Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, amani iwe kwenu.
Habari inayotrend kwa sasa ni tukio la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kumkataza mkewe kutofuatana naye Dar kwa ajili ya kesi ya Kamanda Wema Sepetu. Mke wa Lema amesikika akimshauri mumewe kufuatana naye Dar es Salaam kwa ajili ya kesi hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa leo kabla haijaahirishwa. Hata hivyo, Godbless Lema alimsihi mke wake abaki nyumbani aangalie watoto wakati yeye anapambana kumsaidia kamanda Wema ambaye ameonesha uungwana wa kwenda Arusha mara mbili kwa ajili yake.
Inadaiwa kuwa awali Mama Lema hakuwa tayari kumuacha mumewe aende pekee Dar es Salaam kwa madai kuwa usalama wake upo mashakani. Hata hivyo, Lema alimtoa hofu hasa baada ya kumhakikishia kuwa ataambatana na Kamanda Kalist Mabina.
Godbless Lema atakuwa Jijini Dar es Salaam kwa siku kadhaa kwa ajili ya maandalizi ya hafla ya kumkabidhi Kadi ya CHADEMA Kamanda Wema na kwamba wawili hao watakuwa wanakutana mara kwa mara na wakati wowote kwa ajili ya kukamilisha hafla hiyo ambayo inadaiwa kuwa itakuwa ya aina yake