kwetu sisi tunaoamini Kristo Yesu, (najua wewe haukuwa mkristo, ni dini ile ila umeleta tu mada ili kujaribu kuvuta watu waingie kwenye dini yako, ndio maana haujui maandiko, mkristo yeyote anajua ni kwanini Yesu anaitwa Mungu, ), chukua tu mfano,
Yohana 1:1 inasema, Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu, huyo mwanzo alikuwa kwa Mungu, vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.
ndani yake ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu, nayo nuru yang'aa gizani wala giza halikuiweza. palitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu, Jina lake Yohana, huyo alikuja kwa ushuhuda ili aishuhudie ile nuru wote wapate kuamini kwa yeye. huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. kulikuwa na nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika umwengu. alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. alikuja kwake wala walio wake hawakumtambua. bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika kuwa watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina lake.waliozaliwa si kwa damu wala si kwa mapenzi ay mwili wala si kwa mapenzi ay mtu bali kwa Mungu. naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. ...kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa , neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
yapo mengi yameandikwa pale, nenda kasome. ili ukawafundishe na wenzako huko.