Mtoa mada yuko sahihi ingawa sio kwa 100%.
Mwekezaji yeyote kabla ya kufanya maamuzi ya kuwekeza, anatakiwa kuangalia gharama za uwekezaji na kiwango cha faida anachoweza kupata.
Bei ya kuuza na kununua vipande ni mojawapo ya taarifa muhimu. Bei zilizoorodheshwa hapo ni bei ya siku ya tangazo. Hiyo ni tofauti na bei ambayo mwekezaji alinunua vipande hivyo. Kwahiyo, bado kuna faida mwekezaji atapata iwapo anawekeza kwa muda mrefu.
Mifuko inayonalenga wawekezaji wa muda mfupi kama liquid inakuwa na bei za kuuza na kununua zinazofanana zaidi kuliko mifuko ya malengo ya muda mrefu.
Kwahiyo, cha msingi ni kupiga hesabu ya kiwango cha faida kwa kila kipande kwa muda unaotarajia kuwekeza na kufanya maamuzi yanayoendana na malengo yako.
Kiujumla, Faida Fund na UTT funds hazina tofauti sana.