Hii Quotation ya leo inapasua anga, ardhi na maji

View attachment 3656114

“Mwenyekiti wetu, Freeman A. Mbowe akadai katiba mpya, akafunguliwa kesi ya ugaidi, akakaa gereza la Ukonga miezi 8, pale nilipowekwa mimi sasa.

Tukapambana na kesi ya uongo ya ugaidi. Wakamkuta na kesi ya kujibu. Siku ya kutakiwa kujitetea hatukumuona tena Mahakamani, bali akatokea Ikulu.

Hata jana nimesikia yupo huko Rufiji kwenye uzinduzi wa bwawa la Mwl, Nyerere, anahudhuria uzinduzi wa bwawa ka maji wakati mwenyekiti wake nipo kizimbani kwenye kesi ya uhaini. Mwenzetu yupo na mama.”

Tundu A.M Lissu, Mahakama Kuu, 24.08.2026
😁😁
 
Hizi rasta za Lissu zinanikumbusha kitu huko Kenya. Wakati wa vuguvugu la Mau Mau wafuasi wa Mau Mau walianza kufuga ndevu wakimuiga Mzee Jomo Kenyatta. Ishu hii iliwaudhi sana wazungu. Wakaanza kuwanyoa kinguvu wale waliofuga ndevu makambini.
 
Napenda sana jamaa anavyokuwwa updated na mambo yanayoendelea uraiani na duniani.

Sometimes haya mambo yanamuongezea chachu ya kuwa na ujasiri kujua amebeba matumaini ya mabilioni ya watu ambao wanamuunga mkono.

Lissu kupitia hii kesi naamini ni mwanzo wa ukombozi regarding na kitchoamuliwa huko High Court ila kama kuna siku yatafanyika mageuzi kwenye hii nchi basi jina la Lissu litakuwa namba moja kama chachu.
Hivi updates za nje anapewaga na nani?
 
View attachment 3656114

“Mwenyekiti wetu, Freeman A. Mbowe akadai katiba mpya, akafunguliwa kesi ya ugaidi, akakaa gereza la Ukonga miezi 8, pale nilipowekwa mimi sasa.

Tukapambana na kesi ya uongo ya ugaidi. Wakamkuta na kesi ya kujibu. Siku ya kutakiwa kujitetea hatukumuona tena Mahakamani, bali akatokea Ikulu.

Hata jana nimesikia yupo huko Rufiji kwenye uzinduzi wa bwawa la Mwl, Nyerere, anahudhuria uzinduzi wa bwawa ka maji wakati mwenyekiti wake nipo kizimbani kwenye kesi ya uhaini. Mwenzetu yupo na mama.”

Tundu A.M Lissu, Mahakama Kuu, 24.08.2026
Lissu at his vindictive best. Mbowe hakutokea Mahakamani kwa sababu kesi yake ilikuwa imefutwa. Alitokea rumande kwenda Ikulu kuitikia wito wa Rais. Angekataa wito ule, Lissu na wenzake wange bakia uhamishoni. Na mamia ya wafuasi wa Chadema wangeendelea kukabiliwa na kesi nzito wakiwa rumande.

Mbowe kuhudhuria hafla ya kitaifa hakumaanishi kuwa anamuunga mkono Samia kwa kila analo tenda. Ku insinuate hivyo kunathibitisha chuki aliyo nayo dhidi ya Mbowe. Na ndio maana Mbowe hana mpango nae kwa sababu anajua anapenda majungu na fitna. Yeye hakumuonyesha grace Mbowe wakati ana shambuliwa kwa nini aone ni haki yake kuonyeshwa grace na Mbowe? Mbona yeye alikutana na Rais Samia Brussels wakati Mbowe yuko rumande? Na walipiga picha ya pamoja baada ya mazungumzo yao. Tuseme nae alikuwa upande wa Samia wakati ule?

Ushauri wangu ni aachane na Mbowe, ashindanie kesi yake. Ana watu wa kutosha kumchafua Mbowe. Hawa ndio walioanzisha rumors kuwa Mbowe ni shahidi wa Jamhuri dhidi ya Lissu. Ovyo kabisa.

Amandla...
 
Wakati wenzake wanampigania kutoka jela kwa ile kesi ya uongo, na wenyewe pia wangeweza kufungamana kuwa kitu kimoja na watawala! Ila wao hawakufanya hivyo! Badala yake walishikamama naye mpaka mwisho.

Alichokifanya Mbowe ni kitendo cha ubinafsi, usaliti, usnitch, na undumilakuwili. Taarifa zinaonesha Mbowe anaishi Mikocheni (kilomita 5 tu kutoka kesi ya Lissu inapofanyikia)! Cha kushangaza hajawahi kuhudhuria kesi kwa zaidi ya mwaka sasa kama wafanyavyo viongozi na makada wengine wa chama! Ila kwenye uzinduzi wa bwawa la umeme (zaidi ya kilomita 700 kutoka Mikocheni) ameweza kuhudhuria!

Lissu yuko sahihi kumchana hadharani.
Ni mahali gani panaposema kuwa ni lazima Mbowe ahudhurie kesi ya Lissu?
Wakati wa kesi ya Mbowe, chama chake kiliongoza mapambano ya kumpigania. Wakina Ruge na wenzake walilala sana ndani kwa kuongoza maandamano (wao waliita jogging) kupinga kiongozi wao kubambikiwa kesi ya ugaidi. Kuna wakina mama walijigalala nje ya ubalozi wa Marekani wakidai hilo hilo. Wananchi walikuwa wanajazana kila siku nje ya Mahakama kufuatilia kesi ya Mbowe.

Kwa vile Chadema, Bawacha na Bavicha bado vipo wanazuiwa na nani kuandamana na kufurika Mahakamani kufuatilia kesi ya Lissu? Wakifanya hivyo watakuwa na impact zaidi ya Mbowe kwenda Mahakamani. Swali la kujiuliza ni kwa nini hawafanyi hivyo?

Ina maana hujui kuwa Mbowe bado ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema?

Yaani viongozi wenzako wa kamati kuu wanahangaika na kesi ya mwenyekiti wa chama ila wewe unakwenda kwenye hadhara za watesi?.
Mwenye Vandetta hapa ni Mbowe na siyo Lissu. It seems kushindwa uchaguzi kulimuuma Mbowe mpaka anamchukuia Mwenyekiti wake.
 
View attachment 3656114

“Mwenyekiti wetu, Freeman A. Mbowe akadai katiba mpya, akafunguliwa kesi ya ugaidi, akakaa gereza la Ukonga miezi 8, pale nilipowekwa mimi sasa.

Tukapambana na kesi ya uongo ya ugaidi. Wakamkuta na kesi ya kujibu. Siku ya kutakiwa kujitetea hatukumuona tena Mahakamani, bali akatokea Ikulu.

Hata jana nimesikia yupo huko Rufiji kwenye uzinduzi wa bwawa la Mwl, Nyerere, anahudhuria uzinduzi wa bwawa ka maji wakati mwenyekiti wake nipo kizimbani kwenye kesi ya uhaini. Mwenzetu yupo na mama.”

Tundu A.M Lissu, Mahakama Kuu, 24.08.2026
Aibu sana
 
Wakati ule tunampinga Kamanda Mbowe kwa kung'ang'ania madaraka ya uenyekiti wa chama, baadhi yetu (nikiwemo mimi) tulitukanwa sana humu jukwaani na timu yake. Leo ushahidi wa undumilakuwili wake umewekwa hadharani.
Muda/wakati ni kitu cha kuogopa sana.
 
Ina maana hujui kuwa Mbowe bado ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema?

Yaani viongozi wenzako wa kamati kuu wanahangaika na kesi ya mwenyekiti wa chama ila wewe unakwenda kwenye hadhara za watesi?.
Mwenye Vandetta hapa ni Mbowe na siyo Lissu. It seems kushindwa uchaguzi kulimuuma Mbowe mpaka anamchukuia Mwenyekiti wake.
Kuna mahali panaposema kila mjumbe wa Kamati Kuu ni lazima ahudhurie kesi ya Lissu? Na je wajumbe wote wanahudhuria? Na kumbuka kuwa ujumbe wa Kamati Kuu wa Mbowe hautokani na kuchaguliwa au kuteuliwa. As long as he is a member wa Chadema atakuwa mjumbe wa hiyo Kamati hata kama hatataka.

Kaka yake Lissu ( ambae ni CCM) alimshauri Lissu awe magnanimous in victory, lakini Lissu akampuuza.
Sidhani kama Mbowe anamchukia Lissu kwa sababu alimshinda katika uchaguzi. Kama ana mchukia, ni kwa sababu ya mambo aliyomfanyia kabla na baada ya uchaguzi. Lissu na wenzake wangefuata ushauri wa kaka yake, hali hii isingejitokeza.

Toa mfano wa vendetta ya Mbowe dhidi ya Lissu. Tupe mfano wa juhudi za Mbowe za kuhakikisha Lissu anashindwa katika uenyekiti wake. Kwa maneno mengine, onyesha namna Mbowe anavyo msabotage Lissu.

Mbowe ana haki ya kukubali mualiko wowote atakaopokea. Hahitaji ridhaa ya chama chake. Kuhudhuria ufunguzi wa mradi wa kitaifa sio usaliti. Kama ambavyo kutohudhuria nako sio usaliti.

Hitimisho:
Ulichokiandika hapa kinatokana na mtazamo wako! Hivyo nakushauri na wewe uheshimu mitazamo ya watu wengine wanaoamini kwenye team work, unity na collective responsibility. Usilazimishe mtazamo wako kuwa sheria au kanuni.
 
Wewe ndio unataka wote tuungane na cult ambayo wewe ni mwanachama. Nimepinga ulichoandika kutokana na ninacho kijua. Hamna mahali ambapo nimekulazimisha ukubaliane na mimi. Kwangu mimi hayo unayoita "team work, unity na collective responsibility" ni platitudes. Nyinyi ndio hamtaki watu watofautiane na mitizamo yenu. Mimi binafsi sijali kama utakubaliana au utapingana na mtazamo wangu. Makes no difference to me. Lakini nitaendelea kuwapinga wote ambao kwa mtizamo wangu wana spew uongo na fitna. Hiyo ni haki yangu kama ilivyo haki yako ku spew uongo na fitna. Kama unaona kuna mahali nimekosea mahali nionyeshe wapi nimesema uongo. Kama nitaridhika na hoja yako, sita sita kukiri makosa yangu na kuomba msamaha.

Amandla...
 
Back
Top Bottom