Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Hongera mkuu lkn binadamu hatufanani hasa ukizingatia background ya maisha pamoja na karma... so kila mmoja anajikuna pale mkono wake unapoishia
Labda umenielewa vibaya mkuu..msisitizo wangu hapo ni kwamba kwa kuwa mimi sikupenda nusu nusu haina maana haikua rahis..]
 
Kwa kijana ambaye ni mwajiriwa wa serikali au hata biashara ambazo si lazima uwe DSM nakushauri katafute plot/shamba mkoani….ukipata uwezo jenga huko huko. Dar es salaam ya leo imebadilika. Kama uwezo wako ni mdogo utayaona Maisha machungu kila siku.

Kuna mshikaji wangu alikuwa mwajiriwa hapa DSM kwa miaka kama kumi (shirika zuri tuu)..ila anaishi pembezoni mwa mji..hela anaipata lakini ndo hivo majukumu mengi. Alienda kwa boss wake..akamuomba amhamishie mkoani. Boss hakuamini. Jamaa akakomaa, akapata uhamisho akaenda mkoani. Kwa sasa ameshanunua kiwanja, alishajenga na watoto wanasoma shule nzuri tuu. Juzi alikuja hapa mjini kuchukua Rav4. Well siyo lazima kwamba kila mtu apitie njia hii ya mafanikio. Lakini ukweli ni kwamba DSM ya sasa siyo ya juzi. usipoangalia utaishi kwa machungu siku zote. Ingawa wengi tunakomaa mjini lakini ukiangalia kwa ukaribu wengi tunaishi Maisha ya ku-regret sana.
 
na umesahau vile vile kuna kufa,,ntajenga kipato kikiruhusu ila siwezi kujitesa kisa tu nijenge,,, unakuta mtu hali vizuri avai vizuri kisa tu anajibana ajenge mimi siwezi
Ni wachache sana wanaojenga wakiwaa wanahela kamili mkononi ,Wengi wetu tumeunga unga na kujinyima ndo maana leo tunaitwa baba mwenye nyumba .Mkuu kufa kupo ila ukifa si tunawatoto watarithi .Hivi hujisikii hasra kumpa laki saba ana milioni mtu km kodi huwazi .Pia uhuru unao kua nao kwako hata ukitoka na taulo ama watoto wanacheza kwao.
 
Mtu mwenye uwezo wa kulipa kodi ya nyumba laki 3 na nusu kwa mwezi uchumi wake ni mzuri asee ningekuwa mimi nahamishia maisha pembezoni mwa mji ambako maisha ni nafuu ndani ya miaka 5 ntakuwa nshajenga.

Japo kupanga ni kuchagua.
Nilifanya huu upuuzi. Nilihamia sehemu nje ya mji wanaita Bunju, nikapanga kwa 200,000, na nyumba ni nzuri tu kule ushuani.

Balaaa ni kwenye gharama za uendeshaji maisha huko nje ya mji. Mafuta tu ya gari ni 300,000 kwa mwezi hiyo ni minimum yanaweza kuzidi.

Hapo bado purukushani zingine..... Sasa nikaona si heri kuendelea kuishi huko huko katikati ya mji..... Maana gharama hazikwepeki. Ila unachoweza fanya ni kubudget matumizi yako vema basi.
 
True... ila hiyo 350 ni normal tu kwa wengi... kijiwen nina bwana mdogo mmoja 26 years tunapiga kazi yy analipa 900k.Mawazo yako haya hutakaa mshawishi...atakupiga makofi [emoji23]
350,000 ni nyumba kubwa sana hiyo pengine ni vyumba vitatu hata vinne kwa maeneo yetu haya ya tabata, kinyerezi,, gongo la mboto etc.

Kwa 200,000 hadi 250,000 unapata nyumba ya kisasa ya vyumba viwili. Safi kabisa....
 
ki ukweli hata mimi nikipata hela uwezi kunishawishi nikakae pembezoni mwa mji yaani nikateseke chumba cha elfu 40, sijui nikaangaike kujenga kanyumba akaeleweki polini uko.

big No izi hela namtafutia nan sasa mimi nitapanga apartment nzuri mjini uko nitajenga taratibu nikiwa mzee pembezoni mwa mji.

Duniani hatujaletwa kuteseka jamaani.
kwamba unabishana na maandiko yaliyo sema siku za mwanadamu aliye zaliwa na.mwanamke ni chache, nazo zimejaa tabu na mateso.

duniani tumeletwa tuhangaike,tuhangaishe kichwa ili kuishi vyema
 
350,000 ni nyumba kubwa sana hiyo pengine ni vyumba vitatu hata vinne kwa maeneo yetu haya ya tabata, kinyerezi,, gongo la mboto etc.

Kwa 200,000 hadi 250,000 unapata nyumba ya kisasa ya vyumba viwili. Safi kabisa....
Huyu dogolas bwana yy anakoish ni maeneo nje ya jiji kwasasa kwa mujib wa magufuli 😂😂..yy anasema anataka kuish quality life sio bora maisha...
 
Sema sasa nje ya mji kwa sasa utapelekwa mbali mnoo..sio chanika tena ni mkuranga hko au tuseme kigambon ndani ndani hukoo [emoji16]
MUNGU ametupa akili tuzitumie vema. Kila nyakati zina maamuzi tofauti.

Wakati hao wanawaza hivyo nje ya mji ilikuwa hapo goba, bunju mbezi, tegeta.

Now nje ya mji ni almost 45+Km one way kutoka town hadi eneo husika, nani anataka kutembea umbali wote huo....
 
Kupata kiwanja cha kujenga nyumba hasa katika prime area ni changamoto kubwa kwa sisi tunao safiri kuelekea uchumi wa kati. Unakuta pango la mwezi unapokaa ni 350, 000, ukipiga hesabu kwa miaka miwili unaona ni kheri ujenge ya kwako.

Umepata kiwanja kwa milioni 20. Bahati nzuri ulikua na akiba ya milioni 5, benki wakakupa milioni 20 mkopo. Rafiki zangu wengi walichofanya ni kujenga nyumba ya kujistiri nyuma ya kiwanja. Ina basic needs tu na kuhamia.

Mbele ya kiwanja anaweka banda la kuku hawa wa kienyeji na matuta manne ya mchicha. Hapo amepiga mahesabu ya kurudisha mkopo. Watoto wakilalamika wamechoka kula mchicha wanapozwa na kuku. Maharage ndiyo kubadilisha menu.

Tutafika kweli..kwa plan hizi..
 
MUNGU ametupa akili tuzitumie vema. Kila nyakati zina maamuzi tofauti.

Wakati hao wanawaza hivyo nje ya mji ilikuwa hapo goba, bunju mbezi, tegeta.

Now nje ya mji ni almost 45+Km one way kutoka town hadi eneo husika, nani anataka kutembea umbali wote huo....
Sure...ila sasa ndio huwez jenga tena mjini pamejaa labda uendelee kupanga na kubanana nyumba za uswahili hiz kama ww uwezo ni mdogo kitu ambacho binafsi sikukitaka kwa perspective ya malezi bora ya watoto kimaadili na changamoto za hapa na pale.

Pia currently maeneo yameboreka hivyo yako accessible in terms of miundo mbinu na usafir upo wa kutosha..

Kama financially upo sawa haina shida ..apartment zimejaa kibao everywher in town
 
kwamba unabishana na maandiko yaliyo sema siku za mwanadamu aliye zaliwa na.mwanamke ni chache, nazo zimejaa tabu na mateso.

duniani tumeletwa tuhangaike,tuhangaishe kichwa ili kuishi vyema
Akhela au kwa Mungu uko ndo kuna moto ndio sehem ya kuteseka kwa hyi binafsi siwezi kuteseka mara mbili dunian na akhela mbinguni/ nimechagua duniani nile maisha mazuri( bata) uko mbele hata nikichomwa moto sio mbaya
 
Ni wachache sana wanaojenga wakiwaa wanahela kamili mkononi ,Wengi wetu tumeunga unga na kujinyima ndo maana leo tunaitwa baba mwenye nyumba .Mkuu kufa kupo ila ukifa si tunawatoto watarithi .Hivi hujisikii hasra kumpa laki saba ana milioni mtu km kodi huwazi .Pia uhuru unao kua nao kwako hata ukitoka na taulo ama watoto wanacheza kwao.
nitajenga ila kitu kujinyima kuishi vizuri ili nijenge hapana kwa kweli siwezi
 
Asilimia kubwa ya wanaokomenti hapa inaonekena wapo chini ya 35yrs, ndiyo maana issue ya kununua kiwanja nje ya mji mnaona ni polini.

Mwaka 2016 kuanzia boko kwenda bunju nje ya barabara ilikuwa mithili ya poli, watu wengi walikataa viwanja maeneo hayo na baadhi walijenga na kuziacha nyumba mikononi mwa walinzi, kipindi hicho viwanja/mashamba yalikuwa bei rahisi sana.

Leo mnajua kinachoendelea na wale mnaokomenti kuwa hamuwezi kujenga nje ya mji, huko ni kukosa maono au akili bado hazijafunguka.

Kwani hapo unapopaita mjini kabla ya kuwa hivyo unadhani nani alianzisha makazi na leo unapafagilia?.
 
Hiz habar za kujenga nyumba ndog kwanza halaf et tutajenga kubwa baadae mimi nilishayakataa....unajenga kijumba cha kisela af matokea yke unajikuta unazeekea humo...kwanin usijipe muda tu ukiinuka unainuka mzima mzima?

Ndio yale unakuta mstaafu anajengea nyumba pesa ya pensheni. Si sawa sana sema tu ndio maisha. Binafsi naona ni bora nijenge bangaloo pagare complete nipige bati na kuingia nitai finish taratibu mdogo mdog kuliko kujenga kijumba kidogo na kukipiga finishing huku nina mpango wa kujenga nyumba kubwa baadae hapan

sisi wenye miaka 20-25 tunaoishi kwa wazazi mnatushaurije
Endelea kujifukiza na kunawa maji tiririka,🙄
 
Back
Top Bottom