Hii sasa dharau, yaani mimi wa kunialika mahafali ya mtoto wa chekechea? Kweli?

Hii sasa dharau, yaani mimi wa kunialika mahafali ya mtoto wa chekechea? Kweli?

Kuna mama alimfanyia mwanae sherehe kubwa kweli baada ya kuhitimu kidato cha nne.

Tulikula, kunywa na kusaza. Matokeo kutoka mtoto kazungusha. Hadi leo yule mama akili haijakaa sawa.
 
Ukiona starehe ya mwenzio ya mwenzio inakuumiza ujuwe kuna tatizo sehemu
Sijaumizwa na haitotokea niumizwe na vitu vya watu kama hivyo, kama ni muelewa, utaona kuwa kilichoniumiza ni kualikwa....kuhusishwa.
 
Mda mwengine tujifunze kuthamini furaha za wenzetu. Kuna watu wako hivi.

Let’s say Ni jirani, unaweza kusema usimualike labda hapendi shughuli za watoto napo atasema huyu anatutafuta kipindi cha misiba tu kwenye raha walaa.

Mwengine huyo ni mtoto wake wa kwanza tena ukute kampata kwa shida. Acha afurahie kama amekukwaza msamehe. Hata wewe una vitu vyako unavipenda watu wanakuona wa ajabu.

Nimejifunza kumbe bado sijajua kuishi na watu😂 binadamu sijui hata umshirikishe nini aridhike😂 sasa akiwa na birthday utaalikika kweli?

Alafu kingine. Yeye amemfanyia mwanae mahafali ili kum encourage kwamba kila hatua ikipita tutakupongeza. Wanadamu mna roho gani.
Sawa!
 
We acha tu hapa na mtazama wife anavoshupaza shingo kuhusu hako graduation ka mtoto na huu mwisho wa mwaka .nime mwambia nikikupa hii pesa basi siku kuu utakula ugali
Safi kabisa
 
Yamenikuta jana asubuhi, mpaka sasa sijakaa sawa kwa fikra na hasira. Yaani na ugumu huu wa maisha, upandaji huu wa bei, bado mgao wa umeme na maji na ukaribu wa kufunguliwa kwa mashule eti mtu anakuja kukualika mahafali ya mtoto wake, eti anamaliza chekechea!

Hivi chekechea mtoto anahitaji hongera ya nini kama sio kumuingizia pepo la kupenda kurukaruka ukubwani!

Nimekasirika kweli!
Kata kipande cha sabuni kisindikize na coca bariiiid ili povu lake lifunike jukwaa
 
Huyu bwana NIMEONA aseme tu kama hana hela, na hasira za kukosa hela anajidai zimetokana na kualikwa kwenye sherehe ya mwanachekechea kumaliza uchekechea wake..!! Hivi ingekuwa yanafanyika hayo, si tungekuwa wote tunasubiria ile degree ya mwisho ndo tufanye sherehe..!!??? Maana kila level kuna ya juu yake ambayo ina mambo yasiyopatikana kwenye hii ya chini..!!
Chekechea imezidi ndugu
 
Back
Top Bottom