Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Mtu mwenye uwezo wa kulipa kodi ya nyumba laki 3 na nusu kwa mwezi uchumi wake ni mzuri asee ningekuwa mimi nahamishia maisha pembezoni mwa mji ambako maisha ni nafuu ndani ya miaka 5 ntakuwa nshajenga.
Japo kupanga ni kuchagua.
Tena huko pembeni mwa mji unaweza pata kiwanja kikubwa sana kwa mil 6 au 7 cha muhimu ni kuangalia huduma za muhimu zinapatikana na unaweza fika kwenye shughuli zako kwa wakati.
 
Tena huko pembeni mwa mji unaweza pata kiwanja kikubwa sana kwa mil 6 au 7 cha muhimu ni kuangalia huduma za muhimu zinapatikana na unaweza fika kwenye shughuli zako kwa wakati.
Sema sasa nje ya mji kwa sasa utapelekwa mbali mnoo..sio chanika tena ni mkuranga hko au tuseme kigambon ndani ndani hukoo 😁
 
Acha uongo banda hani la mil 20 kuku wa milioni 2. Kuna watu mnakuaga wachawi sana kwenye kushauri mtu . Sijui mnatokaga famikia za kishua sana au ndo kuhikweza tu.
 
Haya Ni mawazo ya kupuuzwa haya Ni mawazo Kama ya mdogo angu......
Unakimbilia kununua gari la gharama kubwa wakati huna kiwanja Wala nyumba....

 
Sasa rafik tunafanyaje !!?
Akili kumkichwa kama una uwezo kidogo nunua kiwanja hata porini jenga baada ya miaka 5 unaweza kuta kiwanja ulichonunua kwa 1.5m kinauzwa 15m. Kwa wakati huo utakua mjini. Kuna watu wanajidai kua hawawezi kuhama katikati ya mji but wana vyanzo vizuri vya hela. Wengine wana support toka kwenye familia zao.
 
Ni kwel kabisa
 
Tunapo feli mtihani wa maisha ni kukopiana wakati kila mtu anazaliwa na swali lake.
Sure mm najikomba hapa nijenge kijumba mpiji ndani ndani huko jamaa yangu anajicheka et porini. Kiwanja nimenunua kwa kudunduliza.
Kumbe babake ana viwanja kama 7 so unasubiriwa akili zikae sawa apewe kimoja aanze ujenzi hata akikwama suport ipo.
Nikimfuatisha huyo hali yangu baadae itakua je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…