Tuliona wakati wa mbowe yupo ndani Lissu alikuwa analaani na kutaka haki itendeke sasa chakushangaza lissu ana siku 500 ndani ila mbowe hajatamka chechote kile kuhusu huu ukandamizaji....hili suala linafikirisha mno na mbowe ni mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya chadema kwahiyo huyo ni bosi wake...hata wewe itokee shoga yako anakupiga halafu mumeo akae kimya bila kukemea utajisikiaje binti yangu?
Ni kweli kuwa wakati Mbowe yuko ndani Lissu alikuwa anampigania sana. Watu wengi tuliamini kuwa wameshibana sana.
Watu wengi wanapuuza yaliyotokea kabla ya uchaguzi wa Chadema. Lissu alianza vijembe vya mafumbo kuwa Mbowe ni msaliti. Hata Msigwa alipodai Chadema inanuka, Makamu Mwenyekiti alimuunga mkono kwa kudai ana hoja na hoja zake zijibiwe.
Zikaja shutuma za Wenje kushirikiana na Abdul kutaka kumhonga. Hata wakati wa kampeni, Lissu alimuita Mwenyekiti wake muongo. Lissu alidai hadharani kuwa vyanzo vyake vya pesa havijulikani. Alisema hamuamini kiasi cha kutaka uchaguzi usimamiwe na watu kutoka nje.
Mara baada ya uchaguzi zikaanzishwa kampeni dhidi ya timu Mbowe waliobaki upande wake. Kuna wakina mama walisema kuwa walikaripiwa sana ilipojulikana kuwa walienda kumsalimia Mbowe. Sigrida aliandamwa baada ya kumshukuru Mbowe kwenye mkutano wa Bawacha mbele ya Lissu. Aliyekuwa Aidan Kenani aliyekuwa mbunge wa Nkasi aliambiwa kuwa hamna anachofanya kwa sababu tu alisimamia uchaguzi ambao mtu wa Lissu ( Lissu alitangaza wazi kuwa Celestine Simba ni mtu wake) alishindwa na mtu wa team Mbowe ( Sharifa alisema waziwazi kuwa yeye ni team Mbowe). Inawezekana pia kisa cha Heche kumchukia Kiwanga ni kwa sababu baada ya Kiwanga kushindwa katika awamu ya kwanza, wajumbe wakaanza kutumiwa ujumbe kuwa Kiwanga anawaomba waliompigia kura, wampigie Simba. Kiwanga akasimama hadharani na kusema kuwa ule haukuwa ujumbe wake.
Haya mambo na mengine bila shaka yalimuumiza Mbowe na kumfanya akose imani nae. Hiyo ikiwa pamoja na kuwa aliisha sikia kuwa Lissu, Lema, Wenje na Msigwa walikuwa na mpango wa kumuondoa wakati yuko rumande.
Ukweli ni kuwa uhusiano kati ya Lissu na Mbowe umeharibika kiasi kuwa ni vigumu kutibika. Nahisi Heche alipoonana na Mbowe suala hili lilizungumziwa na Mbowe akabakia na msimamo wake wa kutojihusisha hadharani na kesi ya Lissu. Inawezekana hili limechangia tamko la leo la Lissu mahakamani.
Kwa mawazo yangu ni kuwa kama kweli Chadema wanataka Mbowe ashirikiane nao, waonyeshe kwa kuwawekea speed governor wote wanao mkebehi ( pamoja na wale wa Nairobi). Baada ya hapo ndio Lissu na Mbowe wakutanishwe kuweka sawa mahusiano.
Ila kwa hali ilivyo, sidhani kama Mbowe atabadilisha msimamo wake wa hivi karibuni. Chadema waheshimu uamuzi wake na wamuache apumzike. Matamko ya watu kama Martin hayasaidii kitu.
Amandla...