Hapana, jibu lako linahitaji uzi mwingine zaidi ili uelimike kuhusu siri ya ukuu wa jina la Yesu kimamlaka.
Mungu mwenyewe kapendezwa tu kumpatia mamlaka hayo Yesu.
Sawa na Bakhressa alivyokaimisha majukumu yake ya kibiashara kwa mwanaye wa kiume kuyasimamia na kuyaongoza haimaanishi mwanaye Bakhressa ni mkubwa zaidi kuliko Bakhressa mwenyewe.
Pia unapaswa uelewe Yesu alikuja katika mwili kuonesha njia ya uzima wa milele jinsi Binadamu tunavyopaswa kuishi kiimani na kimatendo, na alitusisitizia Binadamu kuwa tunao uwezo kuishi maisha mema kitabia na kufanya makuu kuliko yeye Yesu aliyoyafanya hapa duniani.
YESU JINA LIPITALO MAJINA YOTE KIMAMLAKA.
WAFILIPI 2:9-11.
[9]Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
[10]ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
[11]na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
YESU NDIYE NJIA YA UKWELI NA UZIMA WA MILELE.
YOHANA 14:6.
[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Sent from my CPH2387 using
JamiiForums mobile app