Hii ndiyo huenda ikawa sababu ya mgongano wa viongozi wa dini

View attachment 3510824View attachment 3510825

My people,​

Haya yanayoendelea sasa ni kiporo cha mambo ya nyuma ila bahati mbaya kiporo hiki kinapashwa na ubwabwa wa leo,ndio maana tunaona huu msuguano ambao unaendelea hivi Sasa

Ukiangalia historia huko nyuma TEC imekuwa ikilaumiwa kama kizingiti cha baadhi ya mambo ya Waislamu au haki zao kupewa kipaumbele,mfano haki ya kupata Mahakama ya Kadhi,hii mahakama si jambo la kustaajabisha sana,ni kutokuwa na elimu tu ni namna gani inafanya kazi,lakini ni mahakama ambayo inadili na ndoa na mirathi,sitozungumzia sana hapa kwani lengo sio hilo.

Kumekuwa na hitajio la kujiunga na Umoja wa nchi za kiarabu kwa dhumuni la kupata misaada kwa Waislamu kusaidia kutoa huduma mbali mbali za kijamii,hili nalo TEC wamekuwa mwiba katika kufanikiwa kwake

Kumekuwa na Memorandum of Understanding kati ya Serikali na Kanisa ambapo Kanisa linapewa hela na Serikali ili kufanikisha huduma kwa jamii kama hospital na mashule,swali linakuja je Waislamu hawastahili haya?

Kwahiyo ukiangalia kwa mapana yake kuna mambo ambayo Kanisa limefaidika moja kwa moja kutoka Serikalini na wakati Kanisa hilo hilo limekuwa kikwazo kwa Waislamu kushindwa kufikiwa kwa matakwa yao

Na kuna shutuma kwamba TEC imekuwa inatoa matamko mengi sana pindi tu Raisi anapokuwa Muislamu,na kuna taarifa kwamba ile misamaha ya kodi kwa vifaa vya ambavyo vinaagizwa na taasisi za dini,imeondolewa baada ya kugundulika kwamba viongozi hao wanatumia mgongo huo kwa manufaa yao binafsi,sasa Mama Samia Kachomoa king'amuzi watu wanashindwa kuangalia television,ndio makelele hayo mnayosikia kila kukicha,lakini upande wa pili kuna agenda yao

Sasa ukiangalia kinachotokea leo ni kweli TEC wanapigania haki na malalamiko ambayo watanzania wengi tunayo,lakini upande wa pili wanaamsha dude ambalo lilikuwa limelala,ndio hayo unayosikia Kobazi nao wanaliamsha.

Kwahiyo sio kwamba Kobaz hawajielewi,au wanaropoka hovyo au hawajaenda shule kama baadhi yenu mlivyojawa na propaganda za zamani kwamba Waislamu hawana shule kichwani,acheni hizo fikra zenu hasi

Kwahiyo kuna kiini cha haya mambo ambayo bado hayajatafutiwa ufumbuzi kati ya Waislamu na Wakristo ambayo nayo inatakiwa itafutiwe Tume ya kujua Chanzo na Kujua suluhisho lake

Ila haya kwasasa yasubiri kwanza,tudili na lile kubwa ambalo lipo mbele yetu,kikubwa sisi wafuasi wa dini tusiingie kwenye uhasama wa dini zetu,tuendelee kuwa imara kupendana na kuvumiliana kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote

Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
Tec wanapinga utekaji full stop utekaj haukubaliki
 
1. MaSheikh wapo sawa kupinga Maandamano ya kihuni ambayo madhara yake ni makubwa mno na sioni ubaya kupinga Maandamano ya namna hiyo
Maandamano ni HAKI ya KIKATIBA. Jambo la MSINGI ni UTAWALA wa SHWRIA ufuatwe.

Kama watu wanatekwa maana yake MAHAKAMA hazifanyi kazi.

Kama watu wanataka kuandamana na wanatoa TAARIFA wanapigwa marufuku, yakitokea maandamano usitegemee amani hapo maana tangu mwanzo ulikataa kufuata utaratibu.

Suala la Masheikh kupinga maadamano halizuii watu wakitaka kuandamana.

Na yakitokea, Samia akileta MAGAIDI yake yakirusha RISASI haziulizi DINI, ndio maana SHEIKH MAJINI KAFA.
2. Wamekataa unafiki wa Wakatoliki kuhubiri haki wakati Waislamu wakipigania haki zao na kuonewa hawasemi kitu Wala kusapoti mfano
Unafiki gani?

Kazi yao ni KUSEMA UKWELI na HAKI.

Hawajasema wanatafuta watu wa kuwaunga mkono.
;
I)Mauaji ya Waislamu mwembe chai ,
TEC Ndio waliua?
ii) Mauaji ya Pemba
TEC ndio WALIUA?
iii ) MaSheikh kuonewana kesi za ugaidi , bila kufungukiwa mashtaka
TEC ndio wanawaonea kwa kesi??
iii) Mahakama za kadhi
Nani kawakaza kuanzisha?

Ni TEC?
iv) nk
Hapo Wakatoliki watetezi wa haki walikuwa wapi wakati Waislamu wanaonewa na kudai haki zao ?
Unatakiwa kupambania haki yako kutoka kwa yule anayekunyima.

TEC siyo msemaji wa WAISLAM.

TEC wanasemea watu haki ambazo ni MASLAHI ya kila mtu akiwemo MPAGANI.
Zipo clip kiongozi wa kikiristo akitaka Rais Samia asivae hijabu , huo sio uchokozi wa kidini ?
Leta hapa hiyo CLIP??
 
Mwambie akupe hiyo clip ambayo inassma asivae hijab. Mwambie akutumie hata inbox,
Huwa mnalishana uongo. Mchungaji anawezaje kumpangia raisi avae nini?
Hawa watu, SHULE HAKUNA. Masheikh wao pia SHULE hakuna.

Halafu ndio wanaowasikiliza kwa 100% .

Sasa kama wanataka kuwasikiliza hao Masheikh wao, wawapeleke shule basi.
 
Hakuna MTU wala SERIKALI haijawahi kukataza wala kupinga WAISLAMU kuwa na MAHAKAMA ya KADHI.

Shida kubwa ya WAISLAMU hawataki kuanzisha hiyo MAHAKAMA wao wenyewe.

Wanataka iwe kwenye MFUMO wa SERIKALI, kisheria na IENDESHWE kwa KODI za umma.

Sasa ukishafika hapo, maana yake MFUMO wa KAWAIDA wa MAHAKAMA uliopo unatakiwa KUFA na badala yake kila JAMII yenye mfumo wake wa HAKI ifanye KAZI

TZ siyo DOLA la KIISLAM ila ni SECULAR, sasa kwa akili zenu NCHI inajiunga vipi kwenye JUMUIYA ya NCHI za KIISLAM wakati siyo NCHI YA KIDINI???

Halafu sababu yenyewe eti KUPOKEA MISAADA???

Memorandom of Understanding inasemwa sana, na watu wamekaza FUVU hawataki kabisa kuelewa tofauti.

Serikali haitoi hata 100 kuendesha TAASISI za DINI, ila kinachofanyika ni PESA zinatoka kwa WAKRISTO WA UJERUMANI zinakuja nchini.

Serikali inatoa MSAMAHA wa kodi na WATUMISHI kwa baadhi ya Hospitali kwa masharti kuwa:
  • Hizo taasisi za dini zihudumie watu wote bila UBAGUZI
  • Zifuate SERA YA NCHI ya Afya kama MATIBABU BURE kwa WAZEE, WATOTO na WAJAWAZITO.

Huo msamaha ulikuwepo kwa SHERIA ipi??

Matamko yanakuwa mengi kadri unavyoboronga.

Sasa wewe UNAUWA na KUTEKA watu, unataka watu timamu wenye AKILI TIMAMU wanyamaze??

Unataka kutawala MAJIVU???

Kwasasa tunaye MKAZA mwana wa Samia, Mohamed Mchengerwa yeye AFUTE hiyo memorandom hata muda huu, maana watu wanabonga vibaya sana.

Au aweke wazi ni pesa kiasi gani SERIKALI imetoa imewapa taasisi za DINI.

Umewahi kusikia hizo pesa hata kwenye KAGUZI za CAG??
This is as true as it gets!
 
Maandamano ni HAKI ya KIKATIBA. Jambo la MSINGI ni UTAWALA wa SHWRIA ufuatwe.

Kama watu wanatekwa maana yake MAHAKAMA hazifanyi kazi.

Kama watu wanataka kuandamana na wanatoa TAARIFA wanapigwa marufuku, yakitokea maandamano usitegemee amani hapo maana tangu mwanzo ulikataa kufuata utaratibu.

Suala la Masheikh kupinga maadamano halizuii watu wakitaka kuandamana.

Na yakitokea, Samia akileta MAGAIDI yake yakirusha RISASI haziulizi DINI, ndio maana SHEIKH MAJINI KAFA.

Unafiki gani?

Kazi yao ni KUSEMA UKWELI na HAKI.

Hawajasema wanatafuta watu wa kuwaunga mkono.

TEC Ndio waliua?

TEC ndio WALIUA?

TEC ndio wanawaonea kwa kesi??

Nani kawakaza kuanzisha?

Ni TEC?

Unatakiwa kupambania haki yako kutoka kwa yule anayekunyima.

TEC siyo msemaji wa WAISLAM.

TEC wanasemea watu haki ambazo ni MASLAHI ya kila mtu akiwemo MPAGANI.

Leta hapa

👏
 
Hakuna mgongano, ni mada iliyotengenezwa ili kubalansi mambo.
 
Hakuna MTU wala SERIKALI haijawahi kukataza wala kupinga WAISLAMU kuwa na MAHAKAMA ya KADHI.

Shida kubwa ya WAISLAMU hawataki kuanzisha hiyo MAHAKAMA wao wenyewe.

Wanataka iwe kwenye MFUMO wa SERIKALI, kisheria na IENDESHWE kwa KODI za umma.

Sasa ukishafika hapo, maana yake MFUMO wa KAWAIDA wa MAHAKAMA uliopo unatakiwa KUFA na badala yake kila JAMII yenye mfumo wake wa HAKI ifanye KAZI

TZ siyo DOLA la KIISLAM ila ni SECULAR, sasa kwa akili zenu NCHI inajiunga vipi kwenye JUMUIYA ya NCHI za KIISLAM wakati siyo NCHI YA KIDINI???

Halafu sababu yenyewe eti KUPOKEA MISAADA???

Memorandom of Understanding inasemwa sana, na watu wamekaza FUVU hawataki kabisa kuelewa tofauti.

Serikali haitoi hata 100 kuendesha TAASISI za DINI, ila kinachofanyika ni PESA zinatoka kwa WAKRISTO WA UJERUMANI zinakuja nchini.

Serikali inatoa MSAMAHA wa kodi na WATUMISHI kwa baadhi ya Hospitali kwa masharti kuwa:
  • Hizo taasisi za dini zihudumie watu wote bila UBAGUZI
  • Zifuate SERA YA NCHI ya Afya kama MATIBABU BURE kwa WAZEE, WATOTO na WAJAWAZITO.

Huo msamaha ulikuwepo kwa SHERIA ipi??

Matamko yanakuwa mengi kadri unavyoboronga.

Sasa wewe UNAUWA na KUTEKA watu, unataka watu timamu wenye AKILI TIMAMU wanyamaze??

Unataka kutawala MAJIVU???

Kwasasa tunaye MKAZA mwana wa Samia, Mohamed Mchengerwa yeye AFUTE hiyo memorandom hata muda huu, maana watu wanabonga vibaya sana.

Au aweke wazi ni pesa kiasi gani SERIKALI imetoa imewapa taasisi za DINI.

Umewahi kusikia hizo pesa hata kwenye KAGUZI za CAG??
Kwa mfano, tukiishi bila kuwa na dini yoyote ile, yaani tuishi kipagani pagani tu, kutakuwa na tatizo lolote?​
 
Hayo ni mambo binafsi.

Ndio maana SERIKALI ni PAGANI, na MSAHAFU wake ni KATIBA na SHERIA
 
Dini ilikuja ili kuwafanya watu wawe wastaarabu na kujali utu, sasa kama watu hawawi wastaarabu si bora warudi kwenye upagani tu?​
 
View attachment 3510824View attachment 3510825

My people,​

Haya yanayoendelea sasa ni kiporo cha mambo ya nyuma ila bahati mbaya kiporo hiki kinapashwa na ubwabwa wa leo,ndio maana tunaona huu msuguano ambao unaendelea hivi Sasa

Ukiangalia historia huko nyuma TEC imekuwa ikilaumiwa kama kizingiti cha baadhi ya mambo ya Waislamu au haki zao kupewa kipaumbele,mfano haki ya kupata Mahakama ya Kadhi,hii mahakama si jambo la kustaajabisha sana,ni kutokuwa na elimu tu ni namna gani inafanya kazi,lakini ni mahakama ambayo inadili na ndoa na mirathi,sitozungumzia sana hapa kwani lengo sio hilo.

Kumekuwa na hitajio la kujiunga na Umoja wa nchi za kiarabu kwa dhumuni la kupata misaada kwa Waislamu kusaidia kutoa huduma mbali mbali za kijamii,hili nalo TEC wamekuwa mwiba katika kufanikiwa kwake

Kumekuwa na Memorandum of Understanding kati ya Serikali na Kanisa ambapo Kanisa linapewa hela na Serikali ili kufanikisha huduma kwa jamii kama hospital na mashule,swali linakuja je Waislamu hawastahili haya?

Kwahiyo ukiangalia kwa mapana yake kuna mambo ambayo Kanisa limefaidika moja kwa moja kutoka Serikalini na wakati Kanisa hilo hilo limekuwa kikwazo kwa Waislamu kushindwa kufikiwa kwa matakwa yao

Na kuna shutuma kwamba TEC imekuwa inatoa matamko mengi sana pindi tu Raisi anapokuwa Muislamu,na kuna taarifa kwamba ile misamaha ya kodi kwa vifaa vya ambavyo vinaagizwa na taasisi za dini,imeondolewa baada ya kugundulika kwamba viongozi hao wanatumia mgongo huo kwa manufaa yao binafsi,sasa Mama Samia Kachomoa king'amuzi watu wanashindwa kuangalia television,ndio makelele hayo mnayosikia kila kukicha,lakini upande wa pili kuna agenda yao

Sasa ukiangalia kinachotokea leo ni kweli TEC wanapigania haki na malalamiko ambayo watanzania wengi tunayo,lakini upande wa pili wanaamsha dude ambalo lilikuwa limelala,ndio hayo unayosikia Kobazi nao wanaliamsha.

Kwahiyo sio kwamba Kobaz hawajielewi,au wanaropoka hovyo au hawajaenda shule kama baadhi yenu mlivyojawa na propaganda za zamani kwamba Waislamu hawana shule kichwani,acheni hizo fikra zenu hasi

Kwahiyo kuna kiini cha haya mambo ambayo bado hayajatafutiwa ufumbuzi kati ya Waislamu na Wakristo ambayo nayo inatakiwa itafutiwe Tume ya kujua Chanzo na Kujua suluhisho lake

Ila haya kwasasa yasubiri kwanza,tudili na lile kubwa ambalo lipo mbele yetu,kikubwa sisi wafuasi wa dini tusiingie kwenye uhasama wa dini zetu,tuendelee kuwa imara kupendana na kuvumiliana kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote

Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
Wanapigania haki zao kwa kutishia kuwakata watu mapanga?. Nimesikiliza press ya Kitima mwanzo mwisho. Hakuna sehemu yoyote aliowasema vibaya waislamu wala dini ya uislamu.
 
Hao walio Sema hayo sio MaSheikh ni waislamu wenye mihemko tu maadam wamepewa airtime basi wakaropoka waliyoropoka

Wala sio mafundisho ya dini yetu wala mwenendo wake,bahati mbaya sana yeyote akivaa kanzu na baraghashia basi huwa ni Sheikh

Tamko hilo lingetamkwa na Bakwata au Baraza la Maulamaa lingekuwa na uhalali wa kusema kuwa Waislamu wametoa kauli zenye utata

Kwahiyo lipuuzieni tu
 
Dini ilikuja ili kuwafanya watu wawe wastaarabu na kujali utu, sasa kama watu hawawi wastaarabu si bora warudi kwenye upagani tu?​
UTU ni hulka ya binadamu tu...

Haufundishwi na DINI.
 
ila hii nchi aliyesema watakaoandamana atawakata vichwa yupo huru kuliko wanaodai haki wanaonekana wachochezi
 
Wao wanaamini ili wapewe hiyo MISAADA inatakiwa NCHI ijiunge OIC.
Kuna mtu humu nimetoka kumuambia wana unyonge wa asili. Wao neno kuonewa lipo mbele ikiwa si kweli.
Mufti kakutana na serikali ya Saudi Arabia, amesaini nao MoU. Haya wawaombe Saudi Arabia wawasaidie iwe misikiti, shule au hospital. Saudi Arabia ni taifa tajiri wawaombe yote hayo, lakini wanasubiri kusema TEC haiwapendi
Screenshot_20251203-215114_1.jpg
 
Hao walio Sema hayo sio MaSheikh ni waislamu wenye mihemko tu maadam wamepewa airtime basi wakaropoka waliyoropoka

Wala sio mafundisho ya dini yetu wala mwenendo wake,bahati mbaya sana yeyote akivaa kanzu na baraghashia basi huwa ni Sheikh

Tamko hilo lingetamkwa na Bakwata au Baraza la Maulamaa lingekuwa na uhalali wa kusema kuwa Waislamu wametoa kauli zenye utata

Kwahiyo lipuuzieni tu
Kwanini hawachukuliwa hatua za kisheria?. Niffer alifanya challenge ya nywinywi tu akafunguliwa mashtaka ya uhaini, ndio kusema nchi hii kucheza mziki ni hatari zaidi ya kutishia kukata watu mapanga
 
Sasa mbona mashekhe wanaliandama kanisa moja kwa moja ilhali kanisa halijihusoshi na wala haliwataji popote.

Sijawahi kuona tamko la TEC kuwaongelea waislam, ila mataka ya waislam kwa wakristo/TEC ni hayahesabiki kwakweli.

Fafanua ni kwa namna gani wakatoliki wanazuia hayo uliyoandika, nadhani ni jinsi waislam wenyewe hawajui namna ya kushawishi/kuomba jambo.
Unajua nimesikiliza speech za hawa maaskofi hakuna popote nilipoona wamewasema vibaya waislamu. Huwa nashindwa kuelewa hawa mashehe wamechafukwa na nini.
 
Back
Top Bottom