Tetesi: Hii ndio sababu ya kiroho kwanini watu wanaookota chupa za plastiki wengi huwa wanaishia kuwa wendawazimu

Tokea zamani mtu akiwa haeleweki unaambiwa utaanza kuokota makopo muda si mrefu, wakimaanisha utakua kichaa.
Hiyo ni kabla ya biashara ya kuuza makopo/ chupa kushamiri.

Kwa mtazamo wangu, mtu kufikia kuifanya hii biashara, inamaana tayari kuna tatizo kichwani na kuendelea kuifanya hiyo kazi kunazidi kumfanya kuwa duni kifikra na kisaikolojia, lazima awe mwendawazimu.
Hakuna cha kiroho wala madhabahu hapo.

Inamaana huyo mtu hapo ndio uwezo wake wa mwisho na wa hali ya juu kabisa kufikiria.

Niliwahi kupewa kazi njia ya kuelekea airport kuna kituo kinaitwa karakana kama sio mchicha.

Kampuni ilikua vizuri lakini mazingira yake ya kihindi na maeneo ya chakula kuwa ya shida (sehem nyingi kule ni site za wajenzi) wali nyama 2000/- nilitumikia mwezi mmoja tu nikaacha licha ya kwamba sikuwa na kazi yeyote wakati huo. Nilijiambia tu kwamba kwa akili niliyonayo na uwezo wangu nawezakufanya vizuri zaidi ya hapa.

Chunga sana mawazo na akili yako, unachokipokea na kukikubali akilini ndicho kinachotokea.
 

steji kuokota makopo kuwa maisha yako yamefika katika kufikiri au kukosa pakushikwa mwisho.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
kiukweli ni biashara ya kiwango duni sana na mpaka mtu anaanza kuokota makopo kama kazi si bure kuna nut haziko sawa kulinganana aina ya kazi yenyewe
umenena mkuu, yaani kwa mtu anayefanya ujasiliamali huo ni mtu aliyekata tamaa ya maisha kabisa.
So nakubaliana na mzee wa researches za kichawi mkuu LIKUD
 
Miaka ya nyuma kidogo kuokota makopo ilikuwa ni matokeo ya laana [ukichaa], na ni vichaa pekee waliokuwa wakiokota makopo na kuzunguka nayo [noncommercial]... siku zikasonga mara ikawa biashara ya kujipatia kipato kuendesha maisha [lengo ni ku-recycle].

Kwa asili ya kazi hii kuwa ni ukichaa, bado inaendeshwa katika namna ile ile ya ukichaa.... kwamba ili mtu ‘timamu’ aokote hayo makopo ni lazima ajitie ukichaa kuanzia mavazi na hata mwendo.

Angalizo:
Soon atatokea mmoja wao hapa na kuhoji ‘ukichaa’ ni nini na kuhitaji uthibitisho, haya ni maoni yangu tu na wala sitohusika kuthibitisha.... usiku utapokwisha.
 
Sio kweli, ukichaa wao hautokani na maswala ya kiroho. Ukweli ni kwamba asilimia kubwa wanakuwa wanatumia madawa ya kulevya, pia wanastress.

Yale madawa ndio huwasaidia kusahau stress zao kwa muda mfupi. Kadri siku zinavyokwenda, afya inazorota kutokana na kutopata mlo kamili plus madawa.

Inapofikia hatua ya kushindwa kupata hela ya kutosha kete, hapo stress huongezeka mara mbili.

So madawa na msongo wa mawazo ndio chanzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga mtupu!

Kwahiyo muda huu nikianza kuokota makopo ili nikayauze nitageuka kuwa kichaa?

Au kwa kuwa wanaonekana wachafu wachafu ndio ukahitimisha kwamba wamerukwa na akili?
 
Ni kweli kabisa Majini hupenda kukaa majalalani na kwenye vyoo vya public, Mochware ba Makaburini..
Hakuna cha majini yoyote yale.

Ni imani zenu za kijinga tu!
 
Kweli kuna jamaa naye alikuwa fresh alivyoaanza kuokota makopo baada ya muda akawa kama chizi hivi.
 
Anaokota ndiyo.

Alivyompiga yule kinyozi wa Marekani watu wakadai mmarekani mwenyewe mchovu kumbe kinyozi hoja ikaja sasa mbona Cheka muokota makopo.

Usiniambie hujui chief!?
Cheka anawalipa watu wamuokotee makopo ila yeye hajawahi kuokota makopo kwenye viroba.
 
Mbona wanasema Majini hayapendi uchafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…