Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Watu wengi wanateseka kwa sababu hawataki kukubaliana na uhalisia wa mambo kwa nyakati alizopo na ubinafsi baada ya kufanya mambo kwa ajili ya faida ya kizazi chako baada ya kujiwazia mwenyewe.

Sehemu unayoona ni porini kwa wanao patakuwa ni mji na watafaidika na uwekezaji huo hata sinza yalikuwa mapori ambapo walikuwa wanaishi watu walioshindwa maisha ya mjini lakini leo ni mji mkubwa.

Maisha ni leo na kesho.
 
aya mawazo yako ndio watu huwa mwishoe hawajengi kabisa,
Na haya mawazo yanatolewa bar mtu anapiga bia za 30k anatoka hapo anapitia samaki wa 20k anapeleka nyumbani "siku imeisha" kesho yupo tena bar.

Huyu kipato chake kiko vizuri. Anawaza akikaa pembezon mwa mji hatakula bata. Na ndo wengi wao hata kujenga ni shida.

Uiifuatisha mawazo ya huyu inakula kwako
 
Watu wengi wanateseka kwa sababu hawataki kukubaliana na uhalisia wa mambo kwa nyakati alizopo na ubinafsi baada ya kufanya mambo kwa ajili ya faida ya kizazi chako baada ya kujiwazia mwenyewe...
Kweli kabisa watu wanataka kiwanja cha 20*20 kwa mil 15 wanasahau hata huko vinakouzwa miaka 8 nyuma maeneo hayo yalikua yanauzwa ekari moja kwa laki 5.

Na wengi wanaosema hivyo hawana uwezo wa kujenga nyumba kwa wakati huo au wana suport za familia zao wanategemea
 
Na haya mawazo yanatolewa bar mtu anapiga bia za 30k anatoka hapo anapitia samaki wa 20k anapeleka nyumbani "siku imeisha" kesho yupo tena bar.
Huyu kipato chake kiko vizuri. Anawaza akikaa pembezon mwa mji hatakula bata. Na ndo wengi wao hata kujenga ni shida.
Uiifuatisha mawazo ya huyu inakula kwako
umeona eeh,
 
Kupata kiwanja cha kujenga nyumba hasa katika prime area ni changamoto kubwa kwa sisi tunao safiri kuelekea uchumi wa kati. Unakuta pango la mwezi unapokaa ni 350, 000, ukipiga hesabu kwa miaka miwili unaona ni kheri ujenge ya kwako...
wakati mwingine unaakili ungekuwa ccm ungekuwa diwani
 
Zote hizo ni aproach sahihi.
Watu wote hatuwezi endesha maisha kwa kutumia approach moja.

Mazingira yanatofautiana baina yetu ila ile tu kudhubutu kupanga tofali juu ya jingine ni shahada ya juu ya heshima.

Asilimia kubwa tunajenga nyumba ikiwa ninmatokeo ya kujinyima sana, wachache wanajenga nyumba kama asset ama uwekezaji.
Kupata kiwanja cha kujenga nyumba hasa katika prime area ni changamoto kubwa kwa sisi tunao safiri kuelekea uchumi wa kati. Unakuta pango la mwezi unapokaa ni 350, 000, ukipiga hesabu kwa miaka miwili unaona ni kheri ujenge ya kwako...
 
mimi bora nipange kuliko kuishi kwenye pagare aisee
Nyinyi ndio wenye support za wazazi/walezi.
Akili kumkichwa kama una uwezo kidogo nunua kiwanja hata porini jenga baada ya miaka 5 unaweza kuta kiwanja ulichonunua kwa 1.5m kinauzwa 15m. Kwa wakati huo utakua mjini. Kuna watu wanajidai kua hawawezi kuhama katikati ya mji but wana vyanzo vizuri vya hela. Wengine wana support toka kwenye familia zao.
Na hawa huwa wanawaponza wengi sana wanaotokea familia za kimasikini.
 
Tena huko pembeni mwa mji unaweza pata kiwanja kikubwa sana kwa mil 6 au 7 cha muhimu ni kuangalia huduma za muhimu zinapatikana na unaweza fika kwenye shughuli zako kwa wakati.
Cha muhimu nibarabara ya kufika huko na pia kukaa porini peke yako unaweza kuvamiwa na majambazi. Angalia idadi ya waliohamia.

Maji unavuna ya mvua unakusanya kwenye sim tank. Ukiwa na Sim tank 2 za litre 10,000 unakusanya maji ya kukutosha kwa miezi 5 hivi.

umeme unaweka solar kwaajili ya taa, kupika unatumia gas.
 
Watu wengi wanateseka kwa sababu hawataki kukubaliana na uhalisia wa mambo kwa nyakati alizopo na ubinafsi baada ya kufanya mambo kwa ajili ya faida ya kizazi chako baada ya kujiwazia mwenyewe...
Tumeishi na watu wanafanya biashara hazieleweki leo maandazi kesho mihogo baadae matunda mara anauza icecream.. anajenga porini huko na nyie na mishahara yenu mnabaki kupanga.

Muda unaenda unakaribia kustaafu unaanza kuhangaika kutafuta kiwanja wakati mwenzio muda huo ana wapangaji eneo kubwa anafuga na maisha yanaenda
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu. Mwaka 2003 nilikwenda kumtembelea ndugu yangu aliekuwa anaishi kibada.

Nilimwonea huruma na kumdharau maana alikuwa anaishi porini japo ni dar. Mandhari ya hapo ilikuwa ni full kijijini maana miembe, minazi, vichaka na wanyama wakichungwa maeneo hayo.

Alinishawishi kunikatia kioande cha eneo lake ili nianzishe ufugaji wa mbuzi ila nilimuitikia ili kumridhisha.

Baada ya hapo sikuwahi kumtafuta mpaka mwaka 2016 tulipokutana kariakoo na kuningangania twende kwake.

Loooh, ile sehemu anapoishi yule ndugu badala ya mashamba ni maghorofa mtaa mzima. Yeye mwenyewe ameweka mjengo mmoja hatari sana mpaka naona aibu.

Nilipopakataa bure wakati huo kwa wakati huu ukibahatika kupata plot ambayo iko wazi bei zina range 40m mpaka 80m. Kibada eneo panaitwa shangwe


mwenyewe
Waliojenga maporini ndo wapo mjini sasa. Kuna ndugu yangu mwaka 2007 alienda kujenga chanika porini tena alipata kiwanja 45*90 kwa 900,000tulimcheka sana. Sasa yupo mjini ana nyumba na frem za maduka.
Sisi bado tunakomaa na tunataka viwanja vya mil 15 tena kwa mkopo
Fainali uzeeni.
 
Back
Top Bottom