Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Cha muhimu nibarabara ya kufika huko na pia kukaa porini peke yako unaweza kuvamiwa na majambazi. Angalia idadi ya waliohamia...
Unafikiri mapori yanayoongelewa ni mapori hasa? Hapana kuna maeneo ndo yanaendelea unakuta nyumba zipo mbalimbali wao wanaita pori. Daladala mwisho saa 12 hakuna supermarket ndo kinawakatisha tamaa.
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu. Mwaka 2003 nilikwenda kumtembelea ndugu yangu aliekuwa anaishi kibada....
Acha kabisa mkuu kuna wazee wapo mjini hapa toka miaka ya 80's na 90's wengine wanashangilia wengine wanajuta je tofauti yao ni ipi? Hiyo kibada yanleo kiwanja 20*20 unakuta mil 12 wakati kuna watu walikua na chance ya kumiliki hata ekari 10
 
Unafikiri mapori yanayoongelewa ni mapori hasa? Hapana kuna maeneo ndo yanaendelea unakuta nyumba zipo mbalimbali wao wanaita pori. Daladala mwisho saa 12 hakuna supermarket ndo kinawakatisha tamaa.
Tena sehemu kama hizi ndiyo unaweza kujiongeza zaidi ukaweka container, unauza mahitaji muhimu.
 
ki ukweli hata mimi nikipata hela uwezi kunishawishi nikakae pembezoni mwa mji yaani nikateseke chumba cha elfu 40, sijui nikaangaike kujenga kanyumba akaeleweki polini uko.

big No izi hela namtafutia nan sasa mimi nitapanga apartment nzuri mjini uko nitajenga taratibu nikiwa mzee pembezoni mwa mji.

Duniani hatujaletwa kuteseka jamaani.
Hayo mawazo nilikua nayo hata mm ila mke wangu alikomaa nijenge huku nilipo na palikua polini kiasi ila kwa sasa pamekua town hasa.Ukikaa unasema ule ujana kaa pia ukijua kuna kuachishwa kazi kuna kuna kufilisika kampuni ukajikuta huna pa kushika ukabaki unatoa mimacho tu wakati ulikia unachezea pesa
 
Maeneo ya Dar sio y kudharau hata kidogo, leo mtu akikubembeleza ununue kiwanja kwa 2.5m usikatae hata kama ni shamba. Ndani ya miaka mitano utashangaa, tena ni vile tu mchizi ameharibu mambo, Ila viwanja kwa jiji la Dar haijalishi ni wapi.

Nilienda Tuangoma, hakika nilipapenda. Jamaa wananiambia 2005 viwanja viliuzwa 2.5m, leo hii huna 25...30m hukamati eneo, the place is really nice.
 
Maskini wa Kwamtogole anaeishi maisha sawa na tajiri wa Bura!!
Kupata kiwanja cha kujenga nyumba hasa katika prime area ni changamoto kubwa kwa sisi tunao safiri kuelekea uchumi wa kati. Unakuta pango la mwezi unapokaa ni 350, 000, ukipiga hesabu kwa miaka miwili unaona ni kheri ujenge ya kwako.

Umepata kiwanja kwa milioni 20. Bahati nzuri ulikua na akiba ya milioni 5, benki wakakupa milioni 20 mkopo. Rafiki zangu wengi walichofanya ni kujenga nyumba ya kujistiri nyuma ya kiwanja. Ina basic needs tu na kuhamia.

Mbele ya kiwanja anaweka banda la kuku hawa wa kienyeji na matuta manne ya mchicha. Hapo amepiga mahesabu ya kurudisha mkopo. Watoto wakilalamika wamechoka kula mchicha wanapozwa na kuku. Maharage ndiyo kubadilisha menu.
 
Back
Top Bottom