Dhana ya mapinduzi ni dhana ikiyopo sana katika falsafa za kikomunisti kutoka kwa Georg Wilhelm Friedrich Hegel.
Zamani miaka ya kati ya 1980s nilikuwa naangalia sana Televisheni ya Zanzibar. TV zilivyoanza kuingia Tanzania bara kwa wingi, TVZ ndiyo ilikuwa televisheni pekee, kabla ya CTN, DTV na ITV.
Kuna kitu kimoja nilikuwa sielewi. Kila TV ikifungwa usiku (ilikuwa inafungwa), kulikuwa na maandishi "Mapinduzi Daima".
Mimi nikawa nafikiri wanamaanisha Mapinduzi ya mwaka 1964. Nikajiuliza, hawa watu wanataka kupinduana na kuuana daima?
Baadaye, nilivyokuja kusoma falsafa za Hegel, nikakutana na kitu kinaitwa Hegelian dialectic. Thesis -> Antithesis -> Synthesis.
Unaanza na hoja. Wanakuja watu kuikosoa hoja. Baada ya kuikisoa hoja unajenga hoja bira zaidi.
Na hiyo hoja bira zaidi inakosolewa, na unatengeneza hoja ambayo imedidisha ubora.
Katika mfumo huo, unafanya "Mapinduzi Daima". Kwa sababu, ukizembea dunia itak Ukikubali kuwa mfumo wako wa kutumiana barua kwa pista ni mfumo bora kabisa, hauhitaji mapinduzi, utashindwa kujiongeza na kuvumbua email.
Kwa hivyo, vyama vya kikomunisti na kisoshalisti vina hiyo dhana ya Hegelian dialecyic ya Mapinduzi Daima.
Ndiyo maana hata CCM kinaitwa chama cha Mapinduzi.
It's Hegelian dialectic, at least in theory.