Hii ni nguvu gani?

Huwa naota napigana na Mimi ndo steringi na sijawahi kushindwa! Ikitokea nikapigwa ngumi hata moja tu natoka ndotoni nahairisha ndoto naanza kulaumu director wa ndoto! Hapo nageuka na upande mwengine naanza kuota zile ndoto nakimbiza mtoto wakike tukiwa uchi halafu anavyokimbia anakimbilia kwenye machaka!.

Ndoto zangu hadi raha..😀
 
Bashiri #50 ata comment nani kwenye huu Uzi wako, ili tuamini unabii wako wa ki Tito.
 
Enenda kwa wahenga wako.Unatakiwa urithishwe uganga wa kienyeji.Believe it or don't!😝😝😝😝
 
Unajua "deja vu" (hali ya kuhisi unaweza bashiri matukio yanayotokea) husababishwa na nini? Well! Ukielewa ni nini basi utagundua hiyo sio nguvu yeyote bali ni mchanganyiko wa uwasilishwaji taarifa katika ubongo, kiufupi ni tatizo la taarifa katika ubongo.

Hapo kuna matukio mawili (i)kupigiwa simu na (ii)kumuwaza aliyekupigia
Kilichotokea ni kumuwaza aliyekupigia na sio kupigiwa na uliyemuwaza. Kunawakati ubongo unachanganya mtiririko wa matukio.

Oups! Alafu nilipokuwaza tu nikaona uzi wako. I love charming intelligent ladies[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeandika concept nzito kwa lugha rahisi...Ingawa najua wengi wanaeza wasikuelewe. Naona hata mleta mada kama hajakuelewa vile, ndio maana hajawa interested na post yako.
Huenda sijaelewa, hebu nieleweshe zaidi
 
Its just a coincidence. Probability ya events kama hizo kutokea in a life time ni kubwa.

- Probability ya kukuta pilau sehemu unapoenda ukiwa unaifikiria pilau, ni ndogo lakini inawezekana. Sasa ukienda mara kwa mara miaka yote hiyo probability inaongezeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda sijaelewa, hebu nieleweshe zaidi
My dear CharmingLady naomba nikueleweshe kwa ufupi.

Hii hali unayoipitia ina uhusino wa karibu sana na Ngono + Pombe(ulevi).

Kuna nguvu fulani ya ajabu inayofanya akili yako itulie ( focus/ concentrate ) na kufanya mambo kwa ufanisi mkubwa sana. Nguvu hii inaongezeka kama ukiacha/ukipunguza kufanya mapenzi mara kwa mara na kuacha kunywa pombe hadi kulewa.

Naongea hivi nina ushuhuda imenitokea miezi michache iliyopita (angalia nyuzi zangu )na kuna mambo mengine mengi pia yalinitokea, nilikuwa na uwezo wa kuwasikiliza watu wawili wakiongea kwa mpigo hata kwa masaa mawili mfululizo kwa sauti ya kawaida (siyo kupayuka) tukiwa wote meza moja.

Hii hali ilianza kufifia baada ya kufanya NGONO na mwanamke na kutumia kilevi.

Ushauri.
Kama unaweza kuyaepuka hayo fanya hivyo. Pia fanya shunguli za kuufikirisha ubongo mara kwa mara na uwe unawaza vitu ambavyo unataka kuvifanya/kuvipata na ongeza imani yako kwamba lazima uvipate au lazima uvifanye. Mwisho kabisa hakikisha unakula chakula kiasi na upate MUDA MWINGI wa kulala.

Fanya hayo na utanishukuru baadae
 
Sure hata mimi hii hunitokea pia
Mtu sijawasiliana nae muda nikimkumbuka tu masaa 2 mbele simu au sms yake inaingia
 
Ni kwenye simu tu au na vitu vingine?
Kama ni simu tu, ujue umeshakariri mida ya watu kupiga
 
Ni kwenye simu tu au na vitu vingine?
Kama ni simu tu, ujue umeshakariri mida ya watu kupiga
Sio simu hata wakati mwingine naweza kumfikiria mtu ghafla anafika eneo hilo au namwona mbele yangu… Au nakutana naye, yaani mawazo yanatangulia macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…