Taratibu mnaanza kuukubali ukweli kuwa wakrtisto wengi ndo wenye kushughulishwa na majini.
Mi ninachopata tabu na nyinyi ni katika ugumu wenu wa kuelewa, sijui ni msingi mliotengenezewa ndo unawazuia kuelewa wanachosema waislamu ama ni uelewa sahihi wa lugha ya kiswahili. Mimi ninaposema porini kuna simba na nyati haimaaanishi nina urafiki nao hawa wanyama bali nina-aknowledge kuwa wana exist huko porini. Natambua uwepo wao lakini bado haimaanishi natamani kuishi nao kama ninavyoishi na paka au mbwa nyumbani kwangu. Sisi waislamu tunaamini majini ni moja katika viumbe wa Allah kama ambavyo wanaadamu, malaika na wanyama tulivyo. Zaidi ya hapo tunaamini ya kwamba sisi ni viumbe tofauti kimaumbile na tunaoishi katika uhalisia tofauti (two separate worlds), zaidi ya hapo ni kwamba sisi wanaadamu na hao majini tumepewa akili na uhuru wa kuchagua katika matendo yetu, either tutii maamrisho ya muumba wetu ama tuende kinyume na maamrisho yake. Kutambua uwepo wa kitu ni tofauti na kukiabudia.
Kuabudia kitu ni kuamini kuwa hicho kitu kina nguvu juu yako ya either kukunufaisha ama kukudhuru. waislamu tuna hii kauli mbiu tunayoitumia mara kwa mara "Laa hauwla walaa kuwwata illa billah" which translates as There is no power and no strength except with God. Pia kuna hii kauli ngao tumepewa na muumba wetu "Audhubillah min al-shaytaan ir-rajeem" Which translates as "I seek refuge in Allah from the outcast Shaitan". Kwa mwenye uelewa inamtosha kutambua nafasi ya shetani ni dhalili kwa kiwango gani.
Sisi waislamu tunaamini jema na ovu linalompata mwanadamu ni mipango ya Allah, wakristo walio wengi wanaamini mabaya yanaoyo wapata wamepewa na shetani i.e mathalan kukosa kazi, kukosa mume/mke, umaskini, maradhi yote haya wakristo wanaamini ni kazi ya shetani/majini. Huku ni kumdogosha Mungu kwa kiasi cha juu sana kwasababu ni kama unamlinganisha yeye na Shetani kuwa ni pande mbili zenye kushindana.
Sasa ukiangalia kwa makini kati ya waislamu na wakristo utagundua wanaomuabudu shetani ni wakristo kwa kumpa nguvu asiyo kuwa nayo! wakati upande mwengine waislamu mambo yao yote wameyaegamiza kwa Allah, muumba wao na muumba wa huyo shetani aliyelaaniwa.