Hii ndio sababu ya walimu kupiga wanafunzi mpaka kuwaua

Hii ndio sababu ya walimu kupiga wanafunzi mpaka kuwaua

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
2,317
Reaction score
7,808
Frustration, Frustration, Frustration.

Asilimia 60% ya walimu wamekata Tamaa, tena Frastruation zao sio kwasababu ya mshahara, hapana Frustration kutoka kwa Mkuu wa shule, mwenyekiti wa mtaa, Diwani, MEK na watumishi wote wa halmashauri wanaweza kumpiga kofi mwalimu.

Imagine Mwl anafundisha shule nzima, daraja kupandishwa ni vita kali kutoka kwa Tsc na HR refer kigoma Mc, Tarime dc, lushoto bunda n.k, yaani mwl kupata stahiki zake ni kama vile yupo vitani asilimia 90% mwalimu hapati stahiki zake wanadai madai yao and no body care, ila linapokuja swala la kumpelekesha mwalimu na kumfanyia intimidation wako mstari wa mbele.

Imagine mwl yuko na salary nzuri tu ambayo ni sawa na kada zingine eg tgts d then amekopa kajenga mshahara unakuja 1/3 yupo na familia, unategemea nini? Huyu mwalimu anaachaje kuchanganyikiwa?

Kuna miaka fulani kabla sijakimbia chaki niliandika barua kama nane za kujitoa CWT (makato ya kitapeli) lakini Afsa utumishi akagoma kabisa kutoa makato, Imagine walikua wanakata 2% ya mshahara na hawana wanachokifanya zaidi ya viongozi kugombania tenda na kula hela za walimu lakini ukipambana kujitoa rahisi tu unaambiwa haiwezekani, huyu mwalimu kwanini akirudi shule asiwe na stress? Kwanini mwanafunzi asishushiwe kipigo?

Viongozi idara ya elimu huwa wanamini walimu kama ni wajinga, kwanza wakija kutembea shuleni huoni ile bond ya kuelekezana kwa upendo na kukosoana kwa staha ila wanachokifanya ni kumgombeza mwl na kumdharilisha kwa kumuondolea utu, Imagine huyu mwl mwenye 1/3 ya mshahara bila posho yoyote kiongozi akija ni kumtolea maneno machafu, huyu mwl kwanini asiwape watoto kipigo kizito?

Kuanzia utumishi, Tamisemi mtumishi wa halmashauri akienda anasikilizwa kwa umakini na kama ni tatizo bas wanalitatua kwa weledi, lakini huku halmashauri sijui wana akili gani? Kwa utafiti niliofanya watumishi wengi wa halmashauri walikua ni walimu wakenda kusoma vitu vingine wakarudi wakawa vitengo vingine ila basically ni walimu tu, roho mbaya na chuki.

Mwl akienda kwenye seminar ya kusimamia mtihani 90% ni vitisho kutoka usalama, takukuru, police, waseminishaji, yaani wanauwezo wa kukusimamisha na kukutishia kukufukuza kwasababu hujaandika namba ya mseminishaji hahaha.

Na nyie walimu acheni mambo ya hovyo, utampigaje mwanafunzi mpaka afe? Tena kwa kumchangia? Hiyo energy unapatia wapi? Kwanini usifanye mambo yako? Najua sometimes ni ngumu kufanya biashara ukiwa na mkuu mnoko ambao 90% ni wa hovyo,

Wewe mwalimu nikwambie unachokifanya kufundisha ni kwa ajili ya muajiri wako, lakini ukipatq shida hutokuja kumuona mwajiri akikutembelea central police au mahakamani.

Timiza majukumu yako 100%, nenda shule asubuhi timiza majukumu yako achana na mambo ya fimbo, fundisha, toa kazi, sahisha madaftari, saa nne nenda chini ya mti mbali kidogo na shule kapige fegi zako, zugazuga rudi saa 7 timiza majukumu yako saa nane na nusu ondoka nenda kwa mama kimbo piga mataputapu yako rudi nyumbani.
 
Mkuu wa shule si lolote si chochote, yule ni sawa na monitor tu wa darasa, si wa kumtetemekea sana. Hata ofisa elimu naye si wa kumuogopa sana, mwajiri ndiye bosi mkubwa maana ndiye anayeajiri na kulipa mshahara, hata hivyo naye akipuuza maslahi na haki za walimu anakula za uso tu.
 
Rais Mwinyi alikuwa mtu mwema sana na mwenye huruma (Mungu amlipe mema huko aliko)
Yeye aliona Mwl Hana posho za katikati ya mwezi kama walivyo watumishi wengine wa umma bali anategemea mshahara tu, ambao haukuwa unakidhi mahitaji ya Mwl Kwa mwezi mzima.

Akaamua kutatua changamoto hii Kwa kuweka posho ya Kila mwezi iliyoitwa posho ya kufundisha (Teaching allowance) ambayo kiasi chake lilikuwa ni asilimia 50 ya mshahara ghafi.
Hii posho ilikuwa haina makato yoyote hivyo Mwl aliipata kama ilivyo. Hii posho ilipandisha sana morali na hadhi ya walimu. Mkapa alikuja iondoa alipoingia madarakani na kufanya walimu waathirike sana hadi Leo.
 
Ukimzingua mkuu wa shule akupangii kusimamia mtihani wowote, yani wewe utakuwa ni salary to salary
 
Ukimzingua mkuu wa shule akupangii kusimamia mtihani wowote, yani wewe utakuwa ni salary to salary
kuna mwalimu jina lake lilidondoka na kuondoka wilayani kuwa miongoni mwa walimu wanaopangwa kusimamia mtihani, akaanza kum dis mkuu wa shule kuwa anamfanyia mtima nyongo kwa nini haendi kusimamia mtihani miaka nenda miaka rudi anabaki shuleni kupokea wasimamizi wa mitihani huku wenzake wakiena kusimamia na kupata posho. Mkuu wa shule alimuambia hapangi yeye bali ni maofisa wilayani ndio wanaopanga
 
Rais Mwinyi alikuwa mtu mwema sana na mwenye huruma (Mungu amlipe mema huko aliko)
Yeye aliona Mwl Hana posho za katikati ya mwezi kama walivyo watumishi wengine wa umma bali anategemea mshahara tu, ambao haukuwa unakidhi mahitaji ya Mwl Kwa mwezi mzima.

Akaamua kutatua changamoto hii Kwa kuweka posho ya Kila mwezi iliyoitwa posho ya kufundisha (Teaching allowance) ambayo kiasi chake lilikuwa ni asilimia 50 ya mshahara ghafi.
Hii posho ilikuwa haina makato yoyote hivyo Mwl aliipata kama ilivyo. Hii posho ilipandisha sana morali na hadhi ya walimu. Mkapa alikuja iondoa alipoingia madarakani na kufanya walimu waathirike sana hadi Leo.
halafu walimu si wala rushwa, hawakutani na connection za rushwa
 
mimi ni mwalimu, nishaurini nikasomee career gan ili niachane na ualimu, yaan ntoke kabisa kwny fields zinazohusiana na elimu. maana ni balaaaaaa
 
mimi ni mwalimu, nishaurini nikasomee career gan ili niachane na ualimu, yaan ntoke kabisa kwny fields zinazohusiana na elimu. maana ni balaaaaaa
Vya kusoma ni vingi, na hapo halmashauri wahasibu, engineer, n.k walikuwa walimu wakaenda kusoma.
 
Acheni zenu nyinyi wauza ngenge stend
 
Attachments

  • 1787396963207.jpg
    1787396963207.jpg
    104 KB · Views: 10
Back
Top Bottom