Ndio maisha yalivyo mkuu, tunaishi kwa kutegemeana.
Shida ni mbaya sana hasa ukiwa masikini (sinamaana kwamba wewe ni masikini) Ni kauli jumuishi, Kiufupi umasikini ni mbaya sana.
Kwahiyo mkuu funika kombe mwanaharamu apite kiroho safi kabisa mi nakuona unanafuu, kwani unaweza ukaruka majivu ukakanyaga moto au ukaruka mkojo akakanyaga haja kubwa...
Chakuzingatiza ni kwamba huu mfumo upo kwa karibia watu wote sio wewe tu, ni vile umejua, lakini ukweli ni kwamba wanaume tunasaidiana kulea familia, hawa mama zetu wanasiri kubwa sana awe mama mzazi au mama watoto kunakuaga na wajomba flani hivi wasiorasmi waliotupiga tafu kwenye nyakati ngumu.