Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Kwahiyo unajiona hapo umemaliza yaninkuwa na Viwanja viwili na mshahara WA milion 2 unaona ni hela nyingi.

Saidia watu kijana Acha kulipiza visasi kila MTU duniani ana nafasi yake awe masikini au Tajiri. Ndio maana hata Bakhrresa anamtegemea masikini awe mteja wake WA bidhaa. Usiishi Kwa visasi. Hizo Mali ulizonazo ni ndogo Sana na chache usitake kujiona umefika kuanza kuwadharau watu. Kwanza Mali zenyewe sio Cash inflow kwako means siku ukivuruga kazini ukapigwa chini utauza hizo Viwanja ....


Wewe ndio inabidi uwe mwanzo WA tabia mpya kwenye familia. Vunja roho za visasi
 
Huyo sista hako chinjia baharini

Miye Nina mantra moja tu:

Kama hukunipenda au kunithamini nikiwa chini basi usipoteze muda wako siku nikizipata nikawa juu

Kaa mbali na mimi
 
Miye kama hukunijali kipindi nipo chini,siku nikizipata pita hivi
 
Mama kama binadamu mwingine anaweza kufanya makosa .

Sio mama wote wanapenda watoto wao,

Tusikariri,

Wengine walifanya kila jitihada kutoa hiyo mimba Mungu akakataa.

Sasa mama wa hivyo unazani atakupenda?

Wengine wamejikuta wamezaa tu wala hawakupanga kumzaa huyo Mtoto.

Mtoto anakuwa na Roho ya kukataliwa
 
Kwanza mshukuru Mungu kwa kila Jambo,hizo shida ulizopitia ndiyo ulikua mpango wa Mungu ili wwe utoke kimaisha,na ungesaidiwa na ndg ungebweteka,na hadi Leo ungekua Mtu wakusaidiwa tu!! Kwa hiyo usiwachukie sana ndg zako,mradi umesha wajua rohoo zao,basi wwe ishii nao kwa akili maana huwezi jua kesho yako hata kama tayari uko vizuri kiuuchumi, Maisha saa yoyote ile yanabadilika,na siyo Kiuchumi tu,hata kiafya!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wasaidie tuu ndugu yangu,Utapata baraka zaidi kwa Mungu!
 
Sometime, inabidi ujue mtu huwa anaamini kwa anachokiona na uelewa wenu hauko sawa kati ya wewe na Mama yako.

Usiamini kwamba Mama hakutakii mema, na kweny maisha yote tangu baba ako afariki usimuhukumu Mama kwa suala la kukusimanga tuu,nadhani hilo ni sehem ya mengi.

Weka mzani wa mazuri na mabaya yake, remember kulea mtoto mpaka awe na akili sio kitu rahisi.
 
Kuna watu mnapenda kutetea ujinga,hivi watu waliokutosa ukiwa mtoto wanaweza kukusaidia kipi hasa ukiwa mtu mzima? Ndugu wa namna hiyo akirudi anakuwa amerudi kimaslahi tu, na kamwe asingerudi ungeendelea kuwa kapuku.
Kama wao ndo walilianzisha inabidi muishi humo humo hakuna namna.
 
ili upate mafanikio zaidi wasamehe wote
 

Huyo dada amkatae ila sio Mama, kisa tuualitoa lugha ya masimango, ilhali kashasema mama maisha aliyoyapitia, unaona kabisa mategemeo yake kwa mwanafunzi wa chuo yalikuwa yapi, sometime mabimkuwa ni stress, umri, na ugumu wa maisha ndio huwafanya yote hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…