamu bila kujali hali yake kama ni tajiri ama fukara.

Kwenye Human Development Index (HDI) kuna vitu vinne vinazingatiwa ikiwemo Standard of living ambapo chakula, mavazi na malazi huangukia humo. Na vinatathminiwa kwa mtiririko huo ie chakula kwanza, mavazi kisha makazi.

Kama ambavyo huwezi kumregard mtu ameendelea kwa kuwa anamudu chakula au mavazi, ndivyo ambavyo huwezi kumregard mtu huyo huyo kwa kuwa tu amejenga nyumba ya kulala.

Mtu aliyejenga na aliyepanga wote wana malazi tena yawezekana aliyepanga ana malazi bora kuliko aliyejenga kutegemea na hadhi ya nyumba husika.

Unaweza kuwatofautisha vizuri mtu aliyejenga na yule mwenye uwezo sawa na wake aliyepanga na kisha ile gharama ya ujenzi akaiwekeza ikawa inazalisha na baadae akamiliki nyumba huku akiwa na miradi tayari.

Disclaimer:
Sisemi hata kidogo kuwa kujenga ni jambo baya kwa mtu ambaye anamudu mahitaji yake mengine bila shida ila kukimbilia kujenga wakati with time huwezi hata kumudu mlo na mambo mengine hilo ni tatizo.

Na ndio scenario za ujenzi mwingi wa vijijini watu wanao ufanya kwa maelezo kuwa wanaboresha kwao wakati anao waboreshea wamedumaa kwa njaa.

Kwa nini hiyo gharama ya ujenzi usibuni mradi pale kijijini ambao utapelekea kujenga huku watu wakiwa wanajiingizia kipato na kujipatia chakula, mavazi, elimu, afya njema, huduma za maji, nishati ya umeme nk nk ambavyo actually ndivyo huitwa maendeleo kwa pamoja.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dodoma kuna kipi hasa hadi kuizidi mufindi, njombe, mwanza, kinondoni na temeke yenye bandari
 
Kumbe Chunya tunakuja vizuri. Japokuwa ndiyo funga mkia ktk list tajwa.
 
Zitaweza tuu kwani zote zina migodi? Kuna kilimo,misitu na biashara na ufugaji na uvuvi kuna pesa za kutosha ni suala la uwekezaji tuu.
 

Ikiwa huko kijijini kwenu ndio mnajengewa shule za kata, kuletewa umeme wa REA na vituo vya afya kwa hisani ya CCM.
Uchagani huduma muhimu kama shule, vituo vya afya, umeme, maji na barabara ni vitu ambavyo wazee wetu walivijenga na bado vipo vinavyojengwa na kuendelezwa hadi hii leo.
Na kuhusu suala la kuinuana na kujaliana Wachaga ni moja ya jamii au kabila inayojali kuinuana sana kielimu na kiuchumi.
 
Dodoma kuna kipi hasa hadi kuizidi mufindi, njombe, mwanza, kinondoni na temeke yenye bandari
Wajameni tusiishi kwa kukariri, miaka 5 ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali umezalisha na kuvutia fursa nyingi za biashara, ujenzi, huduma na viwanda

Nani hajui kwamba Dom ni hot spot ya ujenzi kwa sasa nyuma ya Dar,both kwa private sector na public sector? Unapojenga manake kwamba sekta ya ujenzi inakua kwa hiyo mapato kutoka huko ni makubwa ambayo ni leseni za biashara,kuuza viwanja,vibali vya ujenzi na kodi mbali mbali

Lakini pia Dodoma kuwa makao makuu manake kwamba ina wakazi wengi ambao Wana purchasing power kubwa kuliko miji mingi ukiondoa Dar,tafsiri yake ni kwamba biashara nyingi zimehamia huko kufuata hao wanunuzi.

Kana kwamba haitoshi uwekezaji wa viwanda na biashara nyingine kubwa kubwa unashika kasi,mfano mdogo retail sector kwenye sekta ya mafuta ya magari imekua Sana kiasi kwamba vituo vya mafuta ni vingi Sana Dom nyuma ya Dar tuu.

Hata viwanda vinajenga Sana tuu,juzi Kati hapa karibu wazindue kiwanda cha kuchakata dhahabu kama kile cha Mwanza,pia kampuni ya Burundi inajenga kiwanda kikubwa cha mbolea,dola za marekani milioni 400 zinawekwa.

On top of that population ya Dom saiz ni kubwa nyuma ya Dar,Mwanza juu ya hapo ni population yenye pesa tofauti na ya Miji mingine.

Stay tuned,utashangaa zaidi
 
Ndio muwafichue sasa maana pesa inayoliwa ni yako na yangu japo mnufaika wa kwanza utakuwa wewe uliopo Eneo husika.

Kama kuna upotevu wa mapato ni shida ya viongozi wa huko,mtaishiwa kuzidiwa na kulia Lia kila siku mara ooh wamepika data mara ooh sijui nini yaani hoja hopeless
 
Tanga sidhan kama inawashinda watu wa kigoma kwa kipato mana maisha yatanga yanajulikana takwim zako jua ni za TRA so tanga Kuna viwanda vingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…