Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una Waislam tupu. Nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo. Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.

Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu. Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.

Allahu akbar.

PS: Yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.
Unaposema kila mtu huzaliwa muislam, hilo umelijua ukiwa bado mkristo au uliposlimu ndo ukafundishwa hivyo?
 
Uislam ndiyo dini bora kwa binadamu.
Kuna hikma nyingi sana katika maswala ya kibinadamu kama ndoa,mirathi,mazishi nk.

west saivi Kuna crisis ya ndoa, ndoa nyingi zinavunjika wanawake hawashikiki, mambo ya haki sawa na Ushoga umetamalaki.

solution ya yote haya ni uislam
We jamaa hili jina nimeanza kuliona toka mi nimejiunga humu unatetea uislam then unasema umeslim mwaka huu? Dini yenu mnapenda kuieneza kwa matukio ya uongo uongo tu.
 
Yan mapepo yamekuotesha ndoto badala ukemee nawew ukamua kuyafuata.... Maandiko yanasema nahali yamtu yule itakua mbaya kuliko ya awali
 
Maandiko gani? Maandiko pekee nayoamini ni Quran
 
Una uhakika wa kukuta mabikra kibao, wewe kazi yako itakua moja tu. Kutoa hizo bikra zao huku ukinywa pombe tamu inayotiririka kwenye mitomito.
 
True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una Waislam tupu. Nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo. Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.

Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu. Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.

Allahu akbar.

PS: Yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.
Sawa.
 
Karibu sana hapa kwangu nashuhudia kuslim kwa vijana wangu wasaidizi wa kazi......
Alianza dada wa kazi na aliniambia muda kuwa anataka kuslim ila nikampotezea.Kila mara yeye ni kusikiliza qaswida,kujitanda yani aliyapenda mambo ya kiislamu ijapo hakuna aliye mwambia lolote juu ya hayo.Siku si nyingi akaniambia anataka kujifunza kuswali na quran yani alitaka aanze madrassa sasa hapo nikaona yupo serius hivyo nikamslimisha na hadi sasa kawazidi hata hao waislamu wakuzaliwa kiimani.

Kijana wa ofisi kwangu nae tangu mwezi ule wa ramadhan basi maswali yakawa mengi juu ya uislamu huku nae ni mluther tena mchaga.Nikawa namwambia mengi na kumkaribisha kujiunga ila akagoma kwa wakati huo.Aliendelea na kujifunza kuhusu uislamu youtube na huko alikutana na akina mazinge na wajuzi wengine akajifunza ambayo hakuwahi kujifunza kabla.Kiukweli alijifunza mwenyewe na kusikiliza tafsiri ya quran kiswahili na aliipenda kwakweli mana haipiti siku hajasikiza sura yoyote.Basi siku sinyingi akaniambia broo nataka kuslim basi chap tu tukamslimisha.Nikachukua jukum lakumfunza niyajuayo na yale ya msingi hasa kuusu swala na hadi sasa swala tano zimemkaa na naona kama anafuga ndevu yani nae kawazidi hao waliozaliwa kwenye uislamu.

Kijana mwingine wa kazi..Huyu niwazamani kabla ya huyo wa hapo juu huyu hajaslimu ila alionyesha kuupenda uislamu ila kama angenitamkia anataka kuwa muislamu nahisi nae angekuwa ila aliishia kuupenda tu.
Jamani Nawashauri waislamu kujipamba na tabia njema kwani izo ndizo humvutia asiyekuwa muislamu kujiunga na uislamu.Ijapo wengine hujisomea nakuujua wengine ndoa nk ila nahisi na kuamini ili la tabia huwahamasisha zaidi.
 
Mashallah
 
Uislamu huwa unaenezwa kwa propaganda sana angalia kisa cha kutunga ulichokitoa hapa
sasa niongope ili nisaidike nini kama upo morogoro njoo nikukutanishe nao.Binti aliyeslim alikuwa anaitwa Winfrida now anaitwa Salha,Kijana aliyesilimu alikuwa anaitwa Allen now anaitwa Abdulkareem huo ndio ukweli wala sikulazimishi kusadiki haya.
 
Yesu ndiye Kristo, ndio maana sisi tunaomfuata tunaitwa wakristo, yaaani watu wa Kristo. na hiyo sio dini, ni maisha halisi. ukija kwa mlengo wa dini umepotea, na dini haimfikishi mtu popote.
Yesu dini yake ni ipi? Maana nae pia alikuwa anafanya Ibada
 
sasa niongope ili nisaidike nini kama upo morogoro njoo nikukutanishe nao.Binti aliyeslim alikuwa anaitwa Winfrida now anaitwa Salha,Kijana aliyesilimu alikuwa anaitwa Allen now anaitwa Abdulkareem huo ndio ukweli wala sikulazimishi kusadiki haya.
Kwanini waache majina yao waitwe ya kiarabu?
 
hakuna jila la kiarabu bali kuna majina ya kiislamu....jina ni jina ila mtume amefundisha watu kuitwa kwa majina wayapendayo kwa kuzingatia sheria za majina ikiwemo jina lisiwe jina la mwenyezi mungu (yapo 99) unaweja kuyatumia kwa kulinza na neno mja mfano mja wa mkarimu (abdulkareem)...kuna majina hupendeza muislamu akiitwa kwayo.Sio lazima aliyeingia kwenye uislamu kubadili jini bali hupendekezwa ili kuendana na majina mazuri yanye kujinasibu na uislamu (utambulisho).
 
Back
Top Bottom