goswe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2018
- 4,880
- 5,763
Haikuorozeshwa sentensi moja ouna koma na funga koma io ni miti mingine .Mwanzo 2:9 inasema wazi
“BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti... na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.”
👉 Ikiwa hii miti miwili haikutoka ardhini, kwa nini imeorodheshwa katika sentensi moja na miti yote iliyochipushwa kutoka ardhini?
Je, Mungu angepotosha wanadamu kwa kuandika kana kwamba miti hiyo ilichipushwa “katika ardhi” ikiwa kweli haikutoka ardhini?
Kila sehemu kwenye Biblia inaposema “mti” (Mwanzo 1:11-12; Ezekieli 47:12; Mathayo 7:17-19) ni mti halisi unaoota ardhini.
Je, ni wapi Biblia imetumia neno “mti” kwa maana ya tendo la ngono?
Je, kwa nini Mungu aliwazuia Adamu na Hawa wasiule tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya (chakula), kama kweli “tunda” lingekuwa tendo la ngono?
Je, unamaanisha Adamu na Hawa
waliumbwa wasiwe na ngono?
NIKISEMA BRANHAM NI NABII WA UONGO NITAKUWA NAKOSEA?
Soma io sentensi.