Siku nyingine uwe unajitahidi kuficha ujinga wako Mkuu. Kwa kukusaidia tu kama Wewe ni Mtu wa Yanga FC kweli na unayajua ya ndani kabisa fuatilia haraka ujue nini kinaendelea sasa na kwanini Viongozi wa Yanga FC na wale Wabunge wa Yanga huku kukiwepo na Mwakilishi mmoja kutoka SportPesa wanapanga kwenda kutafuta suluhu kwa Uongozi wa Simba SC ili tu Simba wasiende huko FIFA kwa hofu moja kubwa tu kwamba ukweli ukijulikana TFF inaweza kuadhibiwa, Ligi Kusimamishwa na kubwa zaidi kuathiri uwakilishi wa Yanga FC kimataifa na pia kuathiri Udhamini wa SportPesa ambao kuna uwezekano mkubwa wao ndiyo wakawa Main Sponsor msimu ujao wa Premier League.
Jifunze kutofautisha Facebook ambapo kumejazana Wenzako mnaofanana Kiakili na huku JF ambapo ni Home of Great Thinkers.
Simba SC wakienda kweli FIFA Kesho tu asubuhi Yanga FC mtalileta wenyewe Kombe letu mitaa ya Msimbazi. Ombea tu haya mazungumzo yaende vizuri na busara itumike vinginevyo kuna dhahama kubwa inakuja na ambayo itamuharibia sana Rais Malinzi anayetaka kuwa Rais tena wa TFF katika Uchanguzi Mkuu ujao wa mwezi August 2017.