Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Hakuna dini ya kweli na sahihi zaidi ya uislam...makafir vile chuki tu na husda zimewajaa
 
na
QURAN 5: 116-117

116.
Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa mwana wa Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu wawili badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Wewe umetakasika! Haiwezekani mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi Yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.

117. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu.


Nakushauri ndugu yangu uchukue japo muda kidogo uisome QURAN kabla hujaondoka hapa duniani kwani there will never be a second chance, JESUS WAS NEVER EQUAL TO ALMIGHY GOD! HE WAS A PROPHET JUST LIKE MUHAMMAD AND ABRAHAM AND MOSES AND ALL OTHER PROPHETS
Nakushauri soma biblia hapo kitabu Cha yohana mtakatifu chote .utaona uungu wa Yesu...

Kumfananisha Yesu ambae ni Mungu na kina Abraham, Mohamed,sijui mitume ni kumkosea heshima...

Mda bado unao ndugu!!! jitafakari
 
Imani zetu ziko kwa dini na madhehebu zaidi kuliko kwa Mungu. Ndio maana maisha yetu bado yamejaa dhambi pamoja na dini zetu. Biblia inasema "Mkinipenda mtazishika amri zangu." Yohana 14:15
 
Kwahyo huyo Yesu ana mamlaka makubwa kuliko Mungu?
Hapana, jibu lako linahitaji uzi mwingine zaidi ili uelimike kuhusu siri ya ukuu wa jina la Yesu kimamlaka.

Mungu mwenyewe kapendezwa tu kumpatia mamlaka hayo Yesu.

Sawa na Bakhressa alivyokaimisha majukumu yake ya kibiashara kwa mwanaye wa kiume kuyasimamia na kuyaongoza haimaanishi mwanaye Bakhressa ni mkubwa zaidi kuliko Bakhressa mwenyewe.

Pia unapaswa uelewe Yesu alikuja katika mwili kuonesha njia ya uzima wa milele jinsi Binadamu tunavyopaswa kuishi kiimani na kimatendo, na alitusisitizia Binadamu kuwa tunao uwezo kuishi maisha mema kitabia na kufanya makuu kuliko yeye Yesu aliyoyafanya hapa duniani.

YESU JINA LIPITALO MAJINA YOTE KIMAMLAKA.

WAFILIPI 2:9-11.

[9]Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
[10]ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
[11]na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

YESU NDIYE NJIA YA UKWELI NA UZIMA WA MILELE.

YOHANA 14:6.

[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa yangu alisilimu baada kutokea moto nyumbani kwa kaka yake alikokuwa anaishi, ukachoma kila kitu ndani Ila tu Msaafu ukabaki kama ulivyokuwa kabla ya moto.

Mwingine naye alibatizwa hata baada ya kula vidato vingi vya dini, kwa kuota msikiti wake kuwa chanzo cha mauaji makubwa na namna ya yeye atakavyoshiriki.

Kifupi ni kwamba; TUMEWAZOEA, TUMEWACHOKA, NA HATUHANGAISHWI TENA POROJO ZENU ZA BIBLIA NA QUR'AN. NA ANGUKO LENU LIPO KARIBU, KONDOO NYIE.
 
Imeandikwa: "Siku za mwisho wengi watajitenga na Imani, wakisikiliza hadithi zidanganyazo na mafundisho ya MASHETANI."

Kila heri, umeshakabidhiwa mwislamu mwezio wa kukulinda (jini)?
 
Kuna jamaa yangu alisilimu baada kutokea moto nyumbani kwa kaka yake alikokuwa anaishi, ukachoma kila kitu ndani Ila tu Msaafu ukabaki kama ulivyokuwa kabla ya moto.

Mwingine naye alibatizwa hata baada ya kula vidato vingi vya dini, kwa kuota msikiti wake kuwa chanzo cha mauaji makubwa na namna ya yeye atakavyoshiriki.

Kifupi ni kwamba; TUMEWAZOEA, TUMEWACHOKA, NA HATUHANGAISHWI TENA POROJO ZENU ZA BIBLIA NA QUR'AN. NA ANGUKO LENU LIPO KARIBU, KONDOO NYIE.
sasa cha ajabu nini kwa koran kutoungua moto? wakati imetengenezwa kiwandani tu kama vitabu vingine, au hata tungesema kuran ina nguvu nyingine ya ziada kwani hiyo inamaanisha ina nguvu ya Mungu? hata shetani ana nguvu, mbona hiyo ni sababu ndogo sana kukufanya upotelee kwenye imani potofu? kwani majini hayawezi kulinda kitabu chochote kile? kuna jirani yangu ni shehe, nakumbuka tangu tukiwwa watoto, yeye nyumba yake ikifika majira fulani lazima iungue moto. kama yanaweza kuanzisha moto, yatashindwaje kuzuia moto usichome kitabu? unajua ninyi mnavyoongea msiongee kana kwamba sisi hatuishi pamoja na ninyi na tunaijua imani na matendo ya dini yenu, tunawajua na tunaijua imani hiyo sana, na tunawaombea kwa Mungu awasaidie mfunguke macho.
 
QURAN IMEANDIKWA NA SHETANI MPINGA KRISTO NA NABII WA UONGO.

QURAN 2:97 - Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

ADUI WA MALAIKA WA MUNGU NDIE ALIYEITEREMSHA QURAN

1.JE ADUI WA MALAIKA WA MUNGU ATAKUWA NANI?????

2. JE ADUI WA MUNGU NI NANI????

JIBU NI SHETANI.

SITAMANI WAKRISTO JIJIFANANISHE NA HILO SHIMO LA KUZIMU UFUNUO 9.
Kumalamama'ako!
 
Mwanamume unajiita Queeni na picha ya Avatar ya Queeni.
Hata huko kwenye Uislamu sijui kama utafiti.
Kwenye Uislamu huo mwili ulio uweka wazi huwa unafunikwa na Ubaya.
 
Mwanamume unajiita Queeni na picha ya Avatar ya Queeni.
Hata huko kwenye Uislamu sijui kama utafiti.
Kwenye Uislamu huo mwili ulio uweka wazi huwa unafunikwa na Ubaya.
anamhitaji Mungu, arudi kwa Mungu wa kweli. amepotea huko.
 
True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una waislam tupu. nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.
Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu.
Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.
Allahu akbar.

PS: yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.

Mkuu endelea kujifunza uislam nazan mpk mda huu ujajutia uamuzi wako unaeza kua balozi mzuri wa kufundisha hawa vichwa ngumu wanaozani uislam ni vita
 
Back
Top Bottom