Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Baba yangu alifariki wakati nikiwa Mtoto mchanga hivyo nililelewa na Mama tu naye hakuwa na uwezo hivyo nilisomeshwa na wasamaria wema. Mtu pekee Aliyekuwa na uwezo wa kiuchumi ni dada aliyeolewa na yeye hakutaka mazoea kabisa.

Kwa jinsi maisha yalivyokuwa magumu, nilipofika Chuo nikawa natumia boom(mkopo wa elimu ya juu) kumtunza mama. Imagine mtu nilikuwa nalipwa laki tano na kumi na kupaswa niitumie kwa miezi miwili lakini nilikuwa najibana kwa kadiri iwezekanavyo nitumie mama Kati ya elfu 60 na 100,000.

Nilipomaliza chuo nikarudi nyumbani, hakuna ajira na sina mtaji wa biashara au kilimo, nikawa nashinda ndani kwa mawazo au siku nikibahatisha kibarua Cha zege au kumsafishia mtu shamba naifanya kwa nidhamu, napata hela ya bundle la muendelezo wa kusaka ajira.

Ajabu ya karne; Mama mzazi alianza kunisimangia chakula na kunilaumu kuwa nilitumia vibaya mkopo wa Chuo nilikuwa nawapa makahaba wa mjini na kwamba ningekuwa na akili ningetambua kuwa mimi ni Mtoto yatima na ningetunza akiba ili nimalizapo chuo nifungue kioski!

Mungu siyo Shetani, baada ya miaka miwili ya ukosoefu wa ajira, nikapata kazi nzuri Sana kwenye moja ya taasisi za Kimataifa, nimeanza kusahau yale maisha magumu. Nimewekeza katika ardhi, nimenunua ekari 50, nimenunua viwanja viwili Arusha mjini na kimoja Kibaha. Kwa Sasa nawaza kununua power tiller(KUBOTA) ili inisaidie kwenye kilimo ambacho nitakianza mwakani rasmi.

Sasa nikikumbuka vituko vya mama, na Ndugu kuwatumia hela napata taswira ya yale maneno yale masimango. Naghairisha.

Yule dada Aliyekuwa na uwezo wa kunisomesha akagoma, Benki imewafilisi, wakaachana na mumewe. Amebaki kunipigia simu eti "nilikuwa nakusalimu" wakati kipindi nipo down hakuwahi kunipigia na nikimpigia hapokei simu, nikimpigia kwa number ngeni akishafahamu Ni mimi, anakata.

Maisha ya hapa Duniani ni fumbo
 
Baba yangu alifariki wakati nikiwa Mtoto mchanga hivyo nililelewa na Mama tu naye hakuwa na uwezo Hivyo nilisomeshwa na wasamaria wema. Mtu pekee Aliyekuwa na uwezo wa kiuchumi Ni dada aliyeolewa na yeye hakutaka mazoea kabisa.

atumia hela napata taswira ya yale maneno yale masimango. Naghairisha.

Yule dada Aliyekuwa na uwezo wa kunisomesha akagoma, Benki imewafilisi, wakaachana na mumewe. Amebaki kunipigia simu eti "nilikuwa nakusalimu" wakati kipindi nipo down hakuwahi kunipigia na nikimpigia hapokei simu, nikimpigia kwa number ngeni akishafahamu Ni mimi, anakata.

Maisha ya hapa Duniani ni fumbo
Mama msaidie wengine piga chini
 
Back
Top Bottom