Hii ni ajabu ya Dunia. Wana CCM wenyewe hawajui ni kwa nini chama chao kinaitwa Chama cha Mapinduzi!

Nadharia yako nzuri na Bora Sana... Lakini haihusiani na CCM kuitwa chama Cha Mapinduzi. Nina HAKIKA na hilo kwa asilimia mia.
Ukisikia mtu anasema ana hakika na jambo kwa asilimia mia ujue huyo anabumbabumba.

Weka uthibitisho wa asilimia mia hapa.
 
Ukisikia mtu anasema ana hakika na jambo kwa asilimia mia ujue huyo anabumbabumba.

Weka uthibitisho wa asilimia mia hapa.
Wala sibumbi bumbi. Mimi niko "Verified" kwa ivo siwezi kusema nina HAKIKA asilimia mia wakati Sina hakika hiyo.

Ninajua kwa kuwa mimi ni miongoni mwa wanaojua ni kwa nini CCM inaitwa chama Cha mapinduzi.
 
Wala sibumbi bumbi. Mimi niko "Verified" kwa ivo siwezi kusema nina HAKIKA asilimia mia wakati Sina hakika hiyo.

Ninajua kwa kuwa mimi ni miongoni mwa wanaojua ni kwa nini CCM inaitwa chama Cha mapinduzi.
Mpaka hapa bado unabumbabumba tu kwa sababu hujatoa uthibitisho.

Nilitegemea uniwekee video hiki hapa kikao kilitoa jina kikataja sababu, au uweke waraka wa kukipa chama kipya jina unaoelezea jina limepatikana vipi.

Lakini unakuja na essentially habari za "trust me bro, mimi najua" 😂😂😂
 
TANU na ASP vilikuwa Vyama vya kupigania Uhuru

Vikafanyiwa Mapinduzi ya " kifikra" na kuunganishwa kuwa Chama Cha kuwaletea Maendeleo Wananchi

Tarehe 5/2/1977 nilisherehekea pale Shule ya Msingi Mirongo Mwanza na ndipo tulifahamiana na Shujaa Magufuli tukiwa Vijana Wadogo kabisa 😂😂🔥
 
Wewe kwa Magu ni kibabu... Wewe wenzako ni kina Mkuchika😀😆😃
 
Lengo la bandiko litafanikiwa kama nikiweka ithibati sasa hivi?

Ninachotaka ni wana CCM wenyewe waseme ni kwa nini chama chao kinaitwa *mapinduzi"?
 
Chama Cha Mazezeta
 
Somo zuri. Sikumbuki chanzo changu cha elimu hii, ila wakati wa Maafikiano ya TANU na ASP kutengeneza chama kipya, watu wa ASP waliweka sharti kuwa jina jipya la Chama lazima liakisi Mapinduzi kwani kwao ni alama ya utaifa wa Zanzibar na historia. Ndio msingi wa jina hilo.
 
Hili ndilo jibu. Kiranga .

Unadhani tarehe ya kuanzishwa Kwa CCM kulitokea Kwa bahati mbaya? Si ndiyo siku ya kuzaliwa kwa ASP?
 
Wana IQ ndogo
 
Baada ya TANU kuungana na ASP ndo kikazaliwa chama cha mapinduzi hiyo ni sababu mojawapo sina muda wa kuanza kubishana na wafuasi wa lissu
unajibu kindezi halafu unatoa povu
 
Hili ndilo jibu. Kiranga .

Unadhani tarehe ya kuanzishwa Kwa CCM kulitokea Kwa bahati mbaya? Si ndiyo siku ya kuzaliwa kwa ASP?
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kiitikadi imeongozwa na Makomredi kina Abdulrahman Babu na Kassim Hanga mwanzo kabisa. Hanga kasoma kwa wakomunisti Russia. Babu kasoma Marxism London. Ndio waliokuwa ideological strategists wa kina Karume.

Hao ndio waliomsoma Hegel na kuleta hizo habari za "Mapinduzi Daima" niliyoyataja.

Sasa huoni kuwa wewe umetaja Zanzibar na mimi nimetaja huko huko?

Wewe umeeleza neno Mapinduzi limetoka Zanzibar, mimi nimekueleza Wazanzibari wamelitoa wapi hilo neno. Hiyo dhana. Nikakueleza mpaka nilivyojiuliza kwa nini wanataka mapinduzi daima? Nikaja kuunganisha na Hegelian Dialectic ya Hegel.

Mpaka nimekuelezea habari za "Mapinduzi Daima" ambazo mtu akiyesoma Hegelian dialectic za Thesis-> Antithesis-> Syntheis, repeat again, aliyoyaandika Hegel, na Hegel alivyo influence Ukomunisti, na Wakomunisti walivyo influence Mapinduzi ya Zanzibar mpaka shuke zikaitwa Fidel Castro na Mao Tse Tung, ataelewa.

Huelewi wapi?
 
Chama cha mbogamboga
 
Hizo nadharia ulizoandika hazihusiani kabisa na kauli mbiu ya "mapinduzi daima".

Na hao kina Abdulrahman Babu au Kassim Hanga hawakuwa watu wenye ushawishi ASP.
 
Hizo nadharia ulizoandika hazihusiani kabisa na kauli mbiu ya "mapinduzi daima".

Na hao kina Abdulrahman Babu au Kassim Hanga hawakuwa watu wenye ushawishi ASP.
Hujathibitisha jina la Mapinduzi limetoka wapi kwa 100%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…