Hii picha ilipigwa mwaka 1843 na wamissionari wa Kiingereza walipofika Magila, Muheza

Hii picha ilipigwa mwaka 1843 na wamissionari wa Kiingereza walipofika Magila, Muheza

Nipo kwenye research juu ya kwanini miji ilikoanzia uprotestant au uislam ilikua sana kiuchumi kabla ya uhuru ukilinganisha na ile iliyokuwa dominant kwa catholic...

Natafuta connection iliyopo kati ya catholic na umaskini...
Kumbuka kiini cha imani ya Ukatoliki ni kujitoa kwa wengine na kukubali kuishi maisha ya kifukara. Wale walio utawani hata ukiletewa pair ya viatu kutoka kwa familia yako kama una pair ya kutumia muda huo vile unavigawa kwa mwenye uhitaji.

Fikiria unagawa pair ya Versace kisa wiki iliyopita ulipewa pair ya Bata.
 
Nipo kwenye research juu ya kwanini miji ilikoanzia uprotestant au uislam ilikua sana kiuchumi kabla ya uhuru ukilinganisha na ile iliyokuwa dominant kwa catholic...

Natafuta connection iliyopo kati ya catholic na umaskini...
Si vile. Je una takwimu ya kuonyesha?
 
Z

Barua za mwaka Gani? Kijana neno Tanga and Tanganyika ni ya Mjerumani baada ya kupewa kuitawala Tanganyika ya kale katika mkutano wa Berlin
Kwani pilika za mkwawa ni mwaka gani!!?..mkwawa akiwaandikia barua watemi wenzie kupambana na wageni
 
Soma kuhusu Magila: Magila - Wikipedia, kamusi elezo huru.
Ila matini katika post ya juu si kweli. Hii si picha ya 1843 (sijui picha ya kupigwa yoyote ya 1843 katika Afrika). Ludwig Krapf alianza kazi mnamo 1844 lakini pale Mombasa na Rabai.
Upo sahihi kabisa! Na kuonyesha kuwa mwandishi ni muongo wa kuokoteza habari za uongo ni kwamba hakuna Mzungu alikuja anaitwa Johan Krapf' Mjerumani aliyekuja alikuwa anautwa Ludwig Krapf kama ulivyoandika hapo juu. Mimi huwa nachukia sana mtu anayeandika uongo ili kuwarubuni wasomaji na hasa vijana wa sasa ambao hawajui historia hiyo kwa mapana!
 
ROHO INANIUMA SANA KWA HAKIKA MPIGA PICHA NA WOTE WANAOONEKANA KWENYE HII PICHA SIDHANI HATA MAKABURI YAO KAMA YANAJULIKANA YALIKO.
Hata wewe vizazi vjavyo havitakuja kuons kaburi lako, hivyo hakuna kuumia ndiyo mchakato wa maisha ya binadamu. Hata hao unaowaona kwenye hiyo picha hawakuwahi kuona makaburi ya waliowatangulia!
 
Kwanza tu kuonesha maneno uliyoandika hapa kwenye picha hii ni ya kutunga na uongo mkubwa, hakuna Mzungu aliyekuja Tanganyika alikuwa anaitwa Johan Krapf! Mzungu aliyekuja huko Magili alikuwa anaitwa Ludwig Krapf ( Mjerumani). Huyo Johan unayemtaja hapa alikuwa Mholanzi gwiji la soko la Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi ambaye amefariki mwaka jana! Sijaelewa kwa nini hata magwiji ya Historia humu JF hamjamrarua huyu jamaa! Kwanza mwaka huo 1843 anaosema hapa watu walikuwa bado wanavaa majani na magome ya miti!
 
Chakushangaza shule ya kwanza imeanza kwao muheza ila wapo nyuma kielimu kuliko maeneo mengine yaliyofuata kupata shule
Uko sahihi mimi ni mzaliwa wa hapo hapo magila msalabani napajua nje ndani ila mimi nimesoma bwana😂😂
 
Walutheri na Wakatoliki walielekea Lushoto, walipenda hali ya hewa, Anglicana walipenda kujenga Vuga lakini Mtemi Kimweri aliwakatalia. Muheza walipita kwa bahati tu wakielekea Malawi kutoka Lushoto, walipapenda sana na lakini wanakijiji waliwapa eneo la mwamba kuwakomoa. Matokeo yake walipasua mwamba na kutumia mawe kujengea kanisa, shule na hospitali.
Uko sawa kabisa na mimi nilipata ubatizo wangu hapo hapo kanisani
 
Kwanza tu kuonesha maneno uliyoandika hapa kwenye picha hii ni ya kutunga na uongo mkubwa, hakuna Mzungu aliyekuja Tanganyika alikuwa anaitwa Johan Krapf! Mzungu aliyekuja huko Magili alikuwa anaitwa Ludwig Krapf ( Mjerumani). Huyo Johan unayemtaja hapa alikuwa Mholanzi gwiji la soko la Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi ambaye amefariki mwaka jana! Sijaelewa kwa nini hata magwiji ya Historia humu JF hamjamrarua huyu jamaa! Kwanza mwaka huo 1843 anaosema hapa watu walikuwa bado wanavaa majani na magome ya miti!
Acha ubishi wewe. Anaitwa Johann Ludwig Krapf
 
Mi sio Mtaalamu wa soka,
Ila nilipoona waafrika wamevaa nguo nikajua Hii tayar Ni chai
images-541.jpg
 
Nipo kwenye research juu ya kwanini miji ilikoanzia uprotestant au uislam ilikua sana kiuchumi kabla ya uhuru ukilinganisha na ile iliyokuwa dominant kwa catholic...

Natafuta connection iliyopo kati ya catholic na umaskini...
Sure! Hata mimi ujiuliza, kabla ya uhuru ilikuwa hivyo lakini baada ya uhuru naona ni tofauti, je Catholic walifanikiwa vipi, uchumi wao ulichagizwa na nini?
 
Kwani pilika za mkwawa ni mwaka gani!!?..mkwawa akiwaandikia barua watemi wenzie kupambana na wageni
Hakika Mkwawa hakuandika barua. Hakuwa msomi. Tena hakushirikiana na watemi wengine.
Kinyume chake, alijenga milki yake kwa kushambulia majirani. Mwaka 1888 (mwaka wa vita ya Abushiri), Mkwawa alishambulia tena Wasangu na kupora Wakonde.
Mwaka 1890 alijaribu kuwasiliana na Wajerumani waliowahi kuendelea bara, baada ya kushinda Abushiri na Bwana Heri kwenye pwani mwaka 1889.
Maswasiliamo yalishidikana.
Mwaka 1891 kamanda Mjerumani Zelewski aliamua kushambulia Wahehe akashindwa huko Lugalo.
Wakati wa mapigano ya Mkwawa dhidi ya Wajeumani, Abushiri hakuishi tena na Bwana Heri alipatana nao.
 
Back
Top Bottom