Hii ndiyo sababu ya matajiri kuwa na watoto wachache

Hii ndiyo sababu ya matajiri kuwa na watoto wachache

Basi Mzee wangu alikuwa Tajiri sana watoto 17
Kama aliweza kuwalea vizuri na kuwatunza na bado akawa tajiri hao 17 hawakua wengi kwake...

Nikisema wengi namaana watoto wengi hadi kushindwa kuwahudumia au kujijengea mazingira ya kiuchumi yako binafsi ukizeeka...
 
Au uzae watoto wengi uwekeze katika majukumu uitwe maskini na ubaki ukilaumu kuwa watoto hawakusaidii.
Kuna masikini hawana watoto kabisa, kuna masikini wana raha kuliko matajiri, kuna matajiri hawana dhiki ila wana shida zisizoisha, kwa maana hiyo maisha ni naturally configured na hayana formular, let nature take its course for everyone
 
Acha kujifariji mkuu. Zaa watoto wachache ili upate akiba ya kuwasaidia wale wasio na baba wala mama. Alafu kumbuka world resources are so limited lakini idadi ya watu inaongezeka kila uchao.
Kuzaa watoto ni jukumu langu, siwezi kuchukua kitu ambacho si jukumu langu kikaingilia au kuathiri jukumu langu. Kwani wewe unalea watoto wangapi yatima? Pamoja na hayo yote kusaidia ni moyo wa mtu na ndio maana hata masikini wanasaidiana wenyewe kwa wenyewe kwa kile kidogo wanachopata.
 
Kuzaa watoto ni jukumu langu, siwezi kuchukua kitu ambacho si jukumu langu kikaingilia au kuathiri jukumu langu. Kwani wewe unalea watoto wangapi yatima? Pamoja na hayo yote kusaidia ni moyo wa mtu.
Unasikitisha sana. Laiti kama wazungu wangekuwa na mentality kama hii, basi hata ndugu zetu wasingepata msaada wa ARVs
 
Ni kiasi gani dunia inapoteza katika kutekeleza familly planning kwa ukuaji wa uchumi wa watu binafsi na dunia...?

Tuache basi kusema utajiri maana ni kama neno lenye ukakasi tuseme uchumi bora...

Na wakati huo huo fahamu tajiri hawezi kujaribu mbinu za mtu maskini...

Kupinga ukweli ni kuipinga asili.
Fahamu tajiri hana muda wa kufanya ngono muda wake wote anawaza kutumikia mali yake,masikini akisha kula na kushiba achoeaza ni kutia tu

Ifahamike kuwa na watoto wengi sio sababu ya kuwa masikini na kuwa na mtoto 1 sio sababu ya kuwa tajiri
 
Fahamu tajiri hana muda wa kufanya ngono muda wake wote anawaza kutumikia mali yake,masikini akisha kula na kushiba achoeaza ni kutia tu

Ifahamike kuwa na watoto wengi sio sababu ya kuwa masikini na kuwa na mtoto 1 sio sababu ya kuwa tajiri
Kwa mawazo hayo

Fanya tuweke uhalisia

Swali je Gharama za kuhudumia mtoto mmoja ni sawa na Gharama za kuhudumia watoto watano...????

Naomba jibu???
 
Mmoja au wawili tu baaas
Utajiri ni kipaji kuzaa mtoto 1 au wengi au kuishi bila familia sio kigezo cha kuwa tajiri unaweza kuwa na watoto kama timu ya simba lakini utajiri ukakuijia tu wengi miaka hii hawazai kabisa au wakizaa ni mtoto 1 au 2 ajabu wanashida mpaka sura zao zinaonyesha walivio choka
 
Acha kujifariji mkuu. Zaa watoto wachache ili upate akiba ya kuwasaidia wale wasio na baba wala mama. Alafu kumbuka world resources are so limited lakini idadi ya watu inaongezeka kila uchao.
Bila shaka wewe unae mtoto 1 au 2 taja unamiliki nini katika mali kuliko wanye watoto 6?
 
Ni kweli jamaa anavyosema kuwa matajiri wanawagharamia sana watoto wao , kwa chakula,kiafya kimasomo, mf. Mtu anapelekwa nje kusoma , akirudi anapewa hela ya kufungua biashara kweli
Ukitaka kuwa tajiri usioe ndugu ishi wewe pekee yako tu
 
Unajidanganya huko kwawarabu mambo yakuoa wake wa 4 wala hawaya entertain ila masheikh wahuku pangu pakavu ndo balaa
Wewe mpaka sasa huna hata mke wala mtoto je uwekeza nini?
 
kuna vitu ukiwashauri watu hata hawawezi kukuelewa. ishi wewe uavyoona ila hepuka kuwapangia watu waishije. ila dhibiti usiumizwe na uzembe na kutokujali kwa mtu mwingine. ndugu yako akizaa usimsaidie kulea mwache apambane na hali yake. binadamu wa leo wabishi sanaa.
 
Bila shaka wewe unae mtoto 1 au 2 taja unamiliki nini katika mali kuliko wanye watoto 6?
Mgawanyo wa matumizi hutegeme Kipato kilichopo

Ni kiwa na maana kama vipato vinatofautiana ni sahihi pia matumizi yatofautiane...

Jambo la msingi hapa ni uwiano wa mapato yako na matumizi na akiba yako ya uzeeni.

Kua na watoto 6 si idadi kubwa au idadi ndogo

Inategemeana na kipato chako...

Kuna mwingine mtoto mmoja tu ni mzigo ndo maana kuna wengine wanatupa watoto na kuna mwingine watoto 10 si kitu kwake...

Msingi wa hoja hii ni kutambua binadamu anapozaliwa ni gharama katika kukua kwake hadi kujitegemea...

Gharama hizi ni Juu ya nanniiiiiii?

Ni yule aliye mleta duniani...

Sasa kama ukileta binadamu wengi duniani na ukashindwa kuwatunza na kuwahudumia kwa misingi husika fahamu kua wewe umemkosea Mungu na dunia yenyewe na huyo mwanao...

Kwa kifupi ifahamike maana ya idadi ya watoto wachache au wengi inategemeana na vile mzazi unavyoweza kuwahudumia kimsingi na wewe ukabaki na akiba yako ya uzeeni....

FULL STOP.
 
Mimi hata kama sina uwezo, ikitokea afya ikaruhusu nitazalisha watoto wakutosha.

Kwanza huku Uswahili tunasema kila mtoto anakuja na bahati yake
 
Mimi hata kama sina uwezo, ikitokea afya ikaruhusu nitazalisha watoto wakutosha.

Kwanza huku Uswahili tunasema kila mtoto anakuja na bahati yake
Kila mtoto anakuja na baraka zake....Kitaaluma hiyo ni BETTING...

Kanuni hizi ndio huzalisha makahaba na vibaka...!

Binadamu waliokosa msingi wa malezi na kesho yao,ikiaminika watakuja kujitafutia wenyewe....!
 
Back
Top Bottom