Hii sasa dharau, yaani mimi wa kunialika mahafali ya mtoto wa chekechea? Kweli?

Hii sasa dharau, yaani mimi wa kunialika mahafali ya mtoto wa chekechea? Kweli?

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Yamenikuta jana asubuhi, mpaka sasa sijakaa sawa kwa fikra na hasira. Yaani na ugumu huu wa maisha, upandaji huu wa bei, bado mgao wa umeme na maji na ukaribu wa kufunguliwa kwa mashule eti mtu anakuja kukualika mahafali ya mtoto wake, eti anamaliza chekechea!

Hivi chekechea mtoto anahitaji hongera ya nini kama sio kumuingizia pepo la kupenda kurukaruka ukubwani!

Nimekasirika kweli!
 
Yamenikuta jana asubuhi, mpaka sasa sijakaa sawa kwa fikra na hasira. Yaani na ugumu huu wa maisha, upandaji huu wa bei, bado mgao wa umeme na maji na ukaribu wa kufunguliwa kwa mashule eti mtu anakuja kukualika mahafali ya mtoto wake, eti anamaliza chekechea! Pumbavu!

Hivi chekechea mtoto anahitaji hongera ya nini kama sio kumuingizia pepo la kupenda kurukaruka ukubwani!

Nimekasirika kweli!
😅 Kafanikishe furaha ya mtoto aiseeh
 
Na Leo graduation zilikuwa nyingi 😂😂
Mimi Sina mtoto wa kugraduate ila wazazi wa shule nzima tulialikwa, ni vile tu NIMEONA una ajenda zako ila ni RAHA sana ukiwaangalia watoto kwenye functions kama hizi.
Mungu akupe wepesi
 
Kweli ndugu... mimi huwa nikipita sehemu nikakuta watoto rika la pre-school wanacheza lazima nisimame nitazame burudani kwa muda. Hata nikiwa na shughuli zangu zitakazonitaka niende kwenye hizi huwa napenda nifike wakati wa mapumziko nifurahie. Kuna raha fulani hivi kuwatazama na yale makelele.
 
Back
Top Bottom