Hii ndio Sababu ya Mungu Kutoonekana

Mungu yupo utakuja kumwona tu siku moja japo si kwa macho ya nyama.
 
Hebu tujaalie unachokisema ndio sahihi.

Inamaana mungu hakuweka sababu yeyote ya sisi kumjua yeye, maana hakuweka mitume wala malaika, sawa.

Hivyo maana yake viumbe wote hawajui (wajinga) juu ya uwepo wa mungu.

Sasa wewe haya uliyoyaandika hapa umeyatoa wapi?

Hapa ndipo unadhihirika ubatili wa hoja yako maana unatudanganya.
 
Hebu tujaalie unachokisema ndio sahihi.

Inamaana mungu hakuweka sababu yeyote ya sisi kumjua yeye, maana hakuweka mitume wala malaika, sawa.

Ndio hakuweka Mitume wala Malaika.
Maana Kama Angeweka Kungekuwa na Muongozo Mmoja Tu siyo Miongozo na Vitabu vinavyopingana

Hivyo maana yake viumbe wote hawajui (wajinga) juu ya uwepo wa mungu.

Sasa wewe haya uliyoyaandika hapa umeyatoa wapi?

Hapa ndipo unadhihirika ubatili wa hoja yako maana unatudanganya.

Viumbe wanajua Uwepo wa Mungu ila Si kama Wewe unavyotafsiriwa kwenye Vitabu vyako. Kwamba Yupo mahali popote pale ukimuiita Anakuja kukusikiliza. Malaika, majini. Binadamu wote Tumeumbwa naye ila Hayupo Na Viumbe wake kila Kiumbe kipo mahali pake.

Kuhusu swala la Nimeyatoa Wapi nis Sawa na Nikuulize wewe umejuaje Kuhusu Mungu. Kila Kitu Kimeandikwa na Kusimulia na Mababu na Wazee wa Mwanzo kuwepo Hapa Ulimwenguni
 
Kuna watu wanasema Wamemuona Mungu.
Hao wanaodai wamemuona Mungu hawana tofauti na wewe, maana wewe unakuja na kuanza tu kusema Mungu hivi Mungu vile mara hivi mara hivi.

Najiuliza kwani wewe ni nani au una uhusiano gani na Mungu mpaka ukaweza kuyajua hayo yenye kuhusu Mungu na sie wengine tusijue?
 
Kwahiyo hao wazee nao wameyatoa wapi ikiwa mungu hakutoa muongozo wowote?
 
Sawa mfalme zumaridi,
Tumekusikia..
 
Soma surah ikhlas utumuelewa MUNGU vizuri
 


Wewe ukitumwa na Mungu hauwezi ukapigwa na viumbe vilivyokuzidi uwezo kiakili, kiteknolojia na kimaumbile?

Kwenye Manabii na mitume mbona nao walitumwa na Mungu Baadhi Yao waliuawa na watu?

Kwa Uelewa wako; unafikiri malaika wanafanana na kulingana uwezo?

Zipo Aina nyingi za malaika(wajumbe wa Mungu) waishio mbinguni. Wapo malaika wenye mbawa mbili, wapo wenye mbawa nne, sita mpaka 24.
Kuna makerubi na maserafi.

Unafikiri wanalingana uwezo?

Hata Majini yapo ya Aina kadhaa kulingana na jamii zao. Hayalingani uwezo Kama tulivyobinadamu.


Mungu kukutuma haimaanishi hautapigwa na waliokuzizi uwezo ikiwa ni Mungu ataruhusu upigwe
 
 
Hivyo vitabu vya mwanzo, viliandikwa na nani kama sio binadamu??
 
Wewe ukitumwa na Mungu hauwezi ukapigwa na viumbe vilivyokuzidi uwezo kiakili, kiteknolojia na kimaumbile?

Kwenye Manabii na mitume mbona nao walitumwa na Mungu Baadhi Yao waliuawa na watu?
Ndugu yangu jiulize Mungu wa Kweli atume mtu halafu Huyo mtu ashindwe na Auawe. Yaani Mungu atume Kitu halafu kishindikane. Huyo atakuwa Mungu wa Kweli na Asiyeshindwa kitu kweli. Yaani Mungu aliyeumba Ulimwengu kwa Muujiza wake leo hii atume Kitu kishindikane na Kiuawe

Wewe huoni hao waliotumwa Walishindwa. Wakishindwa wao si ndio Mungu kashindwa ndugu yangu



KABLA Hujawajua Vizuri hao Viumbe jijue kwanza Wewe upoje kabla Hujajua viumbe wengine. Mjue Kwanza Mungu alikuumbaje ili uweje ndio ufuate Viumbe wengine



Mungu kukutuma haimaanishi hautapigwa na waliokuzizi uwezo ikiwa ni Mungu ataruhusu upigwe

Mungu hamtumi mtu maana Mungu hafanyi kazi zake kwa Kushirikiana na Viumbe wake. Hao wanaotuma ni Ma-mola wa Ulimwengu huu. Ndio maana Unawaona Sometimes mambo mengi yanashindikana pale wanapotuma hao Manabii na Mitume

Mungu Alifanya Vitu kwa Muujiza wake na Vikafanyika Havikushindikana Kufanyika. Ukiona Vinashindikana Ujue huyo Si Mungu mwenye Vyote
 
Paragraph ya nne, umezungumzia vitabu vya mwanzo, hata vyenyewe viliandikwa na binadamu
Ndio viliandikwa na Binadamu Ndugu. Ndio maana Nasema Tutumie Akili timamu kuvichambua Vitabu hivyo kujua Kama Ndani yake Vina Ukweli wa Kibinadamu na Ki utu kuliko kukubali mambo tu bila kutumia akili timamu
 
Binadamu wa kwanza Hakuongea na Mungu ila Aliwezeshwa kujua haya na Muujiza Wa Mungu
Inamaana mungu hakutuwezesha mimi na wewe kujiua haya Bali alimuwezesha binadamu wa kwanza kujua, na huyo ndio akawafikishia mababu ndio na sisi tukajua.

Sasa hapa huyo binadamu wa kwanza anakuwa anatofautigani na mtume/ mjumbe?
 
Kuna source yako muhimu na yenye kuaminika kuhusu hiki ulichoandika ?, au unaandika kulingana na upana wa ufahamu wako?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…