Hii picha kuna kitu hakiko sawa: Mzee George Mkuchika amesimama vijana wamekaa

Hii picha kuna kitu hakiko sawa: Mzee George Mkuchika amesimama vijana wamekaa

Nimefikiria kuhusu suti,jibu nililopata ni hili "suti zimakaa kitapeli sana"
 
Hayo ni mambo ya itifaki ndugu. Itifaki haingalii umri.
Professor Nagu aliijua vizuri dhana ya itifaki. Mkewe Mary Nagu, akiwa waziri, alipotembelea IDM Mzumbe (sasa Mzumbe University) hakuwahi kusogelea meza kuu bali alikuwa anakaa na wahadhiri wenzake na watumishi wengine akisikilizia maelekezo kutoka kwa mkubwa. Ila kimoyo moyo alikuwa anawaza, ‘ngoja siku iishe, chumbani atajua mi ni nani’ 😁
 
Wengi hawamfahamu mzee George Mkuchika.
Ni mzee, kwanza alianzia kazi ya ualimu na baadaye kwenye siasa.
Nilimfahamu kupitia Mwalimu wangu aliyeitwa Chiwile ambaye sasa ni marehemu,
Mzee Mkuchika hana makuu,
Miaka yote hana scandal,
Hana kujikweza pamoja na utumishi wake ulio tukuka,
Aliwahi kuwaonya watu wenye madaraka wawe na kiasi,
Mzee Mkuchika ni mcha Mungu

Hao vijana waliokaa sasa .......

Kuna wenye fleet za mabasi,
Kuna wennye maghorofa kadhaa nchini,
Kuna weneye wake wengi kama mfalme Daudi,
Kuna wenye ukwasi wa kutisha pamoja na kwamba ni awamu zao za kwanza uwaziri.

Neno linasema;

Ayubu 12 : 12
12 Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.


Wananchi tuna wafahamu viongozi wetu.
Hizo haziwezi kuwa sababu za yeye kukaa hajakaa kwenye kiti kwa sababu za kiprotokali hapo hawakai eti kwa sababu hawana makuu au kwa sababu ni wacha Mungu ingekuwa hivyo hakuna ambaye angekaa. Yaani katibu mkuu kiongozi asimame mkuchika akae eti kisa Mkuchika alianza kama mwalimu! Au AG asimame Mkuchika akae eti kwa sababu Mkuchika hana mabasi🤣🤣🤣 au deputy PM asimame Mkuchika akae kisa Mkuchika hana scandal? Hapo hawakai kwa hisia wala huruma wala umri wala ujauzito.
 
Kiongozi hem edit uzi wako andika kilichopaswa kufanywa kulingana na sheria na taratibu.


Maana kwa upesi upesi mimi nadhani protocol ndozo zinaongea nani akae wapi na si umri.

Heb nieleze kulingana na protocol ipoje maana ukiongelea umri mkuchika angekaa kwa Samia hapo
Af akina kabudi, akina lukuvi pembeni yake sio ??
Mkuu upo sawa. Hapo kinachoangaliwa sio umri kama wanavyodhani vijana wasiomjua. Hapo ni Protocol ndio inafanya kazi! Maana kama ni umri basi inawezekana hata Rais akasimama sasa!
 
Namba 3 ni mwanasheria mkuu wa serikali mh johari
Owky protocali yule ni mjumbe asiyekua na kura kwenye Baraza. Naamini may be wangemsimamisha yeye halafu Mzee Mkuchika akakaa. Maana ni Waziri wa ofisi ya Raisi asiyekua na wizara maalumu. Na pia ni Mzee. Wengine waliokaa protocali zinataka wake na sio kusimama.
 
Owky protocali yule ni mjumbe asiyekua na kura kwenye Baraza. Naamini may be wangemsimamisha yeye halafu Mzee Mkuchika akakaa. Maana ni Waziri wa ofisi ya Raisi asiyekua na wizara maalumu. Na pia ni Mzee. Wengine waliokaa protocali zinataka wake na sio kusimama.
Itifaki hapo Lukuvi waziri mwandamizi baraza la mawaziri, karibu mkuu kiongozi kusiluka, mwanasheria mkuu wa serikali kwahyo kwenye mpangilio wa vyeo mzee mkuchika hapo alipaswa kusimama, kwasababu itifaki inapangwa kulingana na vyeo na ikitokea vyeo vinafanana wanapanga kulingana na uandamizi (kuwa kwny nafasi Kwa muda mrefu) mfano wanapokutana Marais. Mwenyeji atakaa kati Kisha wengine watafuata kulingana na kuwa muda mrefu madarakani
 
Hizo haziwezi kuwa sababu za yeye kukaa hajakaa kwenye kiti kwa sababu za kiprotokali hapo hawakai eti kwa sababu gawana makuu au kwa sababu ni wacha Mungu ingekuwa hivyo hakuna ambaye angekaa. Yaani katibu mkuu kiongozi asimame mkuchika akae eti kisa Mkuchika alianza kama mwalimu! Au AG asimame Mkuchika akae eti kwa sababu Mkuchika hana mabasi🤣🤣🤣 au deputy PM asimame Mkuchika akae kisa Mkuchika hana scandal? Hapo hawakai kwa hisia wala huruma wala umri wala ujauzito.
Kuwa na akili basibkuelewa kuwa mengine niliyosema ni just background informaton.
Kiprotokali kama unavyidai, mwanasiasa wa siku nyingi lazima awe juu ya mtendaji mkuu wa serikali.
Hilo halihitaji akili sana kulielewa.
 
Kwa huo mkao ni itifaki imezingatiwa na siyo suala la Mkuchika kuwa wa siku nyingi Ikulu. Hapo ni mpangilio wa kiitifaki tu na siyo blah blah unayotaka kutuchafulia bongo zetu hapa.
Hakuna cha itifaki wala nini, vijana kimbembele kingi bila kutazama uzito wa busara na hekima.
 
View attachment 3407042
Kuna kitu hakiko sawa, sijui kama nanyi wana JF mme note.

Waziri wa siku nyingi, mzee George Huruma Mkuchika ambaye yuko Ikulu miaka mingi, kiasi cha vijana wengi mawaziri kumuamkia shikamoo.

Kaachwa amesimama, wakati vijana wamekaalia viti!!
Kuna kitu hakiko sawa!
Mama naye kumbe haamini sana wanawake mbona wamejaa madume
 
Itifaki hapo Lukuvi waziri mwandamizi baraza la mawaziri, karibu mkuu kiongozi kusiluka, mwanasheria mkuu wa serikali kwahyo kwenye mpangilio wa vyeo mzee mkuchika hapo alipaswa kusimama, kwasababu itifaki inapangwa kulingana na vyeo na ikitokea vyeo vinafanana wanapanga kulingana na uandamizi (kuwa kwny nafasi Kwa muda mrefu) mfano wanapokutana Marais. Mwenyeji atakaa kati Kisha wengine watafuata kulingana na kuwa muda mrefu madarakani
Itifaki, my foot!
Kwani kuna itifaki zaidi ya kuheshimu umri in Govt service?
Kwani hapo mzee Mkuchika ame gate crah?
Vijana, give respect where it is due!
 
Wengine huko ikulu ni kazi ya store na kusoma magazeti nani akupe kiti cha mbele.

Kabineti ni wanaume watupu, huo usawa uko wapi ?
 
Raia wa nchi gani? kuna mpaka Waarabu na Wahindi(ambao ni raia) kwenye mfumo.
Nenda jimboni kwake uone anavyowabeba watu wanaotokea Hima Empire.

CDF Mkunda alikuwa sahihi aliposema tumekosea sana kuruhusu Wageni kuingia kwenye inner circles. Na hiyo ni sababu ya kwanini Paul Kagame ana jeuri sana.
 
Unafahamu nini kuhusu protocol?!
Ujinga wa vijana , matako hulia mbwata wakipata.
Hawajui thamani ya uzee wanapopata mihemuko.
Huyo mzee ana kazi ya kutuliza munkari kati ya makundi ndani ya "system".
Apewe maua yake.
 
Kuwa na akili basibkuelewa kuwa mengine niliyosema ni just background informaton.
Kiprotokali kama unavyidai, mwanasiasa wa siku nyingi lazima awe juu ya mtendaji mkuu wa serikali.
Hilo halihitaji akili sana kulielewa.
Unatumia uzeefu kubishana yaani kwamba mwanasiasa wa siku nyingi awe juu ya mtendaji mkuu wa serikali hiyo protocal ni ya wapi? Hapo wanatumia the order of seniority na seniority does not mean age seniority ya kimamlaka sio kiumri. Hiyo seniority ya kufanya kazi kwa muda mrefu inatumika pale ambapo wote wana vyeo sawa mf wote ni mawaziri hapo wangekaa kulingana na muda wa utumishi wao. Au mf wote ni marais Ataanza Museven,aje Kagame,aje Salva Kiir,aje Samia then aje Ruto.
 
wazee wanashika hatamu vijana mkalime
 
Back
Top Bottom