Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Ingekuwa vizuri zaidi kama ungeweka mawazo yako badala kutumia ya mtu mwingine.Hiyo kesi alifuta nani? ngoja nikutolee maoni ya mwamba mmoja mwenye anafikiri kwa kuona mbali naleta nukuu yake mazima akimjibu jamaa mmoja mwenye akili kama yako ''ubongo wako kama upo vizuri, basi jitahidi kuutumia vizuri. Hapo anaonyesha kuwa mahakama za Tanzania si huru, bali zinaingiliwa na ikulu yaani rais akiamua anaingilia mahakama. Kwa kesi ya Mbowe, tayari mahakama, ilikuwa imesema ana kesi ya kujibu. Hivyo rais alipaswa kuiachia mahakama iendelee hadi mwisho wa kesi na mahakama iamue, ila kuonyesha kuwa mahakama zetu ni matawi ya CCM, mahakama ilinyang'anywa mamlaka na rais kisha Mbowe akaenda zake ikulu na hata mahakama haikulazimisha, ili mchakato ule ufike mwisho wa uamuzi wa kisheria
Anayeleta mashtaka Mahakamani ni DPP. DPP ana haki ya kuondoa Mashtaka hayo Mahakamani wakati wowote bila hata kutoa sababu.
Mahakama haina haki au uwezo wa kulazimisha kesi iendelee kama meta mashtaka amesema kuwa hana nia ya kuendelea nayo. DPP akighairi ( nolle prosequi) ndio mwisho wa kesi. Utaratibu huo uko dunia nzima. DPP anaweza pia kughairi kuendelea na kesi ya Lissu. Akifanya hivyo, Lissu ataachiwa na atakuwa huru kwenda kokote anako taka. Baada ya Nolle Prosequi haiwezi kuendelea na kesi.
Hapa kwetu watu huwa wanatilia shaka matumizi ya Nolle Prosequi kwa sababu DPP anateuliwa na Rais wa JMT. Mara nyingi panakuwa na imani kuwa Rais ana uwezo wa kumuamrisha kufungua au kufuta kesi.
Bahati mbaya huyo uliye muamini hayuko vizuri sana katika mambo ya sheria.
Amandla...
